Mume dhehebu tofauti na mke dhehebu tofauti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mume dhehebu tofauti na mke dhehebu tofauti

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Misana, May 25, 2009.

 1. M

  Misana Member

  #1
  May 25, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani nina jirani yangu yuko soo frustrated na suala la mke wake kuchukua family dominance kiimani kwasababu mwanzo walikuwa wanaenda njia moja na mmewe na watoto wao. Ghafla mke kaanza kwenda kusali sabato na watoto kila jumamosi na kumuacha mumewe akisimama kanisani mwenyewe. Sasa hii imemuadhiri mwanaume kwa kuona kama amebaki mwenyewe. Amejaribu kuongea na mkewe amegoma kusikia. Jamaa amesha tishia kumwacha mkewe kwani amekuwa akimislead watoto wa huyu baba. Tusaidiane afanyeje? this is a true story
   
 2. M

  Msindima JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mmmhhh,kwa nini mwanamke aamue kufanya hivyo?ulijaribu kukaa na huyo jirani akakueleza vizuri kuhusiana na hilo swala?Yawezekana kuna mgogoro ndani ya familia ndo maana mama akaamua kuchukua huo uamuzi,iko sababu.
  Jaribu kukaa na jirani yako akueleze vizuri,haiwezekani from no where tulikua tunasali dhehebu moja nibadili msimamo bila sababu.
   
 3. M

  Malila JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  je unajua kabla hawajaoana walikuwa dhehebu gani? kama walikuwa tofauti basi ujue ndo yale mambo ya kudhani kuwa unaweza kumbadilisha mwenza wako ndani ya ndoa. Kwa kauzoefu kadogo niliko nako juu ya wasabato, ni kwamba wako makini sana (wale wanaomaanisha juu ya imani yao),hawabadiliki/kuhamahama madhehebu.
   
 4. G

  Giroy Member

  #4
  May 25, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa uzoefu wangu ni vizuri kumtafuta mnayefanana imani.nimeona watu wakibadili dini hata dhehebu kwa ajili ya kuolewa au kuoa.Hii ni hatari sana kwa umoja wa familia.watoto wanaweza kukosa mwelekeo wa imani.pengine huyo mama alishawahi kuwa msabato,akaamua kubadili dini ili kupata mume.ndg awe mvumilivu pengine MUNGU atampa mlango wa kutokea,wakawa na umoja, asifanye maamuzi haraka.KUMBUKA KUNGURU Hafugiki akikumbuka porini huwezi kumzuia.
   
 5. D

  Deom New Member

  #5
  May 25, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wasabato husoma sana Biblia, kwa hiyo mshauri huyo bwana akae chini asome biblia. Aitafakari vizuri ajue ni kitu gani kimemshawishi mke wake kuhamia sabato. Wako wengi walifanya hivyo. Hata kama walikuwa dini moja na mume wake, halafu mke amepata ujumbe wa wasabato ukamkolea itakuwa vigumu kumtoa huko. Mshauri rafiki yako asiache ndoa kwa sababu ya dini madhara yake kwa familia ni makubwa sana baadaye. Ampe nafasi mke wake, wakae chini waongee vizuri nayeye afanye maamuzi sahihi kuhusu dini ya mke wake.
   
 6. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Amwache Mkewe anendelee na imani yake mpya, na yeye vivyo hivyo aendelee na Kanisa lake. Kwani si anakwenda kuabudu! Sasa bila Mkewe na watoto Mungu hatamsikia? Aendelee kumwombea Mkewe abadilika kama anadhani anakwenda njia mbaya. Wazo la kuachana alifute kabisa kwani litachanganya familia nzima na yeye akiwemo.
   
 7. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwauzoefu wangu Mungu hapendi kuhusishwa na siasa, hata zakifamilia. I dont see how mtu kuwa na imani tofauti ni tatizo other than the issue ya watoto. Lakini nadhani the besrt thing nikuwalea kujua mafundisho ya Yesy Kristo maana yeye alipokuwa duniani hakukuwa na wasabato, wakatoliki, walutheri etc.. infact kulikua hakuna ata wakristo as they exist today. Sasa tatizo hapa nini? Endoctrination inawafanya watu wawe wajinga. Na zaidi huyo mama hana busara. To be honest watoto nivigumu kuwa na dini in a true sence. They simply accept whatever they are taught and there is a need to make sure watoto wanafundishwa imani na wazazi mpaka pale watakapo kuwa tayari kutambua kinachowafaa. Their minds are young and unable to comprehend the difficult concepts of religion. Wanakuwa spoon fed simplified religious teachings which they take to be absolute truths and this is hardly ever the case. So kama wewe ni mkristo wafundishe watoto wako ukristo na kwa mfano wako mzuri watafuata tuu. Haya mambo ya madhehebu ni siasa tuu za binadam. People need to remember that.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,083
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana kwa majibu mazuri. Tumewaona watu wa dini tofauti wameoana na kila mmoja kubaki na dini yake na waliishi katika maisha ya ndoa vizuri tu huku kila mmoja akiheshimu dini ya mwenzie bila matatizo yoyote. Sasa hawa wote ni wakristo eti tofauti ya madhehebu tu inataka kumfanya mwanaume avunje ndoa!!! Hivi dhehebu lina umuhimu mkubwa kiasi hicho kwa huyo jamaa kiasi cha kutaka kuisambaratisha familia yake. Kama watu wa dini tofauti (Wakristo na Waislamu) wameweza kuishi katika ndoa bila matatizo ya kidini kwa nini huyu bwana asiendelee na ndoa yake na kuweka tofauti zao za kimadhehebu pembeni!!? Watu wengine wanapenda kuyakuza mambo!
   
 9. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Kama watu mpo dini moja ya kikristo, sioni kama dhehebu ni big deal inayoweza kusababisha ndoa ivunjike, labda huyo bwana ana jingine. Kanisa ni kanisa tu ilimradi linafundisha mambo ya Mungu.
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Imetulia sana hii ndugu yangu.
  Kuchanganya watoto kwa sababu ya dini ni kitu kibaya sana.Siasa za wazazi kwenye eneo hili ni sumu!
   
Loading...