Mume huyu anapenda kazi kuliko mimi

Nashindwa kushangaa na miye aiseee kuhusu hawa ndugu zetu!!
Upande mwingine wanataka uwahudumie kila kitu..sasa bila kufanya kazi hela zinatoka wapi?
Mwambie huyo shogaako mradi anakula na kuvaa avumilie tu..mwambie mumewe anamtafutia maisha..si unajua maisha yalivyo magumu!...ngono sio muhimu kama ugali na samaki!!

makubwa basi,haya ya yote kisa tunaficha mishahara yetu?duh mboni kazi ipo my pacha!duh
 
Napenda kuishi na watu waelewa wasioipa ngono percent kubwa katika maisha ,watambuzi wakuweza kusoma alama za nyakati bila bughza.
 
Hapo kunaweza kuwa na matatizo mengi na ni vizuri kufikiria kwa mapana. Je, huyo jamaa kaanza hiyo tabia au alikuwa hivyo toka mwanzo wa mahusiano yao? Bila kujua jambo hili, napata shida kutoa comments zaidi.
 
The husband needs to learn how to balance between his work life and home life.

He needs to understand that life is not all about work or money.

Perhaps some form of counseling would help.

In order for that to be helpful he'll have to open up his mind for it to even have a prayer.

So him being open minded is of critical importance.

Otherwise his marriage could be doomed.

like!!well said
 
Kuna christmas moja nilimpigia mdada simu asubuhi, akaniambia mumewe yuko kazini! Sio askari wala daktari wala watchman! Ana 3 little kids! Imagine papaa not home on christmas day, na ni wakristo!
Kuna mabalaa mengine mtu hujitafutia!
may be anafanya kazi za viwandani.., niliwahi fanya kiwanda fulani cha vinywaji. christmas ndo ratiba ipo tait balaa.... hakuna kupumzika.
 
Labda anatumia kazi kuficha kitu. Unajua siku hizi magonjwa mengi...inawezekana kiwango kimeshuka...anaogopa kukwambia ukweli. AU labda ndivyo alivyo... ila angekuwa yuko fit sidhani kama kazi zingemsahaulisha gemu.
 
...ndoa nyingi zinazotetereka chanzo huwa ni malezi ya hovyohovyo toka kwa wazazi walikotoka...

najifunza tu.
 
Huyo atasababisha nichague kati ya kazi au yeye.
Na obviously nitachagua kazi yeye tu, so analazimisha red card tu!!

Ningekua mvivu wa kazi usingeniona na haya maisha mazuri nliyokua nayo, so probably usingenipenda.

So long as umehakikisha sipo nyumba ndogo piga kimya, otherwise kama unaweza kuni-sustain through your salary, I am gonna leave this job
 
Wakati mwingine hali ya uchumi inalazimisha mtu kukaa ofisini/mahali unapopatia rizki muda mrefu. Nakumbuka kile kipindi cha Mwinyi,sikukuu zilipokuwa zinafidiwa,mimi nilikuwa nalipwa kwa siku, kisia mwenyewe hali ilikuwaje hizo siku za fidia.

Inawezekana kelele za nyumbani zikamfanya mtu kukaa ofisini masaa mengi, ili ndege arudi tunduni mapema ni lazima kuwe na mazingira mazuri pia.

msome tena Nyani Ngabu utaewa maana yangu. Baba, sasa hivi babako na mamako kama wapo hai wanakumisi na kukutamani lakini ndo ishatoka hiyo. Ni muhimu kubalance muda wa familia na kutafuta. Kuna wazazi huwa wanakuwa surprised watoto wao kutoa mimba, kwa sababu they were too busy. Its ok kufanya kazi za ziada lakini usisahau kuangalia familia aisee. Kuna siku za kumpumzika na familia, walau eid ama krismas jamani.
 
Napenda kuishi na watu waelewa wasioipa ngono percent kubwa katika maisha ,watambuzi wakuweza kusoma alama za nyakati bila bughza.
suala sio ngono tu. Ndoa goes beyond that, its about companionship and being there to cherish the good memontos! Hawa ndo wababa wanajikuta hata hawawajui watoto wao!
 
Mimi ndio maana hao so called ma workaholic hazikuwa zangu...napenda mtu anaye socialize (mimi na yeye tu lakini. Lol).

Si lazima tuwe ma bilionea...cha kwanza ni furaha ya familia.

Kuna watu wako busy kutafuta tuuu...hata muda wa kutumia hawanaga. Hela za nini sasa kama zinakufanya mpaka ushindwe kutoa chakula cha usiku?

Watoto hata wasimjue baba. Nope.
 
ila jamani mnasema tu
kuna mazingira unajikuta bora uende kazini tu, hasa kama wewe ndiye 'bread winner'

unakuta watu wanasema 'kaa nyumbani basi leo' wakati huo huo hawana wazo hata moja la kipi kinatoka wapi na kwa gharama gani.

Ikifika jioni, tupeleke sijui God knows where for dinner au blah blah zingine, na wanajua kote huko ni pesa inahitajika.

Afu at the same time wanaomba innocently hata kuwanyima huwezi na unaona wanaenjoy kiasi gani.

Kama hujajipanga unaweza jikuta unafanya kazi extra hours sababu ya demand za watu wa nyumbani kwako mwenyewe, ni kuamua kupiga mstari tu.
 
Huyo atasababisha nichague kati ya kazi au yeye.
Na obviously nitachagua kazi yeye tu, so analazimisha red card tu!!

Ningekua mvivu wa kazi usingeniona na haya maisha mazuri nliyokua nayo, so probably usingenipenda.

So long as umehakikisha sipo nyumba ndogo piga kimya, otherwise kama unaweza kuni-sustain through your salary, I am gonna leave this job
Umeoa kaka?
Kwenye ndoa ili amani iwepo lazma kuwe na negotiations. Kuwa dictator works only if you are the president of this damned country from ccm!
Unatishia kuacha kazi kwa manufaa ama faida ya nani? Hivi hata kuweka muda tu wa kufurahia maisha ni ngumu? Mimi ningechagua kukuacha, uendelee kufanya kazi na ulete hiyo child support manake umeamua kuwa kihongwe.
 
mkuu sio wote, huenda mtoa mada hata hajaolewa. mf. kuna uzi nimeanzisha. kiukweli mhusika sio mimi cos mie sijaolewa. ni issue ya rafiki yangu ndio alinieleza nikamwambia tupange muda tuzungumze. nami nikaja humu kuomba maoni ya wenzangu!
its just that some ya hizi thread ziko 'too personal' so nikawa nashangaa. Not specifically kwa mtoa mada hii lakini nimeziona baadhi hapa MMU na zinatia mashaka, hopefully hujakwazika na my comment
 
Kongosho unadhani hao wanaofanya kazi namna hiyo ni masikini??? Mara nyingi ndio hao wana majumba yaso na idadi...wanaendelea kutafuta tuuuu. Huku wake zao wanaishia kumegwa na madereva huku wakionga ela za mtafutaji

ila jamani mnasema tu
kuna mazingira unajikuta bora uende kazini tu, hasa kama wewe ndiye 'bread winner'

unakuta watu wanasema 'kaa nyumbani basi leo' wakati huo huo hawana wazo hata moja la kipi kinatoka wapi na kwa gharama gani.

Ikifika jioni, tupeleke sijui God knows where for dinner au blah blah zingine, na wanajua kote huko ni pesa inahitajika.

Afu at the same time wanaomba innocently hata kuwanyima huwezi na unaona wanaenjoy kiasi gani.

Kama hujajipanga unaweza jikuta unafanya kazi extra hours sababu ya demand za watu wa nyumbani kwako mwenyewe, ni kuamua kupiga mstari tu.
 
Waliosema tajiri na mali zake masikini na watoto unadhani walikosea.
Kuna wanaoua watoto/wake kupata utajiri.
 
ila kweli wapo wengine wanapesa na ndio hawana hata muda wa wake zao.

Yaani kuna bosi mmoja lol
mkewe asipomegwa na muuza genge basi tena.

Maana anasafiri hata miezi 2, akirudi anakaa siku chache, max wiki moja na hapo anatoka ofisini saa 12 jioni.

Kongosho unadhani hao wanaofanya kazi namna hiyo ni masikini??? Mara nyingi ndio hao wana majumba yaso na idadi...wanaendelea kutafuta tuuuu. Huku wake zao wanaishia kumegwa na madereva huku wakionga ela za mtafutaji

Similar Discussions

Back
Top Bottom