Mume wa rafiki yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mume wa rafiki yangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Annina, Jun 3, 2010.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wapendwa nina rafiki ambae pia ni jirani yangu. Urafiki ulianzia kwa mtoto wao wa miaka 4, tukafahamiana na mama wa mtoto na tukawa marafiki na hatimae nikatambulishwa kwa baba wa mtoto ambae pia ni mume wa huyu rafiki yangu. Tulipoonana mara ya kwanza akadai nafanana sana na dada mmoja na haamini kama hatuna undugu na huyo dada - mke wake hamfahamu huyo mdada ninaefananishwa nae nami simfahamu pia.

  Toka siku hiyo kila tunapoonana amekuwa hakosi cha kusema juu yangu, mara nina macho ya uhamasishaji, lips sijui za kufanyaje.... umbo la kampeni... nk nk. Amekuwa akiyasema hayo mbele ya mke wake na rafiki zake. Sijamzoea wala sina utani nae, na nimeweka wazi kwamba sifurahii anachokifanya lakini ni kama hanielewi. Leo asubuhi tumekutana akiwa na mke wake wanaelekea kazini, mke wake akaja kunisalimia na kunihug, mume nae akaja akafanya kama mke wake hii ni mara ya kwanza kwa yeye kunihug, akashtuka kama kapigwa shoti na akasema nina ngozi laini hajapata kuona! Nilijisikia vibaya na niliona mke wake pia amekosa amani. Sijui kilichoendelea baada ya kuachana nao. Nimebaki na maswali mengi na sijui ana maana gani kwa anayoyafanya lakini naona anavuka mipaka. Nilikuwa na imani mke wake atachukua hatua na kumkanya, sijui kama amefanya hivyo.

  Wapendwa mnalionaje hili?


  Annina
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,060
  Likes Received: 24,064
  Trophy Points: 280
  Annina bana....... Hujambo lakini? Za masiku? Mbona umepotea kama miguu ya nyoka?

  Ngoja ni-reserve comments zangu kwanza. Will be back soon
   
 3. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Mwambie mbele ya mke wake kwamba hupendi tabia yake, la sivyo atadhani unafurahia huo ujinga wake... au mpotezee kabisa
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Hili mbona rahisi sana...Wewe usi-entertain hayo mambo yake kama kweli huna nia naye. Fanya jitihada zote za kumkwepa, kumuepuka, na kumwonesha kuwa you are as serious as a heart attack. Kwamba hutaki, hupendi, na hufurahishwi na anachofanya. Unaweza kuanza na lugha yako ya mwili. Lugha ya mwili inaweza kuelezea mengi sana bila hata ya kufungua mdomo wako. Asipoelewa lugha yako ya mwili basi mwambie. Mweleze kwa lugha inayoeleweka na isiyo na utata wowote.

  Hii siyo sayansi ya maroketi ya kwenda angani. Mtu yeyote mwenye maarifa ya kawaida tu ataweza kujua jinsi gani ya kukabiliana na jambo kama hilo kama KWELI ana nia ya kufanya hivyo. Ila sema akina dada wakati mwingine nao wanapenda hizi attention halafu wanajifanya hawazipendi.
   
 5. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35


  Asante NN kwa ushauri, nimejaribu kumuonyesha na kumwambia spendi anachokifanya, na kama nilivyosema awali sina mazoea nae wala utani ni kama anaang'ang'ania kunizoea. Hapo kwa bold inawezekana wadada tunapenda attention lakini kwangu mimi anachokifanya si attention bali ni udhalilshaji!


  Annina
   
 6. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Kama kaanza siku nyingi nawe huthemi kitu live then wapenda kisirisir!! na kibaya zaidi mume wako akijua ndo mambo yatakuwa magumu zaidi. Usimkwepe. Face him na umwambie awache ukuda na ikiwezekana vunja mahusiano nao wote. put a line lakini kama unatbasam halafu ndani waimia atajuaje?
   
 7. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Xpin mi nipo salama namshukuru Mungu. Majukumu tu wakati mwingine tunalazimika kupotea. Asane kwa kujali


  Annina
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Kama unaona unadhalilishwa au kunyanyaswa kijinsia (sexually harassed) basi sijui kwa nini hujaenda kutoa taarifa kwenye mamlaka husika i.e. polisi, human resources office, or whatever authority.

  Ni jambo rahisi sana hili. Mwambie yeye pamoja na mkewe kuwa hiyo tabia ikiendelea basi utampeleka huko kwenye mamlaka i/zinazohusika na mambo ya unyanywasaji wa kijinsia. Unasubiri nini - maoni ya wanaJF?

  Kuwa na msimamo/ chukua msimamo thabiti.
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  chriss! naomba unieleweshe "umbo la kampeni" lipoje ili niweze kuendelea......watu wengine wanatafutaga kudhalilishwa mbele za watu jamani,...huyo mama hakumuonja kakofi azinduke labda bado yupo ucngizini.
   
 10. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  NN umenifanya nicheke uliposema nasubiri nini - maoni ya JF? Well, kwa haraka haraka ushauri wako unafaa, lakini ukifikiri matokeo ya ya uamuzi huo waathirika wakuu watakuwa ni rafiki yangu na mtoto. Kama nilivyotangulia kusema, nilitegemea kwa kiasi kikubwa mke wake atachukua hatua - pengine amejaribu na kushindwa kama mimi sijui maana hatujazungumza juu ya hili.

  Si vibaya kupata mawazo ya wengine kupitia JF kabla sijachukua hatua, naamini kuna watu wengine yamewahi kuwatokea au yatawatokea - ndio lengo la kushare hili tatizo. Mpaka sasa tayari nina hali tofauti na asubuhi - nimeweza kucheka - naamini itanisaidia kufikiri na kuamua bila kuongozwa na jazba!

  Asante sana,

  Annina
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mpendwa,
  Unazifahamu Body langauges??? Unafahami facial expression...nk. Vitumie hivyo ataelewa tu, wala huhitaji kugombana na mtu wakati Muumba kakupa akili.

  Lakini dada, kweli toka moyoni mwako hakuna hata chembe ya kumtamani mkaka wa watu??? maana na nyie dada zetu nyie...

  One thing; Muombe Mungu akuepushie na akupe ujasiri wa kumuona mkewe na kumweleza kuwa hupendelei tabia ya mumewe kwako.

  Hapo Vipi?? Kumbuka kale ka wimbi ka JIDE: Usikatae..akikuita, labda kesho yatakukuta..dunia...
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Mkewe ni rafiki yako, ongea nae hizo kero msikie nae atasema nini. Muhimu msisitizie hupendezwi na hizo 'mbwembwe' za shemeji, hata kama atakuhakikishia "hang'ati!"
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Sorry kwa makosa ya ki-uandishi, nadhani mwalimu wangu wa typing alitumia keyboard ya kichina
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Jun 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Kuathirika kwa mke na watoto yatakuwa ni matokeo ya matendo ya huyo jamaa. Vile vile nilitegemea na wewe mwenyewe ungejiona mwathirika (kwa sababu umesema unadhalilishwa) lakini sidhani kama unaliona hilo na kama unaliona basi unalifumbia macho. You can't be serious sister girl.

  Lakini pia, nimesema kwamba umwonye na umwambie hatua utakazochukua endapo ataendelea na hiyo tabia yake na katika kumwonya huko ni pamoja na kuzingatia athari zitakazotokea. Na hata ukimpeleka kwenye mamlaka husika, sidhani kama watampa adhabu ambayo itawaathiri sana wanaomtegemea. Sana sana atapewa onyo mara ya kwanza. Akirudia tena labda atadungwa no contact order. Mpaka hapo akiwa hajapata ujumbe basi hatua madhubuti na kali zaidi ndio pengine itabidi zichukuliwe.  Sidhani kama unakerwa hivyo na anachokifanya. Kama kweli ungekuwa unakerwa basi ungekuwa angalau umeshalijadili na mkewe.


  Hapo wala sina ubishi. Hakuna ubaya wowote kupata maoni ya wengine.
   
 15. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hehehehe!
  kweli hata thread yako ni za kikampeni zaidi.........
  halafu watu wanapingana na INFIDELITY..............
  SUBUUUUUUUUUUUUUUUUTUUUUUUUUUUUUU
   
 16. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red.....Natamani kukuona ili niongeze exposure:bounce:!

  Kwa vile bado hujamfahamu vizuri huyo bwana, inawezekana ni mapema mno kufanya conclusion yoyote hasa ukizingatia mambo hayo anafanya mbvele ya mekewe (hayafanyi mafichoni). Kwa mfano suala la ku'hug' kwa baadhi ya watu sio ishu kihivyo. Na hilo la kusifia, kuna watu wana tabia ya mzaha sana hata kwa watu wageni.

  Lakini kama walivyosema wengine kama ukaribu huo unakukera ni vema ukamueleza wazi huyo bwana bila kuuma maneno na hasa body language yako ioneshe kweli hupendi/hutaki!
   
 17. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160


  Annina - aminia mwanangu - nimependa hiyo sentensi inawezekana ukawa umejaariwa. si vibaya kusifiwa ila jaribu kumkwepa jamaaa anakoendea ni kubaya sana na kumbuka Mume wa mtu ni hatari kubwa, kuwa naye ni sawa na kuchezea kwenye manuru la moto - mpe live achana naye fastaa kabla hujaanza na wewe kumpenda kitambi chake, mavazi, tai nk....
   
 18. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  akikukera sana ,mnadie mwizi bana!
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Omba mungu umkute njiani peke yake ...........upate umpe kitu in black and white.
  kisha unamalizia kwa kumwambia kuwa akiendelea utamuadhiri mbele za kadamnasi
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Anina ......
  I miss u so........

  Hujambo?

  Kuhusu huyo jamaa,unahitaji a man around,ili amfumue mangumi siku moja ndo aelewe...
  Ngoja nije huko.........
   
Loading...