Mume wangu anabaki na housegirl mpaka saa tano /sita NDIO ANAKUJA KITANDANI

Hahaha! Umeonae, yaan mimi nnavyopenda kulala, huyo jamaa angekuwa ndio h'band wangu sahizi labda wana mtoto na h'gal, ntaachaje kulala nimlinde mtoto wa mwanamke mwenzangu ambae sijui hata kitovu kilitupwa wapi? Huyo jamaa ana lake jambo asee, anasubiri h'gal amalize kazi ili amkague au?

hilo la kitovu ni thread tosha ya kuja nayo hapa jamvini. heri umenikumbusha, hii kitu ilileta utata mkubwa mtaani kwetu juzi kati.
 
Nimependa comment yako. Ila napenda tu akina mama wanipe majibu. Hivi ni sawa kumfanyisha house girl, ambaye ni minor, kazi kuanzia saa kumi alfajiri mkapa saa sita usiku kila siku - yaani siku saba za wiki? Hivi mahousegirl huwa hawafanyi mambo mazuri ya kupongezwa hata siku moja au ni kanuni za kawaida za kiutawala kuangalia makosa peke yake na kumgombeza? Je ukimpongeza housegirl mara moja moja kwa jambo zuri alilofanya utakuwa umekiuka kanuni? Am just being curious!

mkuu inashangaza sana kwa kweli, ila kama unataka ndoa ianze kuyumba au ikose amani basi anza kuleta kanuni zako za u-HR na kiutawala kwa hawa ma-HG, wallah mkeo hatakuelewa hata kidogo, hivi sijui huwa wanawaonaje hawa watoto / wadada wa kazi ... wana wa-under rate sana sana ... hv kazi nzito wanazofanya hawastahili kupongezwa?? hawa stahili kupewa shukrani?? me ilibidi nitoe darasa tu kwamba binti yeyote awaye wa kazi kama atakuwa ana-perform vizuri, kuanzia kazi za ndani mpaka matunzo ya watoto basi mwisho wa wezi ana ka-bonus kake fulani (offer ya nywele salon, hela, kununuliwa nguo, etc) ambacho wife ndo atakuwa responsible kuka-excecute mwisho wa mwezi baada ya a thorough review ... mwanzo ilikuwa shida lkn nashukuru baadae wife alielewa na tuliona mabadiliko makubwa sana katika utendaji wa dada yetu wa kazi ... hawa ni bin adam kama sisi tu jamani, na kazi wanazofanya ni ngumu hata kuzidi pengine zetu ... tuwaheshimu na nyie wake acheni uvivu, timizeni wajibu wenu kama mama wenye nyumba na sio "watawala" au "malkia" ... acheni visingizio visivyo na mashiko!
 
...lol,...mume si mlinzi wa familia? acheni ahakikishe usalama wa nyumba yake bana...
hata mimi nahakikisha usalama kwanza na wote wamekwenda kulala, ndio 'nahodha' naingia kulala!

Mbu ni sahihi kabisa, nahodha lazima uwe mtu wa mwisho kutoka kwenye chombo bana!!

kwake mama mwenye nyumba, chunga sana huo usingizi unaouendekeza utakuponza!!
 
Inaonyesha mume anahuruma sana. Sa we fikiria..HG awe mwenyewe hadi saa sita usiku wengine wote wanakoroma! Manyanyaso haya yanamfanya mme kutokutaka awe sehemu hiyo. Anamsubiri kwa nia njema. Tafadhali kazi za usiku wa kutisha zisitishwe nyote mlale mapema. Halafu hadi saa sita mumeo hajalala...watoto mnatafuta mida gani?
 
Ndugu zanguni pamoja na kwamba tunapenda aman kwenye ndoa bado nimeona kuna haja ya somo la ufahamu kuwepo kwenye maisha ya kila siku ya wanandoa...leo nilikuwa na kikao na ndugu fulani mmoja wao akilalamika mumewe amekuwa akiingia kitandani saa tano ama sita wakati yeye amekuwa akiingia saa tatu..baya akaenda mbali kwa kusema amekuwa akisubiri mpaka dada wa nyumban amalize kazi aingie kitandan mwake ndie na yeye unasikia amezima taa.......Ukiwa kama wewe kabla ya kuendelea unalimalizaje hili swala..NBHAKUNA SIKU ALIOMKUTA NA HGIRL WAKIBUSIANA AMA KUFANYA TENDO OVU...KWAKO MWANA MAPENZI WA JF

Baba mwemam huyu anahakikisha milango yote imefungwa na kila mtu amelala ndipo nayeye anaenda lala. Big up kwa mkuu!
 
chakula ya usiku kuliwa saa 3 hata hainogi kwa kweli...ndo maana mume anajionea bora achelewe kulala tu

chakula ipi jamani mmenichanganya kuweni wa wazi -panadol ama??
 
Nakwambia fanya yote usimwache mumeo na hgirl wa singida wanavyojua vya fasta yaani we ukiamka unakuta aanadeki ama kusafisha vyombo watu wamemaliza kwenye kochi kazi mapemaaaaaaaaaaa..aah nawaogopa mabinti wanavyojua mchuchumio loh
 
Haya mambo ya ma house girl waachieni wake zenu kama mnataka kuwa na ndoa za amani. It is a matter of choice H/girl or wife.

Mimi nina experience niliongeza h/girl ili wawe wawili wasaidiane kazi ili wasichoke. Lakini bado wanalala saa sita. Inawezekana hawana usingizi; kwa nini wakupe pressure. Kama hawajuhi kupangilia kazi zao kimpango wao. Mimi nina kazi za ofisi zinazonchosha pia.

From my research hawa ma h/girl huwa wanaangalia TV mchana kutwa wakiona wenye nyumba wanakaribia kurudi ndo wanaanza kufanya kazi that's why kazi zinakuwa zimerundikana.

Yes nakubali bonus ni muhimu. Tena mimi sitohi bonus naongeza mshahara maana bonus haiwezi kutegemewa ni kama mvua.

Haya ya mume kumuonea huruma h/girl ni uzinzi tu. Period!

Nimependa comment yako. Ila napenda tu akina mama wanipe majibu. Hivi ni sawa kumfanyisha house girl, ambaye ni minor, kazi kuanzia saa kumi alfajiri mkapa saa sita usiku kila siku - yaani siku saba za wiki? Hivi mahousegirl huwa hawafanyi mambo mazuri ya kupongezwa hata siku moja au ni kanuni za kawaida za kiutawala kuangalia makosa peke yake na kumgombeza? Je ukimpongeza housegirl mara moja moja kwa jambo zuri alilofanya utakuwa umekiuka kanuni? Am just being curious!
 
Ndugu zanguni pamoja na kwamba tunapenda aman kwenye ndoa bado nimeona kuna haja ya somo la ufahamu kuwepo kwenye maisha ya kila siku ya wanandoa...leo nilikuwa na kikao na ndugu fulani mmoja wao akilalamika mumewe amekuwa akiingia kitandani saa tano ama sita wakati yeye amekuwa akiingia saa tatu..baya akaenda mbali kwa kusema amekuwa akisubiri mpaka dada wa nyumban amalize kazi aingie kitandan mwake ndie na yeye unasikia amezima taa.......Ukiwa kama wewe kabla ya kuendelea unalimalizaje hili swala..NBHAKUNA SIKU ALIOMKUTA NA HGIRL WAKIBUSIANA AMA KUFANYA TENDO OVU...KWAKO MWANA MAPENZI WA JF

Mwambie mama huyo aache uvivu, abaki na baba hata mpaka sasa 6 sebuleni ili housegirl awe anawaacha pale wawili
 
wee kinachokuwaisha kitandani nini?endelea na kausingizi kako na wao waendelee na kamchezo kao,jocking bana
 
We ndo mzembe wa mwisho, utaendaje kulala wakati kazi ulizotoa huna uhakika kama zimeisha? ,Huyo hg anapumzika saa ngapi kama hadi saa sita usiku ndo anamaliza kazi? Huo ni unyanyasaji, mbona wewe huko kazini kwako unarudi mapema. Wanawake wengi mmekua na tabia hii mbaya kabisa ya kuwafanyisha kazi watoto wa wenzenu kama watumwa. Acha ushikishwe adabu ndo utapata akili:A S 465::A S 465:
 
mimi huwa najiuliza hili...
kwa nini housegirl aje kumfungulia mlango 'mume'????
why her?
kwa nini mama mwenye nyumba usihakikishe housegirl analala mapema
na unampiga marufuku 'kumfungulia' mume mlango??????
Hii iliwahi kunitokea. Kila nikirudi HG ndo ananifungulia afu anakuwa amepiga kanga moja, nikaona na udhaifu wetu wanaume itakula kwangu, nikapiga sura ya mbuzi nikapiga marufuku iyo tabia. Mpaka leo ni wife tu ndo anaruhusa ya kunifungulia. Unajua hatari nyingine wake zetu ndo wanazisababisha bana!
 
niliapa beki tatu ndani ya nyumba yangu marufuku....nsijepata kesi bure
We kuwa mvivu ka Mr wako halafu singizia beki 3 utashangaa..Unaleta tabia za umama zaidi wakati mzee bado anajiona chaliii..Atafuata beki 3 wa jirani.Sijui na jirani utamwambia amfukuze beki 3 wakeeee...teheeee..!!
 
..hapa nakiri kukutana na mchambuzi mwenye uelewa na mtazamo wa hali ya juu sana kuhusu maisha ya ndo,JS we mkali kwani ni mikono yao wenyewe huaribu ndoa zao,ati kila ki2 anifanyie hg ndo mana naamua kuutumia mda mwingi kuwa nawe,kama ilivyo tafsiri ya mapenzi sio kitandani tu panaleta umoja bali madogo madogo mengi ambayo mnaojifanya wajanja mmeyakabidhi kwa ma hg wenu..badirikeni basi lol!!..JS utakako kuwako ukawe na maisha bora na kama ni bado sana "I wish ningelikuwa wako"
 
Haya ya mume kumuonea huruma h/girl ni uzinzi tu. Period!

NK, kwanini ni vibaya kuwaonea huruma hawa wadada kwa kazi nyingi za siku (provided yuko peke yake)?? na kwanini wewe uliamua kuongeza mwingine asaidiane na mwenzake, sio kwamba ulimuonea huruma?? sasa iweje baba akimuonea huruma itafsiriwe kama ni uzinzi tu?? ina maana wababa hawana hurma??
 
Simple! Awe anabaki na mume wake mpaka wote waende kulala the same time. Yeye anakimbilia kwenda kulala saa 3 kwa nini, kwani ye mtoto wa shule? Watu wazima mkienda kulala saa 3 watoto walale saa ngapi?


haha dah mkuu nimecheka hadi basi...


 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom