Black Coffee
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 1,931
- 3,177
Habari zenu wanajamvi wenzangu.
Kwa mara ya kwanza naleta kisa hiki cha rafiki yangu wa karibu. Kwanza mtanisamehe kwa uandishi wangu, mimi sio mzuri wa kuandika kwa mpangilio!
Shoga yangu huyu kaolewa ana mtoto mmoja na ana ndoa ya miaka mitano. Shida inakuja alimkuta mwanaume na mtoto 1 hivyo baada ya kuolewa ikabidi aishi naye yaani kiufupi ni familia ya watoto 2.
Tatizo kubwa ni mahusiano ya mama huyo mtoto na mume wake, wamekuwa na mawasiliano yasioleweka. Akiuliza anaambiwa 'we are parents' (Inasemeka walishawahi kuishi wakapata huyo binti ila wakashindwana baada ya mwanamke kwenda nje kusoma kwa nguvu na akatelekeza mtoto wa miezi 6).
Sasa mama alisharudi bongo na ana kazi na kipato kikubwa tu ila hajaolewa! Ratiba iliyopo mtoto anakwenda kwa mama yake kila likizo na ameanza kumchukia mama anayemlea.
Majuzi kaanza kuleta zawadi perfume, soski na T-shirt kwa mume wa rafiki yangu. Baada ya rafiki kuchachamaa zawadi zirudishwe kaambiwa "we are parents sio ajabu kutumiwa zawadi na siwezi kurudisha ila kama hujapenda hazitatumwa tena am sorry"
Kwa madai yake mume wake anampenda sana hajabadilika ila kaambiwa asiingilie mambo ya mtoto ukizingatia yeye ndo anaishi naye(duuh)
My Take: Anaibiwa apige chini anasema anagopa kuwa single mom ila mshaurini na nyie ntampatia asome ushauri wenu.
NB: Ugomvi upo muda baada ya mawasiliano ya karibu na mzazi mwenzie kuzidi. Kikao cha ndugu kilishakaa hakuna cha maana na ndugu wanamtetea yule mama sababu ya pesa kawa karibu na ndugu wa mwanaume kuliko huyu wa ndoa.