Mume wangu hataki kubadilika

lolyz

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
339
199
Jamani wana JF maji yamenifika shingoni,

Ni mume wangu nampenda na kumuheshimu sana ila kuna mambo yanayonikera,mda mwingine ananilazimisha nikae naye kwenye baa mpaka usiku sana nikimshauri kuwa inatosha twende nyumbani yeye anakuwa mkali na kuniamuru nichukue gari au tax nirudi nimuache yeye na mimi kwakuwa sitaki kumuacha inanilazimu kumsubiri mpaka anapotaka yeye kuondoka huwa inaniuma sana kiukweli.

Nimekuwa naye kwa miaka 10 sasa, tuna watoto wawili wadogo sana (under 5 yrs) ila anapenda sana kukaa kwenye ulevi mara nyingine harudi nyumbani ukimuuliza anasema alikuwa na marafiki zake nimemsihi mara nyingi aachane na mambo ya ulevi tufanye maisha kwaajili ya watoto wetu anajifanya anaitikia ila baada ya siku chache anarudia makosa yaleyale,na kuna wakati najiskia kuchoka kuishi naye na natamani nikaanze maisha mapya na watoto wangu nitafute nyumba ya kupanga na niondoke bila ya kumuaga ili afanye mambo yake akishamaliza ndipo turejee (kama atafanikiwa kuyamaliza) .

Tumebahatika kujenga nyumba moja ambapo ndio makazi yetu kwa kipato ambacho kimepatikana na biashara ambayo tuko share mr &mrs(kujenga kwenyewe ilikuwa kazi hataki ilibidi nifunge kwa maombi) toka tuhamie kwetu hamna cha maana ambacho amekifanya zaidi ya kulewa ,night club etc.yeye hajaajiriwa popote ila naumia maana yeye anafuja mali, mimi nimeajiriwa shirika binafsi (no security kama serikalini)huwa najiuliza sana ikitokea tatizo lolote watoto wale ntawaleaje?Nampenda naye hudai ananipenda ila sielewi mwisho wetu utakuwaje?

Naomba ushauri wenu jamani
 
Jamani wana JF maji yamenifika shingoni,
Ni mume wangu nampenda na kumuheshimu sana ila kuna mambo yanayonikera,mda mwingine ananilazimisha nikae naye kwenye baa mpaka usiku sana nikimshauri kuwa inatosha twende nyumbani yeye anakuwa mkali na kuniamuru nichukue gari au tax nirudi nimuache yeye na mimi kwakuwa sitaki kumuacha inanilazimu kumsubiri mpaka anapotaka yeye kuondoka huwa inaniuma sana kiukweli.
Nimekuwa naye kwa miaka 10 sasa, tuna watoto wawili wadogo sana (under 5 yrs) ila anapenda sana kukaa kwenye ulevi mara nyingine harudi nyumbani ukimuuliza anasema alikuwa na marafiki zake nimemsihi mara nyingi aachane na mambo ya ulevi tufanye maisha kwaajili ya watoto wetu anajifanya anaitikia ila baada ya siku chache anarudia makosa yaleyale,na kuna wakati najiskia kuchoka kuishi naye na natamani nikaanze maisha mapya na watoto wangu nitafute nyumba ya kupanga na niondoke bila ya kumuaga ili afanye mambo yake akishamaliza ndipo turejee (kama atafanikiwa kuyamaliza) .
Tumebahatika kujenga nyumba moja ambapo ndio makazi yetu kwa kipato ambacho kimepatikana na biashara ambayo tuko share mr &mrs(kujenga kwenyewe ilikuwa kazi hataki ilibidi nifunge kwa maombi) toka tuhamie kwetu hamna cha maana ambacho amekifanya zaidi ya kulewa ,night club etc.yeye hajaajiriwa popote ila naumia maana yeye anafuja mali, mimi nimeajiriwa shirika binafsi (no security kama serikalini)huwa najiuliza sana ikitokea tatizo lolote watoto wale ntawaleaje?Nampenda naye hudai ananipenda ila sielewi mwisho wetu utakuwaje?Naomba ushauri wenu jamani

Dada chunga chako ukimwacha akae peke yake ndo mwanzo wa kuchakachua.
Wewe komaa hata ikiwa mpaka asubuhi wewe msubiri tu si ulikubali kuishi kwa shida na raha!!
Wenzako wanagombea golden chance kama hizo hata out hawatolewi.
 
Kama ulivyofanya kwenye kujenga, fanya tena (maombi na kufunga). Sidhani kuna kitu zaidi ya hicho kitakachosaidia! Yeye ni mtu mzima, badala ya kutumia muda wako Kulea watoto (umesema wako under 5) utumia kulea baba mzima!
 
Asante Kaunga na Fidel80(kweli mpisi hakimbii moshi nimeipenda) unajua haya mambo ya familia kuna wakati unashindwa hata mtu wa kumweleza kwa kuhofia kuvunja heshima kwa jamii ila nimeona hapa kuna mawazo,asanteni sana mubarikiwe
 
lolyz kwanza pole sana lakin ningependa kujua mambo machache juu yenu:
  1. je wewe unatumia kilevi??
  2. huwa mnapata fulsa ya kuongea (kukaa na kujadili au kupiga story)?
  3. je akiwa kwenye bar huwa anakunywa kwenye makundi au??
  4. je ulishamhisi kuwa na mahusiano nje??
 
BPM
1.mimi imenibidi nijifunze kutumia kilevi japo siwezi kunywa kama yeye na nikinywa sana ni bia mbili,
2.Huwa tunapata kama wkend hivi
3.Hawezi kunywea nyumbani lazima awe kwenye makundi
4.Sijawahi kuhakikisha japo kuna wakati akipigiwa simu huwa hapokei na huwa sielewi ni nani
 
Unajua wanaume saa nyingine tunakuwa na viburi vya kijinga yakishaharibika tunawatupia lawama wake zetu,sasa umepata mke wakuweza angalau kukusindikiza kwenye bar nini kinamfanya asielewe hitaji la mkewe la kwenda kupumzika na kuwecheki watoto tena under 5? Huu ndo muda wa kulea watoto wenu kwa mapenzi ya baba na mama nadhani hajui impact ya kuwa-abandon watoto katika umri huu.Dada wewe komaa na maombi Mungu ashindwi lolote
 
unaweza kuni pm

BPM
1.mimi imenibidi nijifunze kutumia kilevi japo siwezi kunywa kama yeye na nikinywa sana ni bia mbili,
2.Huwa tunapata kama wkend hivi
3.Hawezi kunywea nyumbani lazima awe kwenye makundi
4.Sijawahi kuhakikisha japo kuna wakati akipigiwa simu huwa hapokei na huwa sielewi ni nani
  1. je huwa anapenda kunywa wiki nzima au cku kadhaa katika week??
  2. maongezi ninayozungumzia ni ya kila cku kama stori au kujadili matukio ya kila siku au kukaa pamoja mkaangalia tamthilia, taarifa ya habari etc
  3. je makunndi aliyonayo ni ya aina gani ya watu ulishajaribu kuwafahamu hao watu na yeye anawazungumziaje???
 
pole sana loyz.. Mungu akutie nguvu maana yeye ni mweza wa yote. Pamoja na mawazo mengineyo unayopokea. Usisahu na maombi pia ni muhimu kama wewe mwenyewe ulivyodhihirisha katika ishu ya kujenga. Hawa kina baba (baadhi yao) inabidi wafike mahali wabadilike kwakweli hizi pombe za kila iitwapo leo (daily) ni za nini? mtu akikosa kilauri siku moja ni kama kakosa hewa loh?! Badala ya mama ku tunza familia anakaa na wewe hadi ulewe mbaya zaidi anateseka especially kama yeye si mnywaji na hata kama ni mnywaji mijitu mingine inakunywa hadi inaanza siku ingine haitosheki. Very sorry, na hiki ni kilio cha kina mama wengi.. wanavumilia tu.
 
Tatizo sio kulikimbia, tatizo sharti litatuliwe na wewe mpendwa unatatizo hvo yakupasa kuangalia njia zakutatua tatizo lako,
1. Kaa na mume wako uzungumze nae juu ya madhaya ya anachokifanya kwa wakati huu
2. Zungumza nae juu ya mustakabali wa watoto wenu, kwasababu wakikua mahitaji yao yatakuwa makubwa kwahyo ni vema akipunguza ulevi au kuacha kabisa.
3. Zungumza nae juu ya madhara ya ulevi hasa unapozidi kipimo.
 
lolyz kwanza pole sana lakin ningependa kujua mambo machache juu yenu:
  1. je wewe unatumia kilevi??
  2. huwa mnapata fulsa ya kuongea (kukaa na kujadili au kupiga story)?
  3. je akiwa kwenye bar huwa anakunywa kwenye makundi au??
  4. je ulishamhisi kuwa na mahusiano nje??
BPM
1.mimi imenibidi nijifunze kutumia kilevi japo siwezi kunywa kama yeye na nikinywa sana ni bia mbili,
2.Huwa tunapata kama wkend hivi
3.Hawezi kunywea nyumbani lazima awe kwenye makundi
4.Sijawahi kuhakikisha japo kuna wakati akipigiwa simu huwa hapokei na huwa sielewi ni nani
 
Hili ni jaribu kwako na amini kuondoka kwako ndio kuvunja ndoa yako.
Zidisha maombi na Mungu atakufungulia njia.
Kupambana nae kwa njia za kibinadamu mtaishia kugombana zaidi.
Hakuna neno lililo gumu kwake.
Ubarikiwe.
 
Asanteni wanaJF wote kwa michango yenu nimepata mwangaza wa kushughulikia tatizo langu Sitaacha kuomba Mungu na siku moja ntawajulisha mafanikio ntayopata.though its not easy
 
Asanteni wanaJF wote kwa michango yenu nimepata mwangaza wa kushughulikia tatizo langu Sitaacha kuomba Mungu na siku moja ntawajulisha mafanikio ntayopata.though its not easy

asante kwa kutushilikisha maana siku zote fungua milango ya kupata mawazo ya watu katika kushughulikia matatizo
 
lolyz; Asanteni wanaJF wote kwa michango yenu nimepata mwangaza wa kushughulikia tatizo langu Sitaacha kuomba Mungu na siku moja ntawajulisha mafanikio ntayopata.though its not easy

Ni kweli dada yangu, mambo ya ndoa si rahisi kiivyo, ni kumuomba Mungu na kuvumilia. Usione watu wanazeeka wakiwa pamoja, wamepitia milima na mabonde. Endelea kumlilia Mungu ndo msaada pekee. Unaweza sema labda halikuwa chagua jema kwako kuolewa na huyo lakini unaowaona huko nje pengine wanaonyesha kukupenda inaweza kuwa worse zaidi ukikaa nao kama waume ndani. Banana tu dada, utashinda Mungu ni Mwema hakika.
 
Pole sana dada dumu ktk sala atabadilika, pia shirikisha wazazi wake, , aisee watu wanapata bahati wanaichezea, zipo kesi nyini za namna hiyo mwanaume akishathamini pombe hamtakaa mwendelee matokeao yako atakuletea mke mwenza na maradhi kwani faida ya pombe ndo hiyo, kama ww ndio mshika fedha mlimiti huyu bwana usimpe upenyo wa kuzishika yeye na kama mnashea ATM ndio balaa.na ww nakushauri usikae na baar kwani huko sio kumchunga tenga muda wako zaidi kukaa na watoto,mtoto hawezi kupata malezi memna kama sii kwa wazazi.
 
Mie nakushauri usiwe unaandamana nae kila siku coz atleast mmoja awe anabakia na watoto maana mlevi atataka kulewa kila siku, pia rudi tena kwenye maombi ya kufunga aache pombe, inaonekana ni mume mzuri tu ila pombe ndio imemtawala, kulewa kwa makundi huwa kunamaliza sana pesa aisee, maana round moja si chini ya 40000, embu fikiria mpaka asubuhi, na usichoke kumkumbusha umuhimu wa kuangalia maisha ya kesho ya watoto wenu na nyie wenyewe, mwambie he is not getting any younger, anazidi kuwa mtu mzima na wakati mzuri wa kujijenga ni huu
 
Back
Top Bottom