Mume kutembea na "zana" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mume kutembea na "zana"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chocolate, Mar 3, 2009.

 1. Chocolate

  Chocolate Senior Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Last Sunday nilikwenda kumtembelea rafiki yangu lakini katika maongezi nikagundua hali haikuwa shwari kati yake na mumewe. Baada ya kuwa peke yetu ikabidi nimuulize kulikoni? Akaniambia kuwa amekuta kwenye makabrasha ya mumewe kumehifadhiwa zana (condoms) na kabla hajamuuiliza mume akatoka kwa muda mrefu (Saa tano asubuhi na kurudi mida mibovu usiku sana) akiwa hana zile zana. Mke ikabidi aulize na hapo ndipo ugomvi mkubwa ukazuka. Sasa mke hana raha anaona usalama tena haupo je tumsaidieje?
   
 2. Mchola

  Mchola Member

  #2
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo rafikio alitakiwa amwombe mumewe uroda mara tu walipokuwa kitandani na kama jamaa angeshindwa kudeliver kama ilvyokuwa kawaida angemuuliza kulikoni? Hapo angekumbushia na zile condoms alizoona kwenye kabrasha!! jamaa angekamatika kilaini!!! tena angeomba radhi!! Huyo rafikio amshukuru Mungu mumewe anatumia angalau zana!! Sitetei uhalifu lakini natoa strategy ya kumkamata mhalifu!!

  Kuhusu ushauri mie nadhani wakae wazungumze bila kupigishana kelele. Kama jamaa hatokubali kwamba ametmebea nje ya ndoa basi mama aweke mtego atamnasa jamaa siku nyingine!!! Cha msingi sasa hivi mama akapime afya na aendelee na uchunguzi wake hadi hapo atakapomkamata!!
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...labda mume ni mjasiriamali, muda si kigezo, kuzunguka mitaani kutafuta wateja (wa condom mpya) yaweza kuchukua hata zaidi ya masaa hayo, na wateja wengine kuwa-convince ni mpaka ufanye majaribio na kusubiri matokeo ya hiyo product.

  Ajaribu kuelewa na amsamehe tu.
   
 4. k

  kalld Member

  #4
  Mar 4, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama anatembea na zana basi anamjali na anajijali !anajilinda na ajali kazini .amsamehe
   
 5. Jeni

  Jeni Senior Member

  #5
  Mar 4, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 199
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakuunga mkono Kalld. Ashukuru amezikuta hizo zana na akazitumia inamaana jamaa anajali na wala asikisarike azidishe upendo kwa mzee
   
 6. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Matangazo yametuathiri sana ingawa yanafaa kwa kutulinda. Matangazo yote ya kondomu yanadai tuache zinaa, tuwe na mpenzi mmoja na tukishidwa tutumie kondomu, sioni tatizo la mume kukutwa na kondomu, na bado sio kigezo cha kufanya uzinzi. Tatizo kubwa la wanawake ni kupenda kupata majibu rahisirahisi kwa mambo yanayohitaji majibu mujarabu kwani si kweli kuwa aliyepo chumbani basi kalala. Kwa ufupi afanye uchunguzi wa kutosha na sio kukurupuka
   
 7. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana mama, namshukuru Mungu kwa yote, ila hiyo ni dalili tosha kwamba mwenzio sio muaminifu kabisaaa. Kapime miwaya ukiwa fit shukuru Mungu. Yani kwa kweli jamaa hana aibu kweli. Na mwambie aanze na yeye kubeba condom kwenye pochi yake...atakaye kuja tumia naye na huyo mume vilevile pia atumie naye kama bado wanataka kuendelea na maisha. Duh!
   
 8. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Makubwa, kapime ukimwi dada angu. Kama uko ok, muanze kutumia zana wote.
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...je mke akikutwa na 'morning after pill' packet kwenye pochi, na few pills missing mtasemaje?
   
 10. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  1. Jitulize kwanza, punguza hasira, busara ni bora kuliko mitulinga.
  2. Fanya HIV test, kama uko salama, acha kutembea na mumeo mpaka uhakikishe naye yupo salama.
  3. Ipeleke issuekwa wzazi/msimamizi wenu wandoa maana ndio kazi yake hasa anapofanywa msimamizi wa ndoa wenu waeleze hatari anayoileta mume wako.
  4. Kaa mjadiliane
  5. kama hataki yeye sio OXYGEN, thamini maisha yako kuliko kuwa na yeye.
   
 11. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  well said ma dia! ningekuwa mie ningeleta mtafaruku wa kinafiki ili kumkemea kidogo but rohoni nashukuru kwamba anakumbuka condom, btw hakuwa mwaminifu siku hizi bora huyo anakumbuka zana!
   
 12. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  haaa jamani kuna issues za kupeleka kwa wazazi, haya mambo ni ya kuweka sawa nyie wenyewe wana ndoa.
   
 13. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  haaa jamani kuna issues za kupeleka kwa wazazi, haya mambo ni ya kuweka sawa nyie wenyewe wana ndoa.
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  haaa jamani kuna issues za kupeleka kwa wazazi, haya mambo ni ya kuweka sawa nyie wenyewe wana ndoa.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyo mama punguani kweli.
  Angetakiwa ammpongeze baba watoto kwa kujali....inaonyesha baba yupo makini kweli maana anatumia zana.....je angekuwa anajipigia kavu huyo mama angejua?
  Afadhali ameziona na sasa awe na uhakika mme wake anajali hasahau zana na inatakiwa huyo mama awe ananunua zingine kama siku za week ana muwekea kwa koti.
   
 16. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole na Hongera dada. Mimi nadhani hiyo si dalili ya huyo bw.kutokuwa mwaminifu. Hiyo ni dalili kuwa mvua inakuja. i.e ni dalili kuwa humtoshelezi!ndio maana ana haha haha huko nje kutafuta aridhike. Nampongeza huyo baba kwa sababu katika tafuta tafuta yake anahakikisha hakuletei ugonjwa wa aina yoyote. Hayo yote 9,kama roho yako inaona danger achia ngazi,wenye nguvu wapande waende zao juu(wanaume wenyewe wachache lazima kina dada mkubali kugawana,maisha mafupi!
   
 17. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Ni kweli mkuu,matangazo yanachochea sana kasi ya watu kupenda uroda;na nafikiri lengo lao limekaa kibiashara zaidi kuliko huduma.
   
 18. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Fidel hivi huyu dada mmemuelewa lakini maelezo yake? Naona wengi mnampongeza jamaa kuwa anajali...how far are you people?? Kukutwa na condom kisha ukaondoka uliporudi hazipo haina maana kuwa ulienda kuzitumia jamani. Huyo wanatakiwa wote waende kupima tu mambo ya kuwa eti kukuta condom ndani ina maanisha jamaa anajali si kweli. Kuna rafiki yangu tulikuwa tunaishi gheto moja mle ndani tulikwa tumeweka box la condom for easy accessibility lakini na jamaa tulikuwa tukipiga story night anadai alikuwa ana-maintain kutumia condom, just last week binti kaleta kizaazaa ana mimba na kwenye box condom zinapungua siamini kama napunguza peke yangu!!!
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,461
  Likes Received: 81,711
  Trophy Points: 280
  Nasikia siku hizi baadhi ya akina Mama ambao waume zao wana kazi zinazowafanya wasafiri sana ndani hata nje ya nchi huwawekea condoms ili kujikinga huko waendako. Pia niliwahi kusikia katika mazungumzo mwanadada mmoja akilalamika kutoa mimba nyingi (tayari walikuwa wameshajaliwa watoto wanne) mwenzake akamwambia kwanini wasitumie condoms akasema mume wake atumie condoms nje ya ndoa yao lakini yeye kamwe hatakubali kutumia condoms ndani ya ndoa yao na njia nyingine za kuzuia mimba alikuwa anaziogopa side effects.
   
 20. Lowenstern

  Lowenstern Member

  #20
  Mar 6, 2009
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza pole mpendaji, na alifanya makosa kutomuuliza mwenzi wake kuhusu zana alizokuwa nazo mfukoni, coz kama angeuliza angeepusha mambo flani na mume angekuwa na woga but kwa sasa hana kidhibiti hata akimuuliza mumewe anaweza kukataa 'hakuwa nazo' anyway jambo tayari limetokea chakufanya amtege na ajifanye hajali wala hamfatilii but under the carpet afatilie na kujua kitu na box zilipo tumika hizo zana. pole sana hayo ndio mambo ya ndoa mdada wala asiwe na hofu atavuka tu!!!!
   
Loading...