Mume wa mwimbaji Injili adaiwa kumbaka shemejiye

Dah kama ni kacheza chachandu sio kalienda kumharibia ndoa mwenzie haka? Akiwa hayupo kalifata nini? Mungu amsaidie Flora ni majaribu!
Jina limehifadhiwa. Well, lets do Sherlock Holmes here: mume na mke ni waimba injili+wanakaa tabata kimanga+wana uhusiano na mchungaji gwajima=Huyu ni F.M,yule ambaye mdogo wake alicheza video ya chachandu na M .Ngasa(video ilipata wekwa humu jf). Sasa sijui mdogo wake huyu ni yule au huyu ni mwingine!
 
Ni kweli mrembo ila shetani ni nuksi sometimes.

Hapa shetani anasingiziwa bure tu, jamaa ni bazazi tu. Kama anaweza kutamani na kuchepuka ndani ya nyumba anayoishi, tena kwa mdogo wa mke wake, je huko mitaani kwa watu baki inakuwaje. Kifungo cha maisha ni juu yake...

Though I can't rule out conspiracy kumfunga mume ili waoe mke wake, si mrembo!
 
Habari ikishaingia humu jamvini huchambuliwa kwa kina...........dare to talk openly
 
Sio kwamba natetea wabakaji,lakini Mwananchi hii habari imeandikwa kwa ushabiki zaidi badala ya taaluma nzima na maadili ya uandishi.Kwanza kitendo cha kuweka majibu ya kipimo cha VVU ya mtu hadharani ni makosa(yawe positive au negative).Na hapa tuwaulize Mwananchi ushahidi wa kipimo hicho mmeupata wapi?Majibu anapewa yule aliyepimwa na ni oral,yanapotolewa kwa maandishi kwa sababu maalumu yanatakiwa kuwa siri na wala sio kutangaza gazetini!Ingetosha tu kuandika kuwa baadaye alifanya kipimo cha VVU ili kujua afya yake,basi inatosha,hayo mengine ni udaku na Mwananchi sio gazeti la Udaku nyie!

Jingine mnatuambia binti alibakwa mara 3,mbili kwenye gari!Mwanzoni alikaa kimya lakini baada ya kubakwa mara ya #PILI ndio akaamua kuwaeleza ndugu zake na ndio wakaenda kuripoti polisi,je huo mbako wa mara ya #TATU ulitokea baada ya kutoa taarifa kwa ndugu zake?

Mkuu ndio wewe mume wa FM, au yule mdogo wake aliyeenda kupoza ishu kwa mhariri!?

Uchafu kama huu inatakiwa uandikwe kutoka angle zote ili mabazazi wakome na kubaki njia kuu.
 
inatofautiana vp? Hapo wamekurahisishia.in short mbakaji na mkewe wote ni waimbaji. F.M. na mmewe ni waimbaji na wanaishi Tabata Kimanga.

Acha uongo wako wewe,ama hujui kusoma??? Wapi wameandika kwenye habari hiyo kuwa mke na mume wote ni waimbaji?Acha upotoshaji ndugu yangu
 
Walipata kuimba
"Maisha ya ndoa, yafananishwa na safari......utapita mabonde.......nakupenda mpenzi wangu.......toka unioe sijawahi kujuta......"

Eeh Mungu tuepushie mbali na zinaa
 
myself nimewaza hivyo.. ila mbona mkewe mrembo sana?
. Hili Pepo huwa haliangalii urembo; issue ingekuwa urembo hata wasio na akili timamu wasingezaa! Yaani nahisi damu kunichemka kwa hasira:embarassed2:
 
Makala: Sifael Paul na Mitandao
FLORA Mbasha ni mwimba Injili Bongo mwenye ‘profaili' kubwa ndani na nje ya Tanzania. Kama ulikuwa hujui, ni mmoja wa mastaa wengi wakubwa wa ‘gospo' watakaoshusha upako kwenye Tamasha la Matumaini litakalofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar, Julai 7, mwaka huu.
Flora alizaliwa jijini Mwanza mwaka 1983 katika familia ya Dini ya Kikristo. Ni mtoto wa pili kwenye familia ya Henry Mayallah na Caroline Moses Kulola.
Alimpoteza baba yake mwaka 1998. Kwa wakati huo walikuwa wakiishi jijini Arusha, akamwacha Flora na nduguze Benjamin na Dorcus.
Baada ya baba kufariki dunia walirejea Mwanza ambapo walilelewa na babu yao ambaye wengi wanamjua, Askofu Moses Kulola wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God la Mwanza.
"Nimekulia mikononi mwa kanisa tangu nikiwa mdogo. Nawashukuru babu na bibi yangu kwa kunilea tangu nilipompoteza baba yangu. Walinifundisha kwa kipindi chote hadi nilipoolewa," anasema Mbasha katika mahojiano na runinga moja London, Uingereza.
Baadaye mama yao aliolewa na mwanaume mwingine na kujaliwa mabinti wawili, Suzy na Esther. Flora alihitimu masomo ya sekondari katika Shule ya Taqwa, Mwanza mwaka 2000.
NDOA
Agosti 22, 2002, Flora alifunga ndoa na mwimba Injili, Emmanuel Mbasha wakiwa Mwanza na mtoto wao wa kwanza anaitwa Elizabeth. Agosti 22, mwaka huu watatimiza miaka 11 ya ndoa bila ‘kikohozi' yaani bila migogoro au kuvunjika kama zilivyo baadhi ya ndoa za mastaa wengine Bongo. Wanapendana mno, mahali alipo Flora lazima utamuona Mbasha.
Flora anakiri kuwa mafanikio aliyopata yana mchango mkubwa wa ushirikiano anaopata kutoka kwa mumewe Mbasha.
"Mume wangu amekuwa msaada mkubwa wa mafanikio yangu," anasema Flora ambaye kwa sasa anaishi na familia yake katika nyumba waliyojenga Tabata, Dar.
Anaendelea: "Ananisapoti (Mbasha) kwa kunipa ushauri sahihi na kuniongoza kuwa hivi nilivyo leo. Tumeandika nyimbo pamoja na kupafomu katika albam zangu zote nilizonazo.
MUZIKI WA GOSPO
Flora alianza muziki wa ‘gospo' tangu akiwa mdogo akiimba kwaya kanisani. Anasema pamoja na ubunifu binafsi lakini pia alikuwa akiwaiga waimbaji wengine kwenye kwaya kanisani na kwenye mikutano ya Injili. Baadaye alimtamani kuwa kama mwimba Injili wa Afrika Kusini ‘Sauzi', Rebecca Malope.
"Nilianza kuimba nikiwa mdogo sana. Nilikuwa nikiimba kwenye Kwaya ya Bugando Divine Singers ya Mwanza," anasema na kuongeza:
"Baadaye, kwa msaada mkubwa wa mume wangu nilifanikiwa kurekodi albamu yangu ya kwanza ya Jipe Moyo Utashinda katika Studio ya Backyard chini ya Prodyuza Hingi."

NYIMBO ZOTE KALI
Katika albam hiyo utakutana na nyimbo zenye upako kama Maisha Ya Ndoa, Hakuna Tatizo Kuu, Ukimwi, Yu Karibu, Aliteseka, Tunaye Bwana, Majaribu, Ahsante Yesu na Kila Jambo.
Katika albam yake ya pili iliyokwenda kwa jina la Unifiche, utapata utamu wa nyimbo zake kama Tanzania, Nifiche, Faida Gani, Twende Kwa Yesu, Ninalia, Kwa Kupigwa Kwake, Kristo Amezaliwa na Tupendane.
"Namshukuru Mungu kwa albam ya pili, ilinipa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Gospel mwaka 2004. Niliandika wimbo kwa ajili ya nchi yangu, nikaupa jina la Tanzania. Ulinifanya nijulikane zaidi ndani na nje ya Bongo," anasema.
Mwaka 2008, Flora aliachia albam yake ya tatu iliyoitwa Furaha Yako ikiwa na nyimbo kali 12 kama Furaha Yako, Rudi Nyuma, Adui Yako, Tutamwona, Nibariki, Tufurahie, Mteule Usiogope, Natembea na Yesu, Anaweza, Jerusalemu, Mwanamke na Usife Moyo.
MALENGO
Malengo ya Flora ni kufanya watu wazaliwe upya katika Kristo ndiyo maana nyimbo zake zimejaa mafundisho ya Mungu.
Flora amezunguka mikoa mingi Bongo na nje ya nchi kama Marekani, Uingereza, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kwingineko. Kote alikopita alipokelewa kwa kishindo na akatoa mafundisho ya Mungu kwa njia ya nyimbo.
"Nimefanikiwa kushika mioyo ya watu wengi wanaopenda muziki wa Injili hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kifedha kwa ajili ya kulipia kuingia kwenye matamasha," anasema Flora na kuongeza:
"Ndoto yangu ni kumtumikia Mungu katika maisha yangu hadi atakaponiita. Watu lazima wabadilike, waachane na madawa ya kulevya, pombe na umalaya kisha wamrudie Mungu.
"Moyo wangu unauma sana ninapowaona vijana wakitenda dhambi."

UTUKUFU UTASHUKA!
Flora anayependa kuchati na marafiki ataangusha shangwe za upako kupitia nyimbo zake nyingi nilizokudonolea kidogo hapo juu na nyingine nyingi mpya katika tamasha hilo la Matumani akiwa na Upendo Nkone, Martha Mwaipaja, Edson Masabwite, Ambwene Mwasongwe, Glorious Worship Team, Emmanuel Mgaya ‘Masanja', Enock Jackson, The Voice na Jesca.
Kutoka Kenya atachuana na Anastazia Mukabwa, Solomon Mukubwa, Sara K na 24 Elders.
 
inatofautiana vp? Hapo wamekurahisishia.in short mbakaji na mkewe wote ni waimbaji. F.M. na mmewe ni waimbaji na wanaishi Tabata Kimanga.

FM unamaanisha Flora M? Si mweke hadharani sasa mnafichaficha nini?
 
Sio kwamba natetea wabakaji,lakini Mwananchi hii habari imeandikwa kwa ushabiki zaidi badala ya taaluma nzima na maadili ya uandishi.Kwanza kitendo cha kuweka majibu ya kipimo cha VVU ya mtu hadharani ni makosa(yawe positive au negative).Na hapa tuwaulize Mwananchi ushahidi wa kipimo hicho mmeupata wapi?Majibu anapewa yule aliyepimwa na ni oral,yanapotolewa kwa maandishi kwa sababu maalumu yanatakiwa kuwa siri na wala sio kutangaza gazetini!Ingetosha tu kuandika kuwa baadaye alifanya kipimo cha VVU ili kujua afya yake,basi inatosha,hayo mengine ni udaku na Mwananchi sio gazeti la Udaku nyie!

Jingine mnatuambia binti alibakwa mara 3,mbili kwenye gari!Mwanzoni alikaa kimya lakini baada ya kubakwa mara ya #PILI ndio akaamua kuwaeleza ndugu zake na ndio wakaenda kuripoti polisi,je huo mbako wa mara ya #TATU ulitokea baada ya kutoa taarifa kwa ndugu zake?
Mimi pia naona wameenda mbali kidogo japo sijui maadili au taaluma ya uandishi inasemaje kuhusu hilo. Lakini all in all wao walitaka kufikisha ujumbe uliokamika kwa wasomaji na kweli ujumbe umefika na hakuna maswali zaidi!
 
Mkuu ndio wewe mume wa FM, au yule mdogo wake aliyeenda kupoza ishu kwa mhariri!?

Uchafu kama huu inatakiwa uandikwe kutoka angle zote ili mabazazi wakome na kubaki njia kuu.

Hahahaaaaaaa,sio mimi ila natetea hasa utu wa huyo aliyebakwa,mambo ya matokeo ya vipimo vya ukimwi hayakutakiwa kuwekwa hadharani
 
Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, (jina tunalihifadhi kwa sasa), anatuhumiwa kumbaka shemeji yake mdogo (17).

Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa juzi saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu na kumsababishia maumivu makali.

Binti huyo alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili ambao walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa mtuhumiwa wa kuzima kesi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye alimbaka mara ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alipombaka mara mbili ndani ya gari.

Alisema mara ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba angemdhuru kama angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa sebuleni nyumbani kwako Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa ndugu zake baada ya kubakwa mara ya pili.

Polisi katika kituo hicho walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo lakini walishindwa kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa maelezo kwamba hawakuwa na askari wa kutosha na kuahidi kwamba angekamatwa jana. Hata hivyo, hadi jana mtuhumiwa huyo alikuwa hajakamatwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kutwa nzima ya jana hakupatikana kuzungumzia tukio hilo na kila simu yake ilipopigwa (kati ya saa nane mchana na saa mbili usiku), ilipokewa na msaidizi wake akisema bosi wake ana kazi nyingine.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hakuwa amepokea taarifa yoyote ya aina hiyo.

Mwimbaji anena

Alipoulizwa jana, mwimbaji huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kwa undani tuhuma zinazomkabili mumewe na kwamba alikuwa anajisikia vibaya kutokana na tukio hilo kuhusisha watu wake wa karibu.

“Of course (bila shaka), hili sio tukio zuri. Kwa sasa sina uwezo wa kuzungumza kwa sababu hili suala lipo Polisi. I am confused (nimechanganyikiwa), ukizingatia kwamba linasemekana kutokea wakati sikuwepo nyumbani, naomba tuzungumze baada ya akili kutulia,” alisema.

Kadhalika, jana saa 6:20 mchana, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mtuhumiwa ambaye baada ya kupewa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili alisema: “Samahani sana ujue sikusikii kabisa,” kisha alikata simu.
 
Back
Top Bottom