Mume aua mkewe kwa kumshambulia kwa mchi wa kinu na kumpiga ngumi kutokana na ugomvi wa kifamilia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mwanamke aitwaye Paulina Daudi (30) mkazi wa Mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ameuawa kwa kupigwa ngumi na mchi wa kinu ‘mtwangio’ na mmewe aitwaye Samwel James baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba tukio hilo limetokeo Jumanne Januari 26,2021 majira ya saa tatu asubuhi na kutaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni ugomvi wa kifamilia.

“Paulina Daudi (30) mkazi wa Mageuzi alishambuliwa kwa kupigwa ngumi na mchi mdogo ‘mtwangio’ sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake aitwaye Samwel James akiwa nyumbani”,amesema Kamanda Magiligimba.

Ameeleza kuwa Paulina Daudi alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa Samwel James kwa kosa la mauaji kwani alikimbia mara baada ya tukio hilo.

Kamanda Magiligimba anatoa wito kwa wanandoa kuacha mara moja tabia ya kuwashambulia wenza wao.

Aidha amewasisitiza wanawake wote wanaofanyiwa vitendo vya ukatili mkoani shinyanga wavunje ukimya,wafunguke ili matatizo yao ya kifamilia yaweze kushugulikiwa yakiwa katika hatua za awali kabla madhara makubwa hayajatokea akibainisha kuwa vitendo vya ukatili ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwingine.
 
Kwa nini amekimbia baada ya kumpiga na mtwangio? Nimtie moyo tu asitishwe na agizo la kukamatwa kwake arudi home na mtwangio wake maana Kamanda wa polisi naye ni mwanamke tu hivyo akimfuatilia ampige mtwangio tu 😁
 
Ila Miss Zomboko habari zake hazijawahi kua nzuri.

Eti Serikali yajenga daraja sijui nini nini... Yeye ni Fulani kaua au kanyonga..
 
Si mnasemaga mpaka kifo kitapowatenganisha? Hapo kifo kimewatenganisha bila tabu kabisa.
Mkuu huu usemi Mimi huwa sikubaliañi nao,japo hata Mimi niliapa kwa kauli hiyo lakini kwangu haina uzito,I will marry even ten wives ikiwa tu hatuendani kiitikadi,haya ndo madhara ya kusema kifo kiwatenganishe,mtu unapitia machungu na mateso yasiyo mithirika harafu umekaa kusubiri kifo kiwatenganishe.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mwanamke aitwaye Paulina Daudi (30) mkazi wa Mtaa wa Mageuzi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga ameuawa kwa kupigwa ngumi na mchi wa kinu ‘mtwangio’ na mmewe aitwaye Samwel James baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba tukio hilo limetokeo Jumanne Januari 26,2021 majira ya saa tatu asubuhi na kutaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni ugomvi wa kifamilia.

“Paulina Daudi (30) mkazi wa Mageuzi alishambuliwa kwa kupigwa ngumi na mchi mdogo ‘mtwangio’ sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake aitwaye Samwel James akiwa nyumbani”,amesema Kamanda Magiligimba.

Ameeleza kuwa Paulina Daudi alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa Samwel James kwa kosa la mauaji kwani alikimbia mara baada ya tukio hilo.

Kamanda Magiligimba anatoa wito kwa wanandoa kuacha mara moja tabia ya kuwashambulia wenza wao.

Aidha amewasisitiza wanawake wote wanaofanyiwa vitendo vya ukatili mkoani shinyanga wavunje ukimya,wafunguke ili matatizo yao ya kifamilia yaweze kushugulikiwa yakiwa katika hatua za awali kabla madhara makubwa hayajatokea akibainisha kuwa vitendo vya ukatili ni uhalifu kama ulivyo uhalifu mwingine.

Poleni ndugu ,jamaa na marafiki , Mchi wa kinu ni silaha hatari sana!!!
 
Back
Top Bottom