Mume wangu anabaki na housegirl mpaka saa tano /sita NDIO ANAKUJA KITANDANI

mh huyo hg hadi hiyo mida anakua anafanya kazi gani kama si uonevu huo. mimi ni mama wa watoto zaidi ya mmoja nina house gal na nafanya kazi. lakini ikifika saa mbili kila mtu amemaliza jukumu lake. napika jioni nkitoka job au nadeki au osha vyombo na kuogesha watoto. na watu wakimaliza kula dada anaosha vyombo wakati mie nalaza watoto. saa mbili net kila mtu amepumzika. namtreat kama mwanangu maana najua nae anachoka sasa iweje mtu amfanye house gal punda hadi usiku wa manane na si ajabu anadamka saa kumi na moja afu bado alalame eti mumewe haji kitandani mapema aaalah. watu wanajidekeza sana na kuendekeza uvivu na ubwanyenye. kama hg anamudu kazi zaidi ya maza haus wacha amalizie na majukumu yako.
 
Nanyie mmezidi kuwatesa hao mabinti, mpaka tunawaonea imani. Unaamka asubuhi unamkuta H/g anafanya kazi, unaenda jb unarudi unamkuta anahenyeka mpaka unalala bado mtoto anafanyakazi tu! Huruma inakuingia ,.... Na mengine yanafuata.
 
Awe analala sebuleni kwa muda kwenye kochi, mume akienda kitandani ndo naye ahamie chumbani.
 
Simple! Awe anabaki na mume wake mpaka wote waende kulala the same time. Yeye anakimbilia kwenda kulala saa 3 kwa nini, kwani ye mtoto wa shule? Watu wazima mkienda kulala saa 3 watoto walale saa ngapi?
umenena sawa kabisa, kwanini usibaki na mume wake hadi huo mda? kama hawezi amwambie house girl akalale afanye hizo kazi morn.
kutowafuma siyo sababu dada kinga ni bora kuliko tiba
 
hiyo nyumba ambayo housegirl anafanya kazi mpaka usiku wote huo ni ya aina gani?huyu mama nae ana mawazo magando tu na mumewe labada atueleze kuna jingine ambalo linamtia shaka huwezi mpangia mtu mzima muda wa kulala kama anaona hiyo ni kero na yeye adijust muda wake sawa na wa mumewe.
 
Kweli dunia uwanja wa fujo!
Natamani nifanye collection ya threads za migogoro ktk ndoa hapa JF kisha niandike kitabu. Nategemea kuomba kibari kwa wahusika.
 
Mume wake akimmega house girl wake wa kulaumiwa ni yeye mwenyewe,Ajirekebishe ama sivyo housegirl atachukua kitengo chake
 
hiyo ngojea ngoje ya kila siku inaleta wasiwasi,
ila mpaka saa 5 au 6 HG anafanya kazi gani?
 
Huyo to me ndiye tatizo: yy anaingia kitandani saa 3 baada y kufanya nn? Kula, ku-check news au ? Na huyo HG anafanya kazi gani haswa usiku wote huo hadi saa 5 ? Wengine tukishakula msosi, unapumzika kidogo, check news ect then unakula matunda kidogo then labda ndiyo muda wa kuhakikisha banda la kuku limefungwa vizuri ect kabla ya kwenda chumbani. Wengine baada ya mlo hushushia laga au glass ya wine...! Sasa kama mke baada ya kula tu anakimbilia chumbani then hapo kuna tatizo... unless kaolewa 2 weeks ago..!

Ndugu zanguni pamoja na kwamba tunapenda aman kwenye ndoa bado nimeona kuna haja ya somo la ufahamu kuwepo kwenye maisha ya kila siku ya wanandoa...leo nilikuwa na kikao na ndugu fulani mmoja wao akilalamika mumewe amekuwa akiingia kitandani saa tano ama sita wakati yeye amekuwa akiingia saa tatu..baya akaenda mbali kwa kusema amekuwa akisubiri mpaka dada wa nyumban amalize kazi aingie kitandan mwake ndie na yeye unasikia amezima taa.......Ukiwa kama wewe kabla ya kuendelea unalimalizaje hili swala..NBHAKUNA SIKU ALIOMKUTA NA HGIRL WAKIBUSIANA AMA KUFANYA TENDO OVU...KWAKO MWANA MAPENZI WA JF
 
unaroho mbaya kumfanyisha kazi hadi usiku, then asubuhi labda saa 11 au 12 anaamka tena

labda mume wako anakuonaa una roho mbaya kama mie navyokuona huna hata aibu kuandika kuwa unamfanyisha kazi mtu na apumziki siku nzima

shauri yako labda ndio nyie wanawake mnajiona kazi za ndani hamuwezi kufanya hata kupika, unakula na kulala tuuuuuuu

sasa quality za mwanamke mumeo anaziona kwa housegirl

unalo unaloa ndoa inaondoka hiyo

badilika haraka
 
Huyo Mdada mbona anakua kama sio mtanzania mafunzo alopewa na Kungwi wake aliyasahau basi hata kufikia pia hafikiri? vp unamuacha mume ametoka kazini baada ya chakula ndio mnaanza kulizana yaliojiri na yatakayo fuata kesho wewe unamuacha unaenda kulala sasa unakumbuka shuka kushakucha! mumeo karudi kazini unamhashua kidogo nakupenda kwa sana tena unajitia hulali
kama yeye hayuko karibu yako kifua chake ndio mto wako,leo unamuachia paka sufuria ya samaki? kwambia ajirekebishe kama anaingia saa 5au 6 ampe mda ataingia saa9 kwanza hasa usingizi huo unaupataje bila yeye kukukumbatia unakimbilia kitanda tangu ulipoanza kulala hujatosheka? ebu mwambia aamkeeeeeeeeeeeeee alaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Mi naona mambo mengine wanawake katika ndoa ni kujitafutia tu matatizo. Inakuwaje kwamba kwa siku za hivi karibuni wasaidizi wa kazi za nyumbani maarufu kama housegirls wamekuwa ni tishio katika ndoa?? mbona miaka ya zamani mama zetu walikuwa wanaishi na hao hao housegirls vizuri tu na tena kunakuwa na mipaka? wao waliwezaje?? hii biashara mke unatoka kazini unaweka miguu juu kila kitu msichana afanye kuanzia asubuhi mpaka usiku mume anaona umekaa tu hujishughulishi kama mama mwenye nyumba inaharibu sana ndoa. mmezidi kujibweteka mlioko kwenye ndoa na msipobadilika ndo yale yale mume anaanza kumuonea huruma msichana kutokana na kazi nyingi na ndo ukaribu unapojijenga hapo. kama mke chukua nafasi yako. Mnanichosha kila siku kulalamika kuhusu housegirls. as far as am concerned once i get married inshallah i will be different from the rest of y'all complaining about these poor girls. :behindsofa:

Inshaaalaah ukija kuolewa uapte housegirl mwenye kheri na ww...., kwa maana hali ni mbaya mno...!
 
Huyo Mdada mbona anakua kama sio mtanzania mafunzo alopewa na Kungwi wake aliyasahau basi hata kufikia pia hafikiri? vp unamuacha mume ametoka kazini baada ya chakula ndio mnaanza kulizana yaliojiri na yatakayo fuata kesho wewe unamuacha unaenda kulala sasa unakumbuka shuka kushakucha! mumeo karudi kazini unamhashua kidogo nakupenda kwa sana tena unajitia hulali
kama yeye hayuko karibu yako kifua chake ndio mto wako,leo unamuachia paka sufuria ya samaki? kwambia ajirekebishe kama anaingia saa 5au 6 ampe mda ataingia saa9 kwanza hasa usingizi huo unaupataje bila yeye kukukumbatia unakimbilia kitanda tangu ulipoanza kulala hujatosheka? ebu mwambia aamkeeeeeeeeeeeeee alaaaaaaaaaaaaaaa!

Swadakta arabianfalcon..., M/ke atalala vp kabla ya mumewe hajalala...? kwa wale walioenda vizuri darasa la makungwi wanalijua hili vizuri. M/KE ni pumziko zuri kwa mume mara bada ya shuguli za kila siku. W/KW AMBAO HAWAZINGATIII HAYA, KILA SIKU WATAENDELEA KULALAMIKA KUWA WANAIBIWA NA HSGILRS.

Kuwa responsible ktk kila sehemu uliyoko. Jaribu kubalance muda wako wa kazi ili NYUMBA yako uihudumikie vizuri na sio kila kitu umuachie house girl. Kitu kama chai ya asbh ni jukumu kubwa sana kwa m/ke kumuandalia mumewe kuliko akiandaa housegirl ( najua hili wengi mtakataa. ila ukweli ndio huo) kama ww kweli umekaa na kungwi na akakuelimisha vizuri.

kwa leo napita tuuuuuu.......!
 
Usipende kuongeav kwa tigo yako unayokalia hiyo, we nawe si umwandalie chai mkeo? Huo ni umalaya wako tu, hata uandaliwe kila kitu unaenda kuchungulia nyuchi za nje shenzi typ.. Huo ndo mfumo dume!! Hujiulizi ni kwanini mwanamke afundishwe yeye namna ya kutunza ndoa? Jukumi ni la mwanamke au ni letu sote? Acha ushamba nyama we..
 
Mbona hujiamini mwanamke? H grl ni mtoto kama wanao na kwa muda wote awapo kwako wewe na mmeo mnawajibika kumulea ipasavyo.Mme kama mlezi hana kosa kukaa na hs grl hasa kama anaendelea na kazi.Kwa nini nyinyi familia mlale yeye mumuache akifanya kazi usiku wa manane peke yake?Hata hivyo kama huwezi mambo na haujui kulea atakuwa analamba hasari yako.Mm nakushauri nawe uwe unabaki mpaka amalize kazi tena msaidie amalize mapema ili upate muda wa kujisevia haki yako.
 
Nimependa mchango wako. Hapo kwenye bold kumenifanya nikupe credits. That is how men should behave. Ni kosa kubwa saaana; narudia saaana kwa baba mwenye nyumba kuwa karibu na h/girl no matter what!

Boss wa h/girl ni wife period; mume hana right ya ku comment on kazi za h/girl. Nitakustahi kama uta comment like unawaendekeza hawa ma h/girl (which is what my hubby always says) lakini useme ninawaonea hakyanani patachimbika.

Kwani huyo mwanaume kilema?

kama nawaonea awasaidia some of works, nawaonea wakati wewe wasoma gazeti na kuongeza mafuta through kitambi.

Narudia ma h/girl wengi wanapenda kufanya kazi in a flexible way. Mchana wanapiga umbea usiku wanapiga kazi. Otherwise tuwawekee sijuhi ndo inaitwa CCT ya kuwarekodi uone kama usiku watakuwa na mrundikano wa kazi.

Mkuu ndoa unayojaribu kuongelea ni ya kufikirika...Ndoa nyingi ziko namna hiyo ingawa baba hawezi kukaa sitting room kila siku na mama hawezi kulala saa 3 kila siku!!

Kama baba anajiheshimu basi atahakikisha haweki ukaribu wowote na Beki tatu kama kuangalia naye TV au sijui kumsubiri amalzie kazi. Na huyo mama atakuwa na matatizo kama hamjui mumewe. Kama anajua kuwa adabu ya mume wake ni ndogo, basi anaweza kuhakikisha anachunga mzigo wake hadi ufike salama...Ila hayo ni maisha ya hovyo zaidi ya utumwa!!
 
Mimi ndo maana nilijiwekeaga vigezo kabla sijaolewa, mwananume mwenye tabia za kibosi wala simwoni attractive at all. Anayetaka kuwa treated like a King kwangu mie hata awe na ela kiasi gani; siwezi vutiwa nae. I like simple men who don't mind nani kaandaa chai; who don't mind kunyoosha nguo zao na hata za wife sometimes, if that is a work they are good at and they enjoy doing.

Na asikwambie mtu wanawake wengi wana treat waume zao like Kings not out of love ni wafanyaje tu. My office mate alikuwa ana complain mumewe anataka apigiwe brush viatu na afanyiwe kila kitu na wife hata kama wife ni mgonjwa. Hataki mtu ashike nguo zake zaidi ya wife. Inahuu; mke ni mtumwa au your other half (your rib).

Usipende kuongeav kwa tigo yako unayokalia hiyo, we nawe si umwandalie chai mkeo? Huo ni umalaya wako tu, hata uandaliwe kila kitu unaenda kuchungulia nyuchi za nje shenzi typ.. Huo ndo mfumo dume!! Hujiulizi ni kwanini mwanamke afundishwe yeye namna ya kutunza ndoa? Jukumi ni la mwanamke au ni letu sote? Acha ushamba nyama we..
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom