Mume wangu ananipenda?

tankibovu

Member
Jan 5, 2010
42
16
Nimeolewa miaka saba iliyopita, ila mpaka leo sina hakika kama mume wangu ananipenda kweli au la. Amebadilika mno. Kwa miaka 5 hivi hajawahi kuniambia 'i love you' au kunitajia kitu chochote romantic. Mapenzi yetu yamebadilika sana unaona kama vile anakuwa na wewe kutimiza wajibu tu haonyeshi feelings zozote. Tofauti na jinsi tulivyokuwa tukifanya mapenzi kabla hatujaoana.

Kwa vile nafanya kazi yenye kipato, basi kila kitu najifanyia mwenyewe hata nikiwa mjamzito matibabu yote najigharamia. Hivi ndio inavyokuwa hivi kwa wanawake wote au mimi tu? Nikimwomba anifanyie kitu kama kunisindikiza hospitali mpaka nimbembeleze au anasema hana hela inabidi aendee ATM. Hata nikiumwa hakuna cha pole wala nini. Ananisikiliza tu navyolalamika na kuniacha hapo.
Nimejitahidi sana kumweleza ninavyojisikia akifanya hivyo lakini inaonekana haimsumbui.

Sasa nimeamua kukaa kimya tu na kupeleka mapenzi yangu kwa watoto. Ninampenda sana Mume wangu lakini naona sasa kama nimeanza kuwa mgumu rohoni.:A S embarassed:
 
Pole sana...Kama wazazi wa pande mbili bado wako hai basi washirikishe katika hili ili kurekebisha hali ambayo huipendi katika ndoa yenu au washirikishe ndugu wa karibu toka pande zote mbili....Kuwemo kwenye ndoa ambayo haina mapenzi kwa kweli inatia unyonge sana na unaweza hata kufikiria kuivunja ndoa na kuwa mwenyewe.
 
Kama hakucheat wala kukukosea heshima, vumilia labda ndio style yake ya kupenda, ongea nae kwa utulivu vile unavyopenda awe, na wewe umfanyie vile unavyopenda kufanyiwa, ila hilo la kutokukusaidia matibabu linanitia wasiwasi...
 
Nimeolewa miaka saba iliyopita, ila mpaka leo sina hakika kama mume wangu ananipenda kweli au la. Amebadilika mno. Kwa miaka 5 hivi hajawahi kuniambia 'i love you' au kunitajia kitu chochote romantic. Mapenzi yetu yamebadilika sana unaona kama vile anakuwa na wewe kutimiza wajibu tu haonyeshi feelings zozote. Tofauti na jinsi tulivyokuwa tukifanya mapenzi kabla hatujaoana.

Kwa vile nafanya kazi yenye kipato, basi kila kitu najifanyia mwenyewe hata nikiwa mjamzito matibabu yote najigharamia. Hivi ndio inavyokuwa hivi kwa wanawake wote au mimi tu? Nikimwomba anifanyie kitu kama kunisindikiza hospitali mpaka nimbembeleze au anasema hana hela inabidi aendee ATM. Hata nikiumwa hakuna cha pole wala nini. Ananisikiliza tu navyolalamika na kuniacha hapo.
Nimejitahidi sana kumweleza ninavyojisikia akifanya hivyo lakini inaonekana haimsumbui.

Sasa nimeamua kukaa kimya tu na kupeleka mapenzi yangu kwa watoto. Ninampenda sana Mume wangu lakini naona sasa kama nimeanza kuwa mgumu rohoni.:A S embarassed:

Hiyo tabia haijakaa vizuri, au ulimlazimisha muoane? bila shaka ulimlazimisha muoane au kuna kitu kibaya umekuwa ukimfanyia na amekuwa akikuonya husikii hivyo amekuchoka lakini hataki kuvunja ndoa yake. Kaa naye chini seriously muombe akuambie kuna Tatizo gani.
 
dada yangu kweli nimesoma thread yako nikapatwa na simanzi...ila nachoweza kukushauri ni hiki.

Katika mapenzi wanaume walio wengi huwa wako active sana wakati relation ikiwa mbichi yaani hamjaoana na mnapooana mapenzi hupungua( physically) japo hali halisi ya kukupenda kama mke wake ipo palepale.

cha kufanya kaa nae yeye mwenyewe umweleze ni jinsi gani mlipendana wakati mkiwa hamjaoana na sasa halafu mwambie kitu kimoja " kuwa busy na maisha haimaanishi kuwa mbali na ndoa yako kifikra na kimwili pia" mara nyingi ukitoka kazini mpigie simu mkutane mahali furani amba[po sio kawaida yenu kukutane hasa jioni mnakaa na kupiga story kidogo..hapo kuwa makini usikumbushie mambo ya home ambayo huwa hayapendi.

Weekend kama haendi kazini mpeleke beach mkiwa na wenyewe muoneshe unavyompenda na jinsi gani anatakiwa kukupenda. ninayo mengi sana ya kukupa lakini ngoja kwa leo niishie hapo..

Tatizo la mume wako anaweza kuwa na conflict in his mind ambazo hawezi kukwambia direct.
 
Pole dada, jaribu kuangalia network yake huenda kuna embea umepita hapo ambao yeye hawezi kukueleza direct. Ila ameamini moyoni mwake kwamba ni kweli. Mimi la kuwashirikisha ndugu naona ucheleweshe kwanza, jaribu kucreat story zinazofanana na hali yenu then uje usikie atachangiaje then from there unaweza pata angalau idea ya ufanyeje. Othewise pole sana na yako ni cha mtoto kuna wenzio hata unyumba hawapewi achilia mbali matumizi
 
Pole mpenzi, sina hata cha kukushauri zaidi ya kukuombea. Maana mimi nisipoambiwa hivyo kwa siku nzima naumia saana!

Mshauri aingie JF anaweza jifunza kitu! Ila haya mapride ya wanaume yanakera mpaka basi.
 
pole sana ila inauma miaka 5 bila i love u au hata kijisifa kidogo jamani
ila kama unania na kumbadilisha muwe kua kama zamani hujachelewa jitahidi sana kumuonesha kwa vitendo hata cku karudi home anakuta dinner imezungukwa na mishumaa,kitanda kiko kiromantic,bafuni kunanukia na unazama naye huko kesho unabunia kitu kingine na ukifanya hayo yote usisahau pia kubadili mavazi yaendane na mtego wa siku iyo sina (sio kwamba mtu akishakuoa ndio unaacha kumtega yani unafanya ivo kila siku mpaka kifo kiwatenganishe) trust me mumeo anatakiwa akuone mpya kila siku ....maneno mengi sina ila kama uko kweli serious ni PM nikupe maujanja ya kumrudisha mumeo kabla hajanyakuliwa huko nje ukaja na uzi wa kulia hapa
 
inasikitisha sana...... Wanaume halafu mtaani huko mkeo akisifiwa na wakamjali utalia kuwa wanawake ni wasaliti?

Nikirudi kwenye topic, umezungumza na mumeo? Anajua unavyojisikia?
 
Nimeolewa miaka saba iliyopita, ila mpaka leo sina hakika kama mume wangu ananipenda kweli au la. Amebadilika mno. Kwa miaka 5 hivi hajawahi kuniambia 'i love you' au kunitajia kitu chochote romantic. Mapenzi yetu yamebadilika sana unaona kama vile anakuwa na wewe kutimiza wajibu tu haonyeshi feelings zozote. Tofauti na jinsi tulivyokuwa tukifanya mapenzi kabla hatujaoana.

Kwa vile nafanya kazi yenye kipato, basi kila kitu najifanyia mwenyewe hata nikiwa mjamzito matibabu yote najigharamia. Hivi ndio inavyokuwa hivi kwa wanawake wote au mimi tu? Nikimwomba anifanyie kitu kama kunisindikiza hospitali mpaka nimbembeleze au anasema hana hela inabidi aendee ATM. Hata nikiumwa hakuna cha pole wala nini. Ananisikiliza tu navyolalamika na kuniacha hapo.
Nimejitahidi sana kumweleza ninavyojisikia akifanya hivyo lakini inaonekana haimsumbui.

Sasa nimeamua kukaa kimya tu na kupeleka mapenzi yangu kwa watoto. Ninampenda sana Mume wangu lakini naona sasa kama nimeanza kuwa mgumu rohoni.:A S embarassed:

pole sana ndivyo hivyo mkishaanza kuzeeka kwenye maloveee...
ngoja niendelee kumsikiliza kiba singo boy...
 
Angalia, asije akawa amehamishia upendo kwenye miradi ya maendeleo ambayo ni ya faida kwako wewe na watoto wenu, leo na siku za usoni.
 
we huna mapungufu? we unamwambia i love you?
au unapenda ww kudekezwa peke yako? anza wewe utaona mabadiliko
yawezekana unalishi lifestyle ya aina moja tangu mmeoana
jaribu kumpa visuprise kama kumtoa out hata kwenda picknic wekends
na hata mbuga za wanyama mnapokuwa likizo utaona mabadiliko makubwa
 
Pole mpenzi, sina hata cha kukushauri zaidi ya kukuombea. Maana mimi nisipoambiwa hivyo kwa siku nzima naumia saana!

Mshauri aingie JF anaweza jifunza kitu! Ila haya mapride ya wanaume yanakera mpaka basi.

i miss my Nyumbandogo Omosexy lol Kaunga....
 
Last edited by a moderator:
Nimeolewa miaka saba iliyopita, ila mpaka leo sina hakika kama mume wangu ananipenda kweli au la. Amebadilika mno. Kwa miaka 5 hivi hajawahi kuniambia 'i love you' au kunitajia kitu chochote romantic. Mapenzi yetu yamebadilika sana unaona kama vile anakuwa na wewe kutimiza wajibu tu haonyeshi feelings zozote. Tofauti na jinsi tulivyokuwa tukifanya mapenzi kabla hatujaoana.

Kwa vile nafanya kazi yenye kipato, basi kila kitu najifanyia mwenyewe hata nikiwa mjamzito matibabu yote najigharamia. Hivi ndio inavyokuwa hivi kwa wanawake wote au mimi tu? Nikimwomba anifanyie kitu kama kunisindikiza hospitali mpaka nimbembeleze au anasema hana hela inabidi aendee ATM. Hata nikiumwa hakuna cha pole wala nini. Ananisikiliza tu navyolalamika na kuniacha hapo.
Nimejitahidi sana kumweleza ninavyojisikia akifanya hivyo lakini inaonekana haimsumbui.

Sasa nimeamua kukaa kimya tu na kupeleka mapenzi yangu kwa watoto. Ninampenda sana Mume wangu lakini naona sasa kama nimeanza kuwa mgumu rohoni.:A S embarassed:
Ohh kumbe mlikuwa manafanya mapenzi kabla ya ndoa, nadhani hayo ndo yameleta dosari katika ndoa yenu :biggrin:
 
Dah!pole sn ndo maisha ya ndoa.zdsha kumpa malavdav kwa stail tofaut anaweza akakuelewa!
 
wakati mwingine mtu kukuambia anakupenda haimaanishi anakupenda kweli au kukujali...huyo mtu inabidi uongee nae aonyeshe roho ya ubinadamu...mtu akiwa anaumwa ni budi kumpa pole..leo hii hata jirani yako akisikia unaumwa atakupa pole sasa ka jirani anatoa pole kwa nini mpenzi wako asikupe pole?? vitu vingine ni tabia ya mtu.unaweza ukute anakupenda kweli lakini inabidi abadilishe tabia yake awe anaonyesha ile caring side yake ambayo sometimes inakua ngumu kuionyesha in public...or mbele yako
 
Back
Top Bottom