Mume wangu kakata mawasiliano ya 'Chakula cha Usiku' kwa miezi 8, Nifanyeje?

Lonely heart

Member
Oct 21, 2011
46
20
Anadai sababu kuu ni mimi kutowatii dada zake hivyo ameamua kuhama chumba ili na kukata huduma ya chakula cha usiku kwa miez 8 sasa kunikomoa...

Ni kweli kabisa kuwa mimi na dada zake tumeshindwa kuelewana kabisa kutokana na wao kutaka kunipangia masharti nyumbani kwangu jambo nililolipinga kwa nguvu zote.

...Mume wangu yeye sijui anawaogopa au anawaheshimu hvy kila kitu wanampangia.

Nisaidieni nifanyaje mana uzalendo unakaribia kunishinda na kucheat siwezi kabisa na wala sitakaa niweze...

Nimejaribu kumbembeleza kwa kila khali lakini kasusa, WHAT CAN I DO MY DEAR FRIENDS? Maana upweke umenichosha
 
oh mamii ngoja nirudi muda si mrefu tuongee kwa mapana! The Boss will yu please tell her wat to do wakati mi naend kusonga ugali kisha nitaendelea utakapokuwa umeachia!
 
Last edited by a moderator:
Watafute wasimamizi wenu wa ndoa na uombe kukalishwa kikao kwa pamoja ili kupata ufumbuzi. Japo mi huamini kwamba namna njema ya kupata suluhu ya tatizo la kimahusiano li kwenu wawili.

Jaribuni kuvumiliana ktk mambo ya ndoa na never ever mtu kuingilia ama kuendesha ndoa yenu hata kama ni wazazi wenu, mmekubaliana kuishi wawili na si vinginevyo may be mwenzio hajakua kimaamuzi bt mweleweshe taratibu atakuelewa bt kama ni ngumu best man ni sehem nzuri kuanzia.

Pole sana!
 
Kama wewe ni housewife basi tafuta shughuli kwanza uwe unatoka na kurudi, itamfanya ajiulize 'chakula chako kinaliwa au la' huko nje...

Atakuwa makini kulinda hiyo
 
Aisee pole sana matatizo ya ndoa yanazidi kuongezeka hasa ndoa za siku hizi. Ukiona huelewani na dada zake basi hukubaliki ndani ya familia yao. Jitazame upya ni wapi umeteleza pengine ulilazimisha ndoa ndio maana hata mwanaume anakuwa upande wa dada zake kwa kifupi hamna mapenzi hapo.

Ndoa sio fasheni kama inavyochukuliwa siku hizi bali ni makubaliano ya pande zote mbili ikiongozwa na mapenzi ya dhati. Na kama hauzai lazima utapata mateso
 
hayo ya mpito tu,ndoa ndivyo zilivyo.inaweza hiyo ni kama sababu kwake,akawa na mtu pembeni.jee yeye hicho chakula anakipata wapi?msamaha gani huo usiosameheka?jaribu kumchunguza,ukiona ndio hayo hayo,waelezee wakubwa wake,na kama hataki kujirekebisha.amua ambayo ni sahihi kwako.jitu zima,kubembelezwa hata haipendezi
 
Duh! Kuna Wanaume wengine wa ajabu sana!!! Yaani matatizo ya mkeo na wifi zake badala ya kukaa chini na wahusika ili kutafuta suluhisho na hivyo kuleta amani ndani ya familia anaamua kususia nanihii na kuhama chumba!!!! Duh! halafu mke "akichepuka" kidogo katika hali kama hii na kama akigunduliwa yeye ndio bado atalaumiwa!!! Pole sana dada.
 
lonely heart bado unahangaika na mumeo tu (unless uniambie nakufananisha, maana nilishasoma thread zako za nyumba) kam akakunyima ujue kuna mahali anapewa kwa hiyo uamuzi ni wako kusuka au kunyoa.........


unge define kusuka au kunyoa
wengine tunafikiri umemshauri atafute kidumu labda lol
 
...Kwa maneno ya BT akili mkichwa...na dada kishasema uzalendo wa miezi minane bila nanihii unakaribia kufikia kikomo...yuko tayari kuvua jezi ya team yake na kuvaa jezi ya timu tofauti.

unge define kusuka au kunyoa
wengine tunafikiri umemshauri atafute kidumu labda lol
 
hah! ww unamwendekeza na hujui hata kumrubuni m2, hamia huko anakolala ukalale, akiamka nawe amka, akikaa nawe kaa, akirudi kule kwa mwanzo nawe rudi huko, ataona mnafanya utoto atakubali mlale, saa 8 za usiku muwekee mguu juu, mkumbatie then mwambie naomba...! hakyanan hasira kule, ukiwin nipe jb.
 
Pole shosty.. Mumeo lazima anapata hiyo chakula sehemu nyingine, hilo halina mjadala.
hata mimi ninaamini hivyo,na hakika nimekata tamaa na mapenzi naye yamepungua kabisa mana sipendi mtu mzinzi ila nashindwa nichukue uamuzi gani kujisaidia hisia zangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom