Mume huyu anastaili msamaha??

kisasangwe

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
292
52
Hi everyone. nimekua nikipitia JF kila siku, kwa kweli nafurahia kuwa kuna ufumbuzi wa matatizo mengi sasa wajameni hebu saidia hii rafiki yangu.

NI MWAKA NA MIEZI KADHAA TANGU WAMEFUNGA NDOA,WANA MTOTO MMOJA, TANGU WALIPOKUA WACHUMBA BWANA ALIKUA ANAMCHUNGA SANA MPENZIWE, IKAWA NI AMRI KUVAA HIJABU AU NIKABU KABISA KAMA WANAENDA SEHEMU YENYE WATU WENGI,HII YOTE NI KWA VILE ALIOGOPA KUA MKEWE NI MREMBO SANA NA ANGETONGOZWA NA VIDUME WENGINE. SASA BAADA YA NDOA MAMBO YAKAWA TAIT ZAIDI MAANA HATA HAKURUUSIWA KUWA NA MARAFIKI,SIMU ILIKAGULIWA KILA DAKIKA NA HAKUTAKIWA KWENDA POPOTE.INGAWA BINTI NI GRADUATE ALIAMBIWA ASITAFUTE JOB KWANZA ILA BAADAE AKARUHUSIWA KWA MASHART KUWA SI MAKAMPUNI BINAFSI. ILA BWANA YEYE NI MFANYA BIASHARA NA MARA NYINGI HUSAFIRI NA KUACHA ULINZI WA NDUGUYE KWA MKEWE.BAADA YA MIEZI MITATU BI MKUBWA AMKUTA MMEWE BAFUNI AKIMCHABO HG,ALIPOMULIZA HAKUTOA MAELEZO KAMILI,MWEZI BAADAE YULE HG ALIJAONDOKA BILA KUAGA,AKALETWA MWINGINE HUYU NAE HAKUKAA SANA AKAMWAMBIA BI MKUBWA KUWA SHEMEJI ANAMGHASI, SIKU YA SIKU BWANA AKAMWAGIZA MKEWE AENDE KUFUATILIA MZIGO SEHEMU,BAHATI MBAYA ALIPOONDOKA ALISAHAU POCHI KURUDI AKAMKUTA BWANA ANABURUZA HG KUINGIA CHUMBANI KWAO,ALIPOULIZA HAKUJIBIWA NA BWANA AKAONDOKA HOME KWA SIKU TATU. HAYO NI BAADHI TU ILA MBAYA NI PALE ALIPOANZA KUWATONGOZA NA KUTEMBEA NA BAADHI YA MARAFIKI ZAKE HUYU BI MKUBWA. KUNA KIPINDI ALIONDOKA AKADAI ANAKWENDA MOROGORO KWENYE BIASHARA LAKINI KUMBE ALIKUA KWA NYUMBA NDOGO MANZESE. MKWEWE ALIPOGUNDUA AKAMULIZA ALIAMBULIA KICHAPO USIKU WA MANANE NA MUME KUTOWEKA KWA WIKI. ALIPORUDI BI MKWUBWA AKASEMA ANAKWENDA KWAO MUME AKAITIKA ILA AKAMWAMBIA ASIMJUE KWA MATUMIZI YA MTOTO. MCHANA,BWANA AKALETA GARI AKABEBA VITU VYOTE VYA NDANI NA FUNGUO AKARUDISHA KWA MWENYE NYUMBA.
MUNGU SI ATHUMANI BI MKUBWA KAPATA KAZI WIZARA FLANI AKAHAMIA MIKOANI NA MWANAE, MIEZI SASA IMEPITA JUZIJUZI BWANA KAMSAKA NA ANATAKA WARUDIANE,BINT ALIPOGOMA HUYU BWANA ANAMPA VITISHO NA KUDAI KUA ANAO WATU HUMO WIZARANI WANAOWEZA KUMHARIBIA KAZI, ALIPOONA HATISHIKI BWANA AMEANZA KUTUMA UJUMBE KWA BAADHI YA MARAFIKI ZAKE MKEWE KUSEMA KUA NI MALAYA NA ANATEMBEA NA VIGOGO FLANI,,KWAMBA NI MWATHIRIKA NA ANASAMBAZA VIRUSI HIVYO. AMETUMIA PIA EMAIL AD YA MKEWE KUTUMA UJUMBE WA AJABUAJABU KWA WATU WALIOKO KWENYE AD BOOK, NA PASSWD ALIKUA NAYO TANGU NI WACHUMBA,

SASA JAMANI Wana JF huyu dada anataka nimshauri kama rafikie wa karibu na mi kabla sijamwambia lolote nataka nyie mnambie, huyu bwana anasameheka
 
Ukikubali kuwa bata, ujue utakuwa unaharisha hovyo!!
kwa nn huyo demu alikubali masharti magumu ya jamaa hapo mwanzo?
itachukua muda kuwa kuku tena.
 
mwabie rafiki yako yani asikifikiri kabisa kurudi... nakama ni vitisho yeye sio wakwanza kufanyiwa hivyo most of the losers do the same....

If the password she can change it...
 
huyu mume amefanya uchafu mwingi kwa mkewe lkn mie kwa mtizamo wangu anaweza kusamehewa...endapo..atakiri kua alivyofanya ni vibaya..tena sana..na kwamba hata yeye asingependa mkewe amfanyie hivyo..na aahidi kutorudia..na mke awe na uhakika kua hatarudia tena..hiyo ndio maana ya for mema na for mabaya..na hayo ndio mabaya..yanaweza kua ni sehemu ya majaribu tu na wakiyashinda wakajikuta wakiwa na furaha ya ajabu iwapo watamtanguliza mungu.
 
Ukiona mwanaume ana hofu sana ya kutongozewa mkewe basi ujue na yeye ni kicheche. Hayo maelezo hapo juu yamedhirisha hilo. Mwanaume kama katembea na marafi wa mkewe si ajabu ipo siku atatembea hata na dada zake au hata mama zake wadogo!!!

Mwambie huyo binti aendelee na maisha yake tu wala asimjali! Maisha yenyewe mafupi halafu mtu mwingine anataka kumharibia!
 
huyu mume amefanya uchafu mwingi kwa mkewe lkn mie kwa mtizamo wangu anaweza kusamehewa...endapo..atakiri kua alivyofanya ni vibaya..tena sana..na kwamba hata yeye asingependa mkewe amfanyie hivyo..na aahidi kutorudia..na mke awe na uhakika kua hatarudia tena..hiyo ndio maana ya for mema na for mabaya..na hayo ndio mabaya..yanaweza kua ni sehemu ya majaribu tu na wakiyashinda wakajikuta wakiwa na furaha ya ajabu iwapo watamtanguliza mungu.

Mmmh! Wewe dada naomba nikuulize swali, UMEOLEWA?
 
hapo me ndio nasemaga kila mtu afate moyo wake unavyosema, ngumu kushauri watu wanaojifunika shuka moja..lakini ingekuwa mie hapo na kichwa maji changu haa ndio nitolee iyo...lyfe is 2 short kwa kweli hakuna wa kuniua ki fashion.
 
huyu mume amefanya uchafu mwingi kwa mkewe lkn mie kwa mtizamo wangu anaweza kusamehewa...endapo..atakiri kua alivyofanya ni vibaya..tena sana..na kwamba hata yeye asingependa mkewe amfanyie hivyo..na aahidi kutorudia..na mke awe na uhakika kua hatarudia tena..hiyo ndio maana ya for mema na for mabaya..na hayo ndio mabaya..yanaweza kua ni sehemu ya majaribu tu na wakiyashinda wakajikuta wakiwa na furaha ya ajabu iwapo watamtanguliza mungu.

vipi atakuwa na uhakika kama hatarudia?

achana nae huyo kwani kaumbwa peke yake? mbona wanaume wamejaa tena wazuri wazuri... :rolleyes:
 
Losers wote wako hivyo, vitisho mwanzo mwisho. Huyo mwanume wala hastaili hata kuitwa baba. Mwambie huyo dada ajipange aendelee na maisha. RB muhimu maana huyo mwanaume anaonekana mvurugaji.
 
huyu mume amefanya uchafu mwingi kwa mkewe lkn mie kwa mtizamo wangu anaweza kusamehewa...endapo..atakiri kua alivyofanya ni vibaya..tena sana..na kwamba hata yeye asingependa mkewe amfanyie hivyo..na aahidi kutorudia..na mke awe na uhakika kua hatarudia tena..hiyo ndio maana ya for mema na for mabaya..na hayo ndio mabaya..yanaweza kua ni sehemu ya majaribu tu na wakiyashinda wakajikuta wakiwa na furaha ya ajabu iwapo watamtanguliza mungu.
Mwanaume tangu lini abadilike? huyo dada asidanganyike wengi wamerudi kwenye ndoa walizozikimbia wakiamini waume zao wamebadilika kumbe ndia kwanza wamejua kua bado unamhitaji!

Ukimwi upo jamani!
 
tatizo watu wazinzi huwa wanajidai wana wivu sana
Mwanaume sio mwaminifu dada wa watu aanze tu maisha yake mapya kabla ya kuletewa mgeni huyu mgeni ..anayechukua watu kila kukicha
 
huyu mume amefanya uchafu mwingi kwa mkewe lkn mie kwa mtizamo wangu anaweza kusamehewa...endapo..atakiri kua alivyofanya ni vibaya..tena sana..na kwamba hata yeye asingependa mkewe amfanyie hivyo..na aahidi kutorudia..na mke awe na uhakika kua hatarudia tena..hiyo ndio maana ya for mema na for mabaya..na hayo ndio mabaya..yanaweza kua ni sehemu ya majaribu tu na wakiyashinda wakajikuta wakiwa na furaha ya ajabu iwapo watamtanguliza mungu.

ngumu sana kama si kusema haiwezekani kabisa.
 
mhhh mi inanipa kichwa moto manake ni friend yangu wa karibu sana hadi tumekua kama ndugu.
 
aachanne naye hana mpango mtu anayekuzushia kuwa unasabaza virus kwa ajili ya wivu na vitina ni sawa na muuaji tu.
 
Ushauri wangu kwa mawazo yangu huyo dada aende polisi akamchukulie RB huyo (muuaji) mumewe namwita muuwaji kwasababu hamtakii mema huyo dada. Pili anabalidilisha passward yake ama anabadili kabisa email address yake, hao ndugu wa mume nao hawana akili kama wanadai damu yao itarudi wasije mharibia maisha huyo mtoto, wamwache asome hadi amalize masomo yake maana babayake aliona huyo mtoto hana umuhimu ndio maana akaondoka na kuhama nyumba kabisa ikimaanisha hakutaka mawasiliano yoyote na mkewe sasa wanaona amependeza na ananawiri ndio anajua ni wa muhimu, Mume na nduguze wote ni wauwaji hawamtakii huyo rafikio maisha mema UKIMWI upo siajabu huyo baba kesha athirika nanataka mumwambukiza huyo dada.
 
Hata kama huyo mwanaume atakubali wakapime asirudi hamtakii mema rafikio, Mwambie rafikio asikate tamaa kwani wanaume wapo tena wazuri zaidi ya huyo muuaji kama kuolewa ataolewa tena na mwanaume anae jua nini maana ya mke na ndoa, Asikubali KUDANGANYIKA
 
Wanaume wengine wana wivu wa kutisha, halafu yeye anayafanya yale yale ambayo hataki mkewe ayafanye. Kajipinda miaka chungu nzima mpaka kapata degree yake halafu mwanaume kwa wivu wake hataki afanye kazi! Mwambie huyo dada hakuna ndoa hapo ni bora afikirie kufunga virago vyake mapema na kuanza moja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom