Mume wa mwimbaji Injili adaiwa kumbaka shemejiye

Lussadam

JF-Expert Member
Oct 13, 2007
1,201
2,000
Dar es Salaam. Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, (jina tunalihifadhi kwa sasa), anatuhumiwa kumbaka shemeji yake mdogo (17).

Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa juzi saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule), zikimtuhumu mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu na kumsababishia maumivu makali.

Binti huyo alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili ambao walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa mtuhumiwa wa kuzima kesi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye alimbaka mara ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alipombaka mara mbili ndani ya gari.

Alisema mara ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba angemdhuru kama angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa sebuleni nyumbani kwako Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa ndugu zake baada ya kubakwa mara ya pili.

Polisi katika kituo hicho walithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo lakini walishindwa kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa maelezo kwamba hawakuwa na askari wa kutosha na kuahidi kwamba angekamatwa jana. Hata hivyo, hadi jana mtuhumiwa huyo alikuwa hajakamatwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi kutwa nzima ya jana hakupatikana kuzungumzia tukio hilo na kila simu yake ilipopigwa (kati ya saa nane mchana na saa mbili usiku), ilipokewa na msaidizi wake akisema bosi wake ana kazi nyingine.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema hakuwa amepokea taarifa yoyote ya aina hiyo.

Mwimbaji anena

Alipoulizwa jana, mwimbaji huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kwa undani tuhuma zinazomkabili mumewe na kwamba alikuwa anajisikia vibaya kutokana na tukio hilo kuhusisha watu wake wa karibu.

"Of course (bila shaka), hili sio tukio zuri. Kwa sasa sina uwezo wa kuzungumza kwa sababu hili suala lipo Polisi. I am confused (nimechanganyikiwa), ukizingatia kwamba linasemekana kutokea wakati sikuwepo nyumbani, naomba tuzungumze baada ya akili kutulia," alisema.

Kadhalika, jana saa 6:20 mchana, gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mtuhumiwa ambaye baada ya kupewa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili alisema: "Samahani sana ujue sikusikii kabisa," kisha alikata simu.

Gazeti hili lilimpigia tena simu lakini ilikatwa na baada ya hapo kila alipopigiwa haikupokewa. Baadaye saa 6:35 mchana, mtu aliyejitambulisha kuwa ni mdogo wa mtuhumiwa alipiga simu chumba cha habari akitaka kuonana na mhariri wa gazeti hili, kwa maelezo kwamba alipewa namba husika na kaka yake.

"Samahani, mimi (anataja ina) niko hapa nje Ofisi za Mwananchi, nilifika hapa kutaka kuonana na mhariri maana nasikia mwandishi wenu alikuwepo polisi tangu jana kwenye tatizo lililompata kaka yangu, sasa wakati nasubiri kuonana na mhariri kaka amenipigia simu akisema namba hii imempigia, kwa hiyo naomba tuonane ili tuzungumze tuone jinsi ya kumsaidia," alisema.

Baada ya kuonana na mwandishi wa habari wa gazeti hili, alisema suala hilo lilikuwa likijadiliwa katika ngazi ya familia, hivyo wasingependa liandikwe kwenye vyombo vya habari.

Vipimo vya hospitali

Juzi, baada ya tukio hilo kuripotiwa, mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Amana ambako alifunguliwa faili la matibabu na kupewa namba ya usajili 667. Aliingia chumba cha matibabu namba 21 kumuona daktari kwa ajili ya vipimo zaidi.

Matokeo ya vipimo yalionyesha kuwa binti huyo alikuwa amefanya ngono kwa nguvu. Katika fomu hiyo ya uchunguzi, daktari aliandika ‘High vagina swab'.

Baada ya vipimo, familia ilirudi katika Kituo cha Polisi kupeleka matokeo ya vipimo vya daktari, hivyo kufungua faili la kesi lililopewa namba RB TBT/RB/319/2014 na namba TBT/IR/1865/2014. Jana binti huyo alikwenda tena Amana ambako alifanyiwa vipimo vilivyobaki vya VVU na mimba. Vipimo vya awali vya VVU vilionyesha kuwa hakuwa ameathirika na hakupata ujauzito.

Mtoto alipo

Habari ambazo zililifikia gazeti hili jana jioni, zilisema mtoto aliyebakwa alichukuliwa na familia ya Mchungaji Josephat Gwajima.

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Mchungaji Gwajima bila mafanikio, lakini lilimpata mkewe, Grace ambaye hakuwa tayari kuthibitisha kuwapo au kutokuwapo kwa mtoto huyo nyumbani kwake.

"Naomba nisiwe msemaji katika jambo hilo, yupo msemaji mwenyewe ambaye naamini mnamfahamu naye ni Mchungaji Gwajima, kwa hiyo mtafuteni, yeye atasema kama mtoto yupo hapa au hayupo na kama yupo sababu zake ni zipi," alisema Grace.

Alipoombwa atoe mawasiliano ya simu ya mchungaji huyo, Grace alisema: "Kwa kweli kama unaweza, kesho nenda pale Kanisani Kawe utapewa utaratibu wa kuonana naye.


Source: Mwananchi

Mumewe Flora Mbasha ajitokeza, afichua siri...


Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17. Faili la tuhuma dhidi ya Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.

Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike.

"Tuhuma dhidi yangu ni za kutengeneza," alisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake ambao alisema umedumu kwa siku kadhaa.

"Mimi sijabaka na sijawahi kubaka; sijatenda dhambi yoyote; sijafanya kitu chochote na kibaya haya mambo yote ni ya kusingiziwa tu. Mungu wangu ni shahidi. Na kwa kuwa sijafanya hiyo dhambi kama wanavyodai, basi Mungu wangu atanitetea," alisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.

"Si wamesema wananitafuta, nitakwenda mwenyewe polisi. Nitawasikiliza na nitatoa maelezo yangu. Kama wakinipeleka mahakamani basi ukweli utajulikana... ipo siku kila kitu kitakuwa wazi."

Kabla ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari kung'amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).

Kadhalika binti huyo alifanyiwa vipimo kuona kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi (VVU), pia kupata ujauzito, lakini matokeo ya awali yalionyesha kuwa yupo salama.

Akiwa nje ya kituo cha polisi Jumatatu usiku, binti huyo aliliambia gazeti hili kwamba mara ya kwanza alibakwa mchana Mei 23 na kwamba mtuhumiwa alirudia kitendo hicho Jumapili Mei 25 usiku ndani ya gari katika eneo la Tabata, ambako anadai alifanyiwa kitendo hicho mara mbili.

Hata hivyo, Mbasha alihoji: "Hivi kweli hata kama mimi ni mbakaji, kweli nimbake mtoto wa kumlea mwenyewe mara tatu, yaani Ijumaa halafu nirudie tena Jumapili? Hata kama ni kusingiziwa basi tuhuma hizi zimezidi."

"Huyu binti nimekaa naye miaka mingi na sijawahi kumfanyia hivyo. Hapo nyumbani kwangu wamekaa mabinti wengi, wakiwamo shemeji zangu wadogo zake na Flora na sikuwahi hata kuwagusa, leo hii kwa nini wananifanyia hivi?"

MGOGORO WA FAMILIA

Mbasha alidai kwamba chanzo cha kusingiziwa kwake ni mgogoro baina yake na mkewe Flora, ambao umesababisha mgawanyiko mkubwa ambao umefanya achukiwe na familia nzima ya mkewe.

"Yako mambo mengi tu ambayo yanahusu familia, kwa hiyo ilifika mahali mimi na Flora tukawa hatuishi kwa amani na hata hili jambo limetokea wakati tukiwa na mgogoro huo. Hivyo Flora na ndugu zake waliamua kumlisha binti huyo maneno ili mimi nifungwe," alisema Mbasha.

Hata hivyo, Flora hakutaka kuingia kwa undani katika suala hilo, akisisitiza kuwa Mbasha bado ni mumewe na kwamba yaliyotokea awali alishamsamehe, lakini akamtaka ajitokeze kutoa maelezo polisi.

"Mimi nilishamwambia kwamba hata kama alifanya au hakufanya, nilishamsamehe kutoka ndani ya moyo wangu maana yeye ni mume wangu wa ndoa na Mungu wangu ni shahidi, lakini kuna suala la kisheria polisi ambalo mimi siwezi kuliingilia," alisema Flora ambaye alitamba na wimbo wa injili wa "Tanzania" ambao ulimfanya aalikwe katika shughuli mbalimba za kitaifa.

"Tatizo linakuwa kubwa kwa sababu yeye mwenyewe haonekani na taarifa ni kwamba amekimbia," alidai Flora. "Sasa kama kweli hajafanya kitendo hicho, kwa nini anajificha? Ajitokeze... aende polisi na huko ndiko akatoe maelezo yake. Kuzungumza na vyombo vya habari haisaidii kabisa."

Mwimbaji huyo, ambaye ni mjukuuu wa muhibiri maarufu wa Injili, Askofu Moses Kulola alisema yeye hana uwezo wa kuingilia kesi hiyo kwani hakuhusika kwa namna yoyote ile kupeleka suala hilo polisi kwa sababu hakuwapo wakati likitokea na kwamba linasimamiwa na familia.

"Inawezekana anatamani nikafute kesi polisi, mimi sina uwezo huo kwa sababu ni suala la kisheria na tuhuma zenyewe ni za kijinai. Pili familia yenye mtoto ndiyo inafuatilia kesi hiyo, lakini hilo halifuti msamaha wangu kwake," alisisitiza.

Kauli ya Flora kwamba ameshamsamehe mumewe inafanana na ya Mbasha ambaye pia alisema kwamba kama kuna jambo ambalo mkewe alimkosea, hana tatizo na kwamba alishamsamehe.

"Flora ni mke wangu, mke wa ujana wangu, ninampenda asilimia 100 na yeye analifahamu hilo, lakini sijui ni kitu gani kimemkuta? Sijui ni nini kimeingilia ndoa yetu?" alisema Mbasha.

Alisema ameshampigia simu mkewe mara nne akitaka waonane ili wazungumze, lakini hakuonyesha utayari, kauli ambayo Flora aliikanusha akisema: "Hajanitafuta maana tangu Jumatatu hapatikani kwenye simu."


Mwenendo wa upelelezi


Wakati hayo yakiendelea, maendeleon ya kesi hiyo yanasuasua baada ya faili kutokupelekwa Kituo cha Polisi Buguruni kutoka Tabata kwa ajili ya hatua zaidi.

Baadhi ya wanafamilia wa mtoto anayedaiwa kubakwa walisema jalada hilo lingefikishwa Buguruni Jumatano jioni, lakini kutokana na ofisa anayeshughulikia kesi hiyo kuwa na udhuru, ilishindikana.

Mjomba wa Flora ambaye amepewa jukumu la kusimamia kesi hiyo, alisema wamekuwa wakifuatilia Kituo cha Polisi cha Tabata tangu tukio hilo liliporipotiwa, lakini wakaelezwa kuwa kesi hiyo itahamishiwa Buguruni.

"Tuliambiwa lile faili lazima lihamie kituo cha Buguruni. Nilifika hapa nikaonana na kamanda wa polisi wa wilaya ambaye ametupokea vizuri na kuonyesha moyo wa kutusaidia," alisema.

Kamanda wa polisi wa Ilala, Marietha Minangi alisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kesi hiyo na kwamba hafahamu taarifa kuwa faili hilo linacheleweshwa kuhamishiwa Buguruni. "Tunaendelea kuchunguza, ila siyajui hayo masuala ya faili yanayotoka kinywani mwako. Lakini nimepata taarifa kuwa bado wanachunguza," alisema Minangi.

Mwanzoni mwa wiki jana, Kamanda Minangi alisema kuwa maofisa wake walikuwa wanaendelea kumsaka mtuhumiwa na kwamba walienda mpaka nyumbani kwake, lakini hawakumkuta.


---------------


Wakati sakata la Flora likiendelea, bwana wake Mbasha amefunguka kwenye redio na kusema anasikitika sana mkewe kutaka kumfunga ili aendelee na uhuni wake na jamaa mmoja ambae anasema ni kigogo serikalini wakati wengi wakiongea mara Gwajima mara nani.

Mbasha amefunguka na kusema anajua mchezo mzima na aliepanga hilo na akasema hata akifungwa miaka 30 akitoka ni lazima afe na huyo kigogo liwalo.

Mbasha akaenda zaidi na kusema kuwa tokea zamani mkewe amekuwa akitongozwa na wakubwa na kumwambia mtu fudenge anataka tunda lake lakini tangu alipoanza kutukanana nae kuhusu huyo kigogo ameamua soln ni kumnyima tunda.

Sasa ameamua amfunge ili aendeelee na uhuni wake. Naamini Gwajjima atapumzika kwa statement hiyo na wengine waliohusishwa na Flora.

Nilisema na nitarudia tena sakata zima la Flora na mumewe ni wawili tu ndio wanajua chanzo na upumbavu unaoendelea juu yakee.

Akafunguka mtoto huyo wanaesema nimembaka nimemtoa mwenye kijijini na hata wanavyosema ana miaka 17 si kweli ..waende shule aliyosoma ama waangalie kadi yake ya kuzaliwa ana miaka 19.


Ujue hata mchezo wanaocheza hawana uhakika wanachoongea mwisho wa siku nawaambia watanzaniaMungu yupo na ukweli utafika utajulikana na Mungu atajiidhihirisha kwa hili, Ahsanten.

Nanukuu mbasha alivyoaga so sad kwa waliosikia hili.

Alichosema Mtitu
"Ukiiangalia vizuli hii picha utagundua kitu katika macho ya Frola Mbasha kuna kitu nakiona kinejificha lakini sasa hivi kimeshajitokeza tayali.....hicho kitu ndicho kilichompeleka jera mbasha na asipokuwa makini anaweza asiwe uraiani tena kama ulivyowatokea familia ya nguza .namaanisha mzee nguza na papii kocha wako wapi?

Kiukweli Frola una roho mbaya ya mwisho kabisa ilichanganyika na ukatili wa mwisho kabisa kiasi kwamba nashindwa kuelewa umeokoka nn ww ?

Eti umemrudia YESU ?YESU yupi huyu nnaemwabudu mm au una YESU wako ww na HUYO GWAJIMA wako? Leo umemsahau Mbasha ww ?

Wakati alikuokata umechakaa wakati mbasha dereva teksi leo wataka kumfunga ili iwe nn sasa mbasha akifungwa utapata faida gani ww?

Huyo mtoto akija kukuuliza baba yuko wapi utamwambiaje?

Fine unaweza kujikaza ukamwambia yuko jela je akikuuliza nani alimshitaki utajibu nn ?

Pia waweza kujikaza ukawataja hao wasichana mliowapandikiza je akiuliza ww ulifanya jitihada gani baba asifungwe utasemaje?

Hapo auna jibu Acha roho mbaya NENDA KAMTOE MARA MOJA NA MWENDE NYUMBANI MKAONGEE KAMA FAMILIA TWAJUA UWEZO HUO UNAO ILI NA YEYE ATAFUTE HAMSINI ZAKE KAMA WW ULIVYOAMUA KUJISALIMISHA KWA GWAJIMA. USIJE UKASHANGAA WATU WAKASUSIA KAZI ZAKO ZOTE. GDAY."


Flora Mbasha: Mume wangu ametishia kuniua

SIKU chache baada ya tuhuma za ubakaji na mzozo wa familia ya mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha na mumewe, Emanuel Mbasha, mambo mengine yameibuka.Mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha

Yaliyoibuka safari hii ni taarifa kwamba, juzikati, Flora alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Tabata Kimanga jijiini Dar dakika chache baada ya yeye kuingia na gari akitokea mafichoni anakoishi kwa sasa.Kwa mujibu wa chanzo, siku ya tukio ilikuwa saa 9.15 alasiri ambapo Flora aliingia nyumbani kwake na kufunguliwa geti kubwa kisha kuingiza gari ndani na geti kufungwa tena.

"Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao hawatafungua," kilisema chanzo.Mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha akiwa na mumewe, Emanuel Mbasha,

Chanzo kikazidi kudai kwamba, ilibidi Flora apige simu polisi ili wafike kumuokoa yeye na familia yake.

"Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa na bunduki na kukuta wale watu wamekimbia maana walimsikia Flora akiongea na polisi kuomba msaada.


"Lakini polisi wenyewe ilibidi watumie nguvu kubwa kugonga geti na kujitambulisha ndipo akatokea Flora na kuchungulia nje kupitia dirisha dogo. Alipowaona polisi akafungua mlango," kilisema chanzo hicho.

Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.


Alizungumza na gazeti hili baada ya tukio, Flora alisema: "Unajua kwa sasa nina hofu sana na nilihisi wale watu walikuwa wakinifuatilia kwa karibu kila sehemu, sasa naogopa kuendelea kuishi hapa, wanaweza kurudi na sijui lengo lao."


Hata hivyo, baada ya askari hao kuondoka katika eneo hilo, Flora naye aliingia kwenye gari lake akiwa na mdogo wake na kuondoka.

Mume wa Flora, Mbasha naye yupo mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka binti wa miaka 17 ndani ya nyumba yao huku utata ukitawala kuhusu ukweli wa tukio hilo ambalo limeigawa jamii.
Pitia hii video umsikilize anayoyasema:
Ujumbe wa William Mtitu kwa Frolah Mbasha huu hapa

husomeni wenyewe..

anaendelea..........Mdogo wake Flora Mbasha aliyebakwa ndiyo yule alocheza X na Mrisho

Mwaka wa 2012 kuna Video ilivuja ngasa akila maraha na denti kama Mnakumbuka. Yule denti alikua ni Mdogo wake Flora Mbasha na ndo huyo juzi kati habari zilivuja kwamba katembea na Mume wa Flora.

Nakumbuka ile video ya Ngasa simba walikua wakiificha sana lakini ikashindakana.

Nashangaa leo dogo anakuja kudai kwamba ana miaka 17 na Mbasha ndiye kamtoa bikra yake kwani kambaka mara mbili.

Video ninayo kimaadili siwezi kuiweka hapa. Labda ntawawekeeni picha tu. picha ya mnato.

My take;
Hii ya kubaka ni Mpango wa kummaliza Mbasha. Mbasha inabidi asaidiwe kwa hili kwani huyo mdogo wake mbasha anaonekana kakubuhu kutokana na mambo yake ndani ya hii video.

kama vipi ntawawekeeni kule kwa wakubwa. Mia
 
Last edited by a moderator:

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,681
2,000
heading inatofautiana na kilichomo kwenye maudhui, aidha ni kwa bahati mbaya au kwa dhumuni maalum
 

Lussadam

JF-Expert Member
Oct 13, 2007
1,201
2,000
heading inatofautiana na kilichomo kwenye maudhui, aidha ni kwa bahati mbaya au kwa dhumuni maalum

inatofautiana vp? Hapo wamekurahisishia.in short mbakaji na mkewe wote ni waimbaji. F.M. na mmewe ni waimbaji na wanaishi Tabata Kimanga.
 

mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Kichwa cha habari na habari yenyewe haviwiani full utapeli wa kiuandiahi.
 

Meljons

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
2,842
2,000
inatofautiana vp? Hapo wamekurahisishia.in short mbakaji na mkewe wote ni waimbaji. F.M. na mmewe ni waimbaji na wanaishi Tabata Kimanga.

myself nimewaza hivyo.. ila mbona mkewe mrembo sana?
 

Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,950
2,000
Acha kudhalilisha waibaji wewe!!!! Kichwa cha habari tofauti na stori yako!! Acha tabia hii!
 

Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,323
2,000
Flora Mbasha...

Jamii forum Namba nyingine kabisa, we acha tu!

Lakini hivi vibinti vina tabia ya kutega watu. Labda ktk hili kila mmoja alikuwa na malengo yake, mmoja malengo yametimia mwingine kawa - "disappointed" na hivyo kuipeleka "issue" kwa wanaa.
 

sungura1980

JF-Expert Member
May 20, 2013
1,911
1,195
Sio kwamba natetea wabakaji,lakini Mwananchi hii habari imeandikwa kwa ushabiki zaidi badala ya taaluma nzima na maadili ya uandishi.Kwanza kitendo cha kuweka majibu ya kipimo cha VVU ya mtu hadharani ni makosa(yawe positive au negative).Na hapa tuwaulize Mwananchi ushahidi wa kipimo hicho mmeupata wapi?Majibu anapewa yule aliyepimwa na ni oral,yanapotolewa kwa maandishi kwa sababu maalumu yanatakiwa kuwa siri na wala sio kutangaza gazetini!Ingetosha tu kuandika kuwa baadaye alifanya kipimo cha VVU ili kujua afya yake,basi inatosha,hayo mengine ni udaku na Mwananchi sio gazeti la Udaku nyie!

Jingine mnatuambia binti alibakwa mara 3,mbili kwenye gari!Mwanzoni alikaa kimya lakini baada ya kubakwa mara ya #PILI ndio akaamua kuwaeleza ndugu zake na ndio wakaenda kuripoti polisi,je huo mbako wa mara ya #TATU ulitokea baada ya kutoa taarifa kwa ndugu zake?
 

Swat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,202
2,000
Jina limehifadhiwa. Well, lets do Sherlock Holmes here: mume na mke ni waimba injili+wanakaa tabata kimanga+wana uhusiano na mchungaji gwajima=Huyu ni F.M,yule ambaye mdogo wake alicheza video ya chachandu na M .Ngasa(video ilipata wekwa humu jf). Sasa sijui mdogo wake huyu ni yule au huyu ni mwingine!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom