Je, mwanaume anaweza kumbaka mke wake wa ndoa?

kwa ufupi sana,
...............nina jirani yangu ambaye pia ni ndugu yangu,ameoa miaka mitatu iliyopita na wanapendana na mkewe, wote niwafanyakazi wa hospital ila tofauti!!!mwaka huu mwanzoni,january,mungu aliwajalia,mkewe akajifungua kwa operation,katoto kazuri kakiume ila haikuwa riziki,baada ya siku moja kakafariki,ilikuwa huzuni sana!!basi tukamzika na maisha yakaendelea na wakamsahau!!

Kwenye mwezi wa saba,ulitokea ugomvi mkubwa baina yao,wakitishiana hata kuuana basi mama mdogo wa mume (anakaa jirani kidogo pia) akamwomba mume kuwa mkewe akakae kwake ili wasuluhishwe, akakubali na baada wiki kikao cha usuluhishi kilifanyika.

Mimi nilikuwemo kikaoni na mke akadai kuwa mume alitumia nguvu kufanya tendo la ndoa wakati afya yake ilikuwa haijatengemaa, ndio chanzo cha ugomvi na mbaya zaidi imepelekea apate mimba jambo ambalo kiafya alikuwa bado hashauriwi,basi yaliongelewa weeeeee...

Yakaisha na wakashikamana tena japo mke alionyesha bado kusononeka sana!!sasa wiki iliyopita yametibuka upya kuliko ile ya kwanza,mume kachacha kwamba mkewe ametoa ile mimba kimya kimya kwani kuna siku mke alilala zamu kama siku tatu hivi(ni kawaida pia na mume huwa anakuwa zamu) hivyo inaonekana alitumia nafasi hiyo kuitoa!!!!.......

Tunajianda kwa usuluhishi tena,nikaona niwashirikishe nyie wadau muhimu katika visa mbalimbali vinavyojiri katika ndoa huku mitaani,licha yakwamba zinafundisha pia nitapata points zaidi za kuongea huko......jamani hiyo hali mnaionaje? Nani alikuwa sahihi hapo? Nini kifanyike katika hizi ndoa zetu maana matatizo hayaishi kila kukicha
 
Ningefunga kamba wote wawili naanza kuchalaza viboko..............kwamba
Kwanini mume amlazimishe mwenzie wakati bado afya yake sio nzuri
Na kwa nini mama atoe mimba akati ndio ishaingia hivo
 
Inawezekana ilikuwa hatari kubeba mimba nyingine now,
so maybe ni sahihi....kwa jinsi nilivyoelewa
 
Sometimes marriages are so ugly! I thnk huyo dada ako na kosa, mumewe alikosea ikanasa, naye kakosea kuitoa bila ridhaa ya mume hata kama hakuitaka mimba. Kwa vile anafanya kazi hospital alishindwa nini kumwomba huyo aliemtoa apike jungu kuwa mimba inacomplication so ni lazma itolewe ili wakubaliane? Hakufikiria na hilo laweza isambaratisha hiyo ndoa. By the way, why aitoe hali yuko ndoani na pia haikuwa imemletea madhara? Au...,!
 
Sometimes marriages are so ugly! I thnk huyo dada ako na kosa, mumewe alikosea ikanasa, naye kakosea kuitoa bila ridhaa ya mume hata km hakuitaka mimba. Kwa vile anafanya kazi hospital alishindwa nini kumwomba huyo aliemtoa apike jungu kuwa mimba inacomplication so ni lazma itolewe ili wakubaliane? Hakufikiria na hlo laweza isambaratisha hyo ndoa. By the way, why aitoe hali yuko ndoani na pia haikuwa imemletea madhara? Au...,!
Maswali ya kujiuliza kama hayo yako mengi sabry, hata mimi nilijiuliza pia kwa nini hakupika jungu hilo? hata kama, sidhani kama mume angekubali ukizingatia kulishatokea ugomvi wa mimba hiyo!!au labda mungu alimfumba asipate wazo la kupika jungu hilo? Kweli ndio zina raha na karaha
 
duniani kuna mambo...............................

We acha tu Mkuu!! Yaani kila siku tunasoma mambo ya kustaajabisha sana. Mkeo bado hajapona vizuri baada ya kujifungua halafu unaenda kumbaka!!!! Mijitu mingine ina ny*** ambazo si za kawaida kabisa na kuwafanya wawe kama wanyama!!!! dah!
 
Mhhh Ole wetu sisi wanadamu, Maajabu hayaishi. Kuna jamaa aligombana na mkewe kwa kuwa baada ya mkewe kujifungua kwa operation jamaa hakutaka kumgusa Mkewe kwa miaka miwili mpaka opone kabisa sasa huyu anmwingilia mwenzie kwa nguvu lol! Kilichopo hapo kwa kuwa mara ya kwanza aliyekosea ni Mume waksameheana sasa zamu ya Mke kusamehewa huyo jamaa asijifanye kukomaa kwani operation mfululizo nazo ni hatari sana
 
Huyo mume alimuuliza kwa nini katoa mimba? Kama afya ya mkewe ilikua hatarini je? Na kama aliweza kumbaka mkewe atashindwa kukataa mimba isitolewe hata kama imetunga nje ya mji wa mimba?
 
Huyo mwanaume ni kichaa kabisa...atamlazimishaje mwenzie wakati bado hajapona vyema...
Huyo mwanamke nae angemweleza mumewe kuwa kashika mimba na kiafya lazima atoe... ni ajabu wote wanafanya kazi hospitali ila hawajui afya ya uzazi kabisa
 
fabinyo,

Hivi kumbe unaweza ukampenda mtu mpka kufikia kumbaka? Kama ni madaktari hao ndo wale wanaomfanyia mtu operation ya kichwa wakati mgonjwa anaumwa mguu! kiukweli hapo iko kazi kwani kila mmoja kafanya kosa tena kubwa tuu ila mimi wa kumlaumu kwanza ni huyo mwanaume (kubaka) kwani yeye ndio aliopelekea mwanamke kutenda kosa la kutoa mimba japo hapo upungufu wa maarifa kwa uyo mwanamke ndipo ulioonekana... kama hali ndio hii, basi tunaomba jukwaa la kusuluhisha ndoa, na mahakama ya ndoa ikiwezekana pia
 
We acha tu Mkuu!! Yaani kila siku tunasoma mambo ya kustaajabisha sana. Mkeo bado hajapona vizuri baada ya kujifungua halafu unaenda kumbaka!!!! Mijitu mingine ina ny*** ambazo si za kawaida kabisa na kuwafanya wawe kama wanyama!!!! dah!
hahahaha, umepata hasira sana naona, ndio hivyo
 
Huyo mwanaume ni kichaa kabisa...atamlazimishaje mwenzie wakati bado hajapona vyema...
Huyo mwanamke nae angemweleza mumewe kuwa kashika mimba na kiafya lazima atoe...ni ajabu wote wanafanya kazi hospitali ila hawajui afya ya uzazi kabisa.
...hapo ndio unaamini mganga hajigangi
 
Kubaka ni kosa la jinai. Kama umebaka utaadhibiwa kama mahakama ikiprove kwamba umebaka. Suala la kwamba ni mke wako si utetezi. Mke wako anaridhaa na anamaamuzi kama binadamu mwingine, kama hataki usimlazimishe.
 
Kubaka ni kosa la jinai. Kama umebaka utaadhibiwa kama mahakama ikiprove kwamba umebaka. Suala la kwamba ni mke wako si utetezi. Mke wako anaridhaa na anamaamuzi kama binadamu mwingine, kama hataki usimlazimishe.

Sheria ya wapi unaiongelea we ndugu? Hakuna kitu kama hiki Tanzania labda mkiwa kwenye lawful separation. Otherwise unyumba umeangaliwa kijamii zaidi, kumbuka law emanates from the society kwa hiyo waliangalia suala la jamii yetu mtu umeoa au kuolewa then mwenza wako anakunyima unyumba unreasonably. So mapendekezo yalikuwepo ila waliyakataa baada ya kuconsider walengwa wa sheria hiyo.

Huwezi kumbaka mkeo kwa sheria ya kwetu though it is a rebuttable presumption.
 
Sheria ya wapi unaiongelea we ndugu? Hakuna kitu kama hiki Tanzania labda mkiwa kwenye lawful separation. Otherwise unyumba umeangaliwa kijamii zaidi, kumbuka law emanates from the society kwa hiyo waliangalia suala la jamii yetu mtu umeoa au kuolewa then mwenza wako anakunyima unyumba unreasonably. So mapendekezo yalikuwepo ila waliyakataa baada ya kuconsider walengwa wa sheria hiyo.

Huwezi kumbaka mkeo kwa sheria ya kwetu though it is a rebuttable presumption.

Hapo pekundu scenario ikiwa hivyo sawa. Lakini iwapo mwenza wa ndoa anakunyima unyumba reasonably nawe unatumia nguvu kulazimisha - inatakiwa uwajibishwe. Hivyo kutokuwapo kwa sheria hiyo Tanzania sio sahihi.
 
Sheria za Tanzania kuanzia Cap 16, mpaka Law of Marriage Act 1971 hazitoi nafasi kwa mwanandoa ku institute criminal proceeding kwa allegations za kubakwa cz presumption ni kua wanandoa wako kwenye lawfull marriage. Ingawa hiyo inawezekana kama tu wameseparate na tukio likatokea kipindi cha separation au wako divorced kbsa.>!!!!
 
Mwanafalsafa mmoja anasema hivi:"marriage always and everywhere is the more or less stable heterosexual relationship that society recognizes as the community in which it is appropriate for a man and a woman to engage regularly in sexual intercourse, and to beget and raise children" (LIVING A CHRISTIAN LIFE : Marriage, Sexual Acts, and Family Life).

Fasili ya neno "ndoa" katika sheria yetu ya ndoa ni ya hovyo kidogo. Lakini, tukianzia kwa mwanafalsafa huyu inafuata kimantiki kwamba, marriage entails a "continuous consent" to sex. That's why, sheria yetu ya ndoa ilisita kusema kwamba mume anaweza kuadhibiwa kwa kumbaka mkewe. I think, to this extent, sheria yetu ni rational.
 
Back
Top Bottom