Mume Na Mke Ndani Ya Gari!

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,408
Kuna hii imenitokea sana, nikaulizia kwa baadhi ya watu nao pia wakaniambia kuwa hukumbana nalo ni kawaida, nikaona bora nililete hapa JF kwa magwiji.Mara nyingi ukiwa na mkeo ndani ya gari mmetoka, mnakuwa mmenuniana, hasa hasa mke ndiye anaanzisha mnuno, ukimuuliza kitu anajibu kwa mkato.Lakini kama unatoka na kimada au nyumba ndogo ndani ya gari kunakuwa na furaha ya ajabu,mabusu motomoto, mahanjumati ya kila aina...udi wa mawardi....mengine ni siri!
Wadau jamani hii imekaaje?
 
mie simo maana hayo mambo ni wawili tu wanayajua...lkn pia midume sometimes huanzisha mambo hasa ikinyimwa MKATE WA UZIMA
 
kweli ni kali, lakini ni kweli! Mimi nadhani sababu kuu ya kuwa na minuno ndani ya gari kati ya mume au mke ni kwasababu ya kilichotokea kabla ya kuingia ndani ya gari. Unajua binaadamu kila mtu ana mawazo yake, na mara nyingi ya mke na mume huwa hayatakiwi kupishana sana, na hii si kitu rahisi, maana kila mtu amezaliwa na kulelewa kivyake vyake kutokea kwao, ikija unakutana na mwenza wako ili kujaribu kuweka sawa au kama si sawa basi angalau yakaribiane japo kiasi hapo sasa ndio inapoanza kuwa kimbembe! Kwahiyo ukiona minuno ndani ya gari hii ni sababu kubwa mojawapo, najua zipo nyingi sana!
 
Tatizo liko hapa kwenye ku keep time!Wakati wa kuondoka kina mama wengi huchelewa kwa sababu mbali mbali,mara kujipodoa mara uji wa mtoto,maagizo kwa dada hatimaye amesahau simu yake chumbani,anataka kurudi ndani ,Huyu baba tangu alipoingia kwenye gari yeye shughuli zake ni kidogo mipango mingi iko kule aendako,maamuzi mazito ya kikazi kwa siku hiyo,Kwa hiyo akili yake yote inamtuma kufikiria kuwahi to keep time!Linalofuatia hapa ni honi mtindo mmoja na mama akiingia kwenye gari hana haraka huku akitoa maneno makali kwamba yale aliyokuwa akifanya ni muhimu pia.Wakiingia barabarani hakuna wa kuongea na mwenzake labda awepo abiria mwingine lakini wawili hawa majibu yao yana usongo wa yale ya kule walikotoka.
 
Kuna hii imenitokea sana, nikaulizia kwa baadhi ya watu nao pia wakaniambia kuwa hukumbana nalo ni kawaida, nikaona bora nililete hapa JF kwa magwiji.Mara nyingi ukiwa na mkeo ndani ya gari mmetoka, mnakuwa mmenuniana, hasa hasa mke ndiye anaanzisha mnuno, ukimuuliza kitu anajibu kwa mkato.Lakini kama unatoka na kimada au nyumba ndogo ndani ya gari kunakuwa na furaha ya ajabu,mabusu motomoto, mahanjumati ya kila aina...udi wa mawardi....mengine ni siri!
Wadau jamani hii imekaaje?

Hii ilishawekwa hapa siku nyingi na Mkuu Mbu...lakini wengine huwa na vicheko tu vya nguvu pamoja na kuwa wameshakata miaka mingi pamoja. Nawafahamu jamaa wameshakata karibu ya miaka 20 ukiwaona kama huwajui utadhani hawajamaliza hata mwaka katika ndoa yao kwa jinsi wanavyoonyesha kupendana hata kwenye kadamnasi.
 
Teh teh teh hii ya mkuu Bubu ni another experience ku-maintain inawezekana na ni kweli kuna watu wameweza ku-show up nadhani inatakiwa kuepuka kuchokana tu
 
mkeo tu ana matatizo! pole sana! wengine tunaenjoy tu kama kawa, awe mke awe kimada wote 'level' moja!
 
Kuna hii imenitokea sana, nikaulizia kwa baadhi ya watu nao pia wakaniambia kuwa hukumbana nalo ni kawaida, nikaona bora nililete hapa JF kwa magwiji.Mara nyingi ukiwa na mkeo ndani ya gari mmetoka, mnakuwa mmenuniana, hasa hasa mke ndiye anaanzisha mnuno, ukimuuliza kitu anajibu kwa mkato.Lakini kama unatoka na kimada au nyumba ndogo ndani ya gari kunakuwa na furaha ya ajabu,mabusu motomoto, mahanjumati ya kila aina...udi wa mawardi....mengine ni siri!
Wadau jamani hii imekaaje?
Wewe kweli mwisho sana!
 
Kaka siye tunaotumia usafiri wa dala dala, mambo ni tofauti kidogo.
ingawa kama nikiwa na kimada nitamuwahia siti (si unajua usafiri wa dala dala Dar ulivyo mgumu!)
Ila nikiwa na waifu tunagombania wote lakinin minuno hamna.
 
Kuna hii imenitokea sana, nikaulizia kwa baadhi ya watu nao pia wakaniambia kuwa hukumbana nalo ni kawaida, nikaona bora nililete hapa JF kwa magwiji.Mara nyingi ukiwa na mkeo ndani ya gari mmetoka, mnakuwa mmenuniana, hasa hasa mke ndiye anaanzisha mnuno, ukimuuliza kitu anajibu kwa mkato.Lakini kama unatoka na kimada au nyumba ndogo ndani ya gari kunakuwa na furaha ya ajabu,mabusu motomoto, mahanjumati ya kila aina...udi wa mawardi....mengine ni siri!
Wadau jamani hii imekaaje?

kama tulikuwa wote vile :D , was just talking about this in the morning nilipokuwa nasubiri usafiri, 90% is like that, inategemea mlivyoamka au mlivyokuwa mnatoka nyumbani!
 
Kuna hii imenitokea sana, nikaulizia kwa baadhi ya watu nao pia wakaniambia kuwa hukumbana nalo ni kawaida, nikaona bora nililete hapa JF kwa magwiji.Mara nyingi ukiwa na mkeo ndani ya gari mmetoka, mnakuwa mmenuniana, hasa hasa mke ndiye anaanzisha mnuno, ukimuuliza kitu anajibu kwa mkato.Lakini kama unatoka na kimada au nyumba ndogo ndani ya gari kunakuwa na furaha ya ajabu,mabusu motomoto, mahanjumati ya kila aina...udi wa mawardi....mengine ni siri!
Wadau jamani hii imekaaje?

Ila mimi huwa sitoki na kimada ndani ya gari. Lakini hilo la kwanza ni kawaida kwangu. Huwa tumenunuiana na hakuna mazungumzo akifika kwenye kazi yake anashuka kama alikuwa kwenye Daladala
 
Tatizo liko hapa kwenye ku keep time!Wakati wa kuondoka kina mama wengi huchelewa kwa sababu mbali mbali,mara kujipodoa mara uji wa mtoto,maagizo kwa dada hatimaye amesahau simu yake chumbani,anataka kurudi ndani ,Huyu baba tangu alipoingia kwenye gari yeye shughuli zake ni kidogo mipango mingi iko kule aendako,maamuzi mazito ya kikazi kwa siku hiyo,Kwa hiyo akili yake yote inamtuma kufikiria kuwahi to keep time!Linalofuatia hapa ni honi mtindo mmoja na mama akiingia kwenye gari hana haraka huku akitoa maneno makali kwamba yale aliyokuwa akifanya ni muhimu pia.Wakiingia barabarani hakuna wa kuongea na mwenzake labda awepo abiria mwingine lakini wawili hawa majibu yao yana usongo wa yale ya kule walikotoka.

mkuu Kimatire hasa hiyo ndiyo sababu. Mimi huwa wakati mwingine nikingoja sana ndani ya gari anakuta nshaambaa nikirudi mnuno siku 3
 
watu wenye mtazamo mfupi ndio wanaweza kuwaza kuwa eti mwanamume huwa hana maambo mengi nyumbani mipango mingi iko huko aendako!!!!!! msisahau wanaume ni zaidi ya watoto wadogo... kuanzia chupi aliyovaaa kaandaliwa na mkewe huyo anaeonekana mzembe... chupi soksi suruali shati tai kitana vyote hivyo mwanamume huwa haoni peke yake hadi aonyeshwe na mke, watoto ni wenu wote lakini always mwanamke ndiye anaewajibika kujua wataishi vipi mchana kutwa!!! na bado mwanamke huyo ana ajira yake na wakati mwingine ya kipato kikubwa kuliko mumewe, sema wanaume huwa mnawaza nikifika niwahi kupata supu na hawara wake, hamna lolote la maana eti majukumu............ majukumu my foot!!!
 
Kuna hii imenitokea sana, nikaulizia kwa baadhi ya watu nao pia wakaniambia kuwa hukumbana nalo ni kawaida, nikaona bora nililete hapa JF kwa magwiji.Mara nyingi ukiwa na mkeo ndani ya gari mmetoka, mnakuwa mmenuniana, hasa hasa mke ndiye anaanzisha mnuno, ukimuuliza kitu anajibu kwa mkato.Lakini kama unatoka na kimada au nyumba ndogo ndani ya gari kunakuwa na furaha ya ajabu,mabusu motomoto, mahanjumati ya kila aina...udi wa mawardi....mengine ni siri!
Wadau jamani hii imekaaje?

Kwanini kila mtu asiendeshe gari lake?

Wanaume acheni ubaili wanunulieni wake zenu magari! EBO!

Ndio maana wananuna!
 
mkuu Kimatire hasa hiyo ndiyo sababu. Mimi huwa wakati mwingine nikingoja sana ndani ya gari anakuta nshaambaa nikirudi mnuno siku 3
ndio maana karibu kila mwanamke siku hizi anataka kumiliki gari lake hata ikibidi kuji-express herself (kuuza TIGO)!!!!!!!! ujinga mtupu eti utimke uniache, hakuna rangi utaacha kuona... kama hukukuta kesho nimetimka 11 alfajiri na kukuacha home uonje uchungu wa daladala za asubuhi..... mie napenda usawa kulikokitu chochote
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom