Mume wangu katumiwa Valentines card na mwanamke mwingine

Dada Ishengomaf,

Mshukuru Mungu kwamba una chombo kilichoumbika na kupendeza mpaka kinapendwa na wanamke mwingine. Kutumiwa kadi mmeo kweupe (mchana ) ukiwepona wewe nyumbani siyo tatizo, tatizo kama mmeo atajitoa kimwili kwa kahaba huyo!

Mwombe Mungu apate moyo wa kukuthamini wewe kwanza. Nakushauri usilipize kisasi kwa kuwa ukakayekutana naye kimwili katika kulipiza kisasi, ndiye atakuambukiza ukimwi!!!
 
Hii stori inanikumbusha kamchezo ambako jamaa yangu mmoja alikacheza ili kumpima my wife wake baada ya kugundua kuwa ni mtu wa kuchemka sana kwenye vijimambo vidogo vidogo. Ilikuwa inakaribia siku ya kuzaliwa jamaa, alichofanya alinunua kadi mwenyewe posta mpya pale nikiwa nashuhudia kwa macho yangu akamuomba binti mmoja wa kisutu sekondari aiandike kwa hand writing ya kike kabisa plus maneno ya mapenzi yaliyomo kwenye kadi na mwisho akaweka.. I'll always love u'......G! akaiweka kwenye begi lake la laptop mpaka nyumbani...kama hujui vile akaweka begi kwenye kochi tu na yeye akaendelea na hamsini zake, bibie huku mara kafungua begi anataka kutoa laptop mh! anakutana na kadi......You can guess kilichotokea....Ukitaka zaidi nitakumegea kesho...!!! Baadhi ya wanawake wanakosa busara kidogo kwenye mazingira fulani...Mtu mzima hawezi kuleta kadi ya mpenzi wake wa kweli kweli hadi nyumbani otherwise hamtaki tena huyo mkewe....Tatizo wanashindwa kufikiria kwa mapana!!!
 
Source: http://mapenzibongo.blogspot.com/

Msaada kwenye tuta Mapenzibongo, Mimi nipo na mume wangu huu ni mwaka wa tatu saivi na tumebarikiwa kupata watoto wawili. Jana mume wangu amepata kadi ya Valentine kutoka kwa mwanamke ambaye simfahamu. Alikuja nayo mpaka nyumbani hajaifungua, na kwa bahati mbaya au nzuri mi nkaifungua na likuwa imeandikwa hivi, "Love is not finding someone to live with, It's finding someone you can't live without, wako D", kwa kweli hii imeniuma sana. Nikamuuliza hii inakuaje, akanijia juu nakunijibu ni mfanyakazi mwenzie wa ofisini wanafanya nae kazi na amempa kila mtu ofisini kwao. Hapa nilipo niko na dilema

Wewe nenda naye ofisini kesho ukamuone huyo mwanamama akueleze vizuri nia hasa na sababu ya kumpa mumeo VD card yenye maneno hayo. Hili ndilo litasaidia kuondoa dukuduku ndani ya moyo wako na ikiwezekana pia umpe kibano cha nguvu tu ili aachane na tabia za kuparamia waume za watu.
 
...duuuh, hata nawe kaka umetegeka? hapana, nadhani unatania tu :D
Inaonekana wengi humu wanaweza kurusha ngumi kwa ujumbe (mafumbo) kwenye khanga, ama kwa nyimbo za taarabu!
 
Angekuwa mke wangu (Nshomire wa pale Kikukwe kwa Waziba) moto ungewaka
 
...duuuh, hata nawe kaka umetegeka? hapana, nadhani unatania tu :D
Inaonekana wengi humu wanaweza kurusha ngumi kwa ujumbe (mafumbo) kwenye khanga, ama kwa nyimbo za taarabu!

Mhhh! Mkuu mama ana dukuduku zito moyoni mwake, kwanini aendelee kuishi na wasiwasi kwamba mumewe anachombo kingine nje badala ya kwenda kuonana naye mpaka kieleweke!? Fumbo mfumbie mjinga.....By the way pamoja na kufanya vibaya sana katika zile mechi nne vigongo bado tumo kwenye kinyang'anyiro cha EPL na chochote kinaweza kutokea :)
 
***mama tulia, nenda posta kachongeshe hii kadi...

'love is NOT all about falling in love but rising everytime you fall, I will always be yours forever' I love you my sweet husband'

Kisha utakapo lala iweke katika meza anayoweka ufunguo wa gari lake, au iweke katika dash board ya gari yake, au iweke katika meza/kioo ya/cha kuvalia.

Usimwambie kitu mpaka akuulize!

That's a very nice 'revenge'

Haya ndo maneno bana! diplomat in the making
 
***mama tulia, nenda posta kachongeshe hii kadi...

'love is NOT all about falling in love but rising everytime you fall, I will always be yours forever' I love you my sweet husband'

Kisha utakapo lala iweke katika meza anayoweka ufunguo wa gari lake, au iweke katika dash board ya gari yake, au iweke katika meza/kioo ya/cha kuvalia.

Usimwambie kitu mpaka akuulize!

That's a very nice 'revenge'
.....sio kila mtu ana gari!
 
Back
Top Bottom