Mume wangu anaishi maisha ya hali duni huku pesa yote akisaidia ndugu. Nimkomboe au niwe kama sijui kitu

Huyo jamaa tunaendana naye kabisa,yaani mimi hela zote huishia kwa Ndugu.Nikiweka hela MPESA/TIGOPESA/BANK yaani mtu akilia shida palepale natoa.Inafikia kipindi unabakia na salio la nauli ya daladala pekee.
 
Lakini mambo mengine vipi, mfano, kudinya, anakusepetua vema? Au na huko napo hayupo anakuacha na lichichi zako kila kukicha? Pole sana, bhaa!
 
Kuna kulipa fadhila ila hiyo imekuwa too much..Cha kukushauri tu msaidie kivingine ila sio kuingia mkataba na shetani, hiyo VITA ni mbaya haina mwisho mzuri.
Hata kama kulipa fadhila sio hivyo ni bora wangesoma wao huko ni kumkomoa mtu
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽

Mi naona uachane nae tu, kama unasikitishwa na tabia yake
kuna watu wameumbwa na roho ya huruma sana ya kusaidia ndugu zao inaweza ikawa ata hajafungwa na mtu ila alipotoka kijijini kwao, motisha yake alikuwa anasema nasoma nipate kazi nisaidie ndugu zangu..kwani anakumbuka maisha alivyo yaacha huko.

Nakumbuka nilivyo enda kijijini mara ya kwanza nilipewa hadith za jinsi baba alivyo soma, bibi alikuwa anaenda kuuza mboga zake mjini atume kwa mzee hela, babu na mdogo wake walikuwa wanaenda kushinda maporini kuchoma mkaa illegally kwa maficho ili walipe ada. Alivyo kuja mjini alifikia kwa mjomba wake etc.

Sasa mtu kama huyu roho inamsuta asiposaidia kwao

But of course kusaidia kupita kiasi paka ukajisahau nako kuna shida ila sio ya level yakumfanyia shirk mumeo.
 
Nikushauri nenda kwa ndugu zako ukweni kisha waeleze jamaa anavyopata tabu. Wanaweza kupata roho ya imani wakalegeza. Kawaeleze yote bila kificho. Huku ukiwaomba ushauri jinsi gani mumsaidie.

Pls usiwaambie direct kuwa wao ndio chanzo. Wee waambie tu jamaa hafanyi maendeleo na hujui pesa anapeleka wapi hata vaa yake ni ya shida. So unahitaji msaada wao mumsaidie.
Weee usimdanganye hicho kitu asidhubutu, unataka siku asipowapa wamuakie wanaweza mwambia muache huyo mkeo
 
Nilishafanya hivyo lakin asilimia kubwa waliniambia mi Muongo sababu hela ya jamaa iko nje nje Sana haiwezekan ikawa kweli tena nikaambiwa usiendelee kuongea baba akakusikia hatokuamin na anaweza sema unayako nikafunga bakuli langu
Tena funga kabisa bakuli lako, nenda kama nikanisani piga magoti kwa Mungu amfungue akili yake sio yeye, hao ndugu zake watakugeuka piga maombi
 
Ningakua kimaslah sizan Kama ningekua natoa hell yangu namnunulia nguo, Wala nisingekua nanunua vitu ndan 80% ya vitu vilivyomo ndani kuanzia shuka mpaka vyombo nanunua Mimi Kama nipo kimaslah ningekua nanunua??? Si ningejiwekea hela zangu kwenye ac tu.....
Achana naye huyo yawezekana naye ndiyo tabia yake, watu wahuko tabia zao ndivyo zilivyo hata wajita thuuuu kama hivyo hivyo na midomo michafu balaa muombee afunguke ufahamu wake
 
Wanawake Mungu anawaona. Hutaki asaidie kwao? Una akili ww? Ww kwenu huwasaidii? Ni akilo gani hiyo? Unajua amesomea mazingira gan mpaka kuja kuhitim na kukutana na ww? Kisa tu unampa hiyo k yako yenye sura mbaya ndo iwe kigezo cha kumfany asisaidie kwao? Acha roho mbaya ww.
Na kwa taarifa yako hakuna mwanamke katka nchi wa kumbadilisha msukuma. Uhakika ninao mifano ipo
 
Wengine wanakuwa na chuki wa wake wa watoto wao,na hujaribu kuhakikisha fedha zote zinaenda kwao (wazazi)
Kama ulikuwepo na kama sio chaguo lao au kabila lao wanakuwa hivyo, yaani huyu Mme yupo upande hakumbuki chochote, kuna wazazi wamepinda asikwambie mtu
 
Ningakua kimaslah sizan Kama ningekua natoa hell yangu namnunulia nguo, Wala nisingekua nanunua vitu ndan 80% ya vitu vilivyomo ndani kuanzia shuka mpaka vyombo nanunua Mimi Kama nipo kimaslah ningekua nanunua??? Si ningejiwekea hela zangu kwenye ac tu.....
Muongo ww. Tena muongo mkubwa. Unajua maslai utakayopata endapo atakubaliana na roho yako chafu. Ndo maana roho imekuchafuka mpaka umekuja jamvini huku kuomba msaada jinsi ya kunufaika na msukuma. Yaan apao akuna cha mwanamke bali ni jini
 
Ulizia wafanyakaz wa tanesco watakuambia yet anapewa laki kwa ajir ya nyumba lkn nilimkuta anaishi chumba na sebule Sasa ndio tumepanga nyumba kubwa

Mfanyakazi ana pewa laki mmoja kwajiri ya nyumba kwa mwezi ???lakini anapo safiri yeye ni mkuu wa msafara ana lipwa laki na kitu kwa siku??? Yani pango la nyumba la mwezi lina zidiwa na allowance ya siku??? Kweli kupanga ni kuchagua
 
Kama mzazi ana watoto wengi na ikatokea akawa anabagua watoto kutokana na bifu walizozitengeneza watoto;haoni hasara wewe mmoja kupata hasara.
Mie nimeshuhudia pesa inachukuliwa kwa huyu halafu anapewa huyu wakati huo huo naye anakazi tu mwenzao kila shida anasukumiziwa yeye dada wanadanga huko watoto asomeshe yeye tena wao wapo kwenye nyumba zao huyu kapanga kazi yake kupeleka pesa tu
 
Kama ulikuwepo na kama sio chaguo lao au kabila lao wanakuwa hivyo, yaani huyu Mme yupo upande hakumbuki chochote, kuna wazazi wamepita asikwambie mtu
Ni kweli haya maisha yana changamoto;ndio maana kuna msemo ukiona nyani mzee ujue amekwepa mikuki mingi
 
Mie nimeshuhudia pesa inachukuliwa kwa huyu halafu anapewa huyu wakati huo huo naye anakazi tu mwenzao kila shida anasukumiziwa yeye dada wanadanga huko watoto asomeshe yeye tena wao wapo kwenye nyumba zao huyu zezeta kapanga kazi yake kupeleka pesa tu
Hilo uitwa kuandamwa na pepo la umasikini
 
Kuna kipindi nilikua ukwen...Kuna mawifi zangu 2 wameolewa nao walikuja kusalimia, tukiwa jikon mama akawa anawapa mbinu wanae wa kike za kuomba hela kwa Kaka yao ,wameolewa lkn mama anataka wanunuliwe nguo na nilazima
Yaani hujakosea ikifika sikukuu dada wanaanza kupiga simu watoto wanaomba nguo za sikukuu hapo yupo kwa mmewe na niwatoto wao wema gani huo wema ukizidi ni ujinga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom