Mume wangu haniweki Profile Picha katika Mitandao ya Kijamii, nifanyaje?

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,689
14,596
Samahani hapa najua wanawake wooooote huku mtanichukia lakini I don't care 💃

Kuna mtu hapa analalamika kuwa mume wake haweki picha yake profile picha kwenye WhatsApp au Facebook hata Instagram

Mimi: Kwani lazima uwekwe?!

MTU: Ndio ili Dunia ujue kuwa Nina mume anaenipenda

Mimi: kwahiyo asipoweka picha yako hakupendi?!

MTU: Upendo umepungua🙄

Mimi: kwakweli namsapoti asilimia 100 mumeo kutokuweka wewe wala watoto wenu kwenye profile picha, maana NI ushamba na ulimbukeni mkubwa

Cha mwisho Mapenzi ya kweli hayapimwi kwenye profile picha za social medias..

Ivi kwanini midada ya sikuhizi ina ulimbukeni, kutokujiamini?!

Zamani mama zetu walikuwa hawana social medias, ina maana walikuwa hawapendwi??

Me nasema hivi mwanaume asiekuweka profile picha anakupenda zaidi kuliko anaekuweka🏃🏃🏃🏃
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom