Mume au mke kubadili dini kutoka ukristo kwenda dini nyingine, je, Kunaifanya ndoa yake ya kanisani kuvunjika kidini na kisheria baada ya kubadili?

Hapa tutaweka maelezo mengi, ndio maana kila tunashauriana kila siku mtu aoe/aolewe na wa dini yake, kimsingi kufanya hivyo ni kuepusha matatizo.

Mtu anaweza akawa dini yako leo..ila mbeleni akabadili dini akiwa ndani ya ndoa
 
As a general rule there can be no valid marriage where there is a subsisting marriage, until the latter is dissolved by the court.

.... Christian marriages a strictly Monogamous

..... Islamic marriages and Civil marriages are potentially Polygamous.
 
Ninavyoelewa ndoa ikishafungwa iwe katika dini yeyote,hapo tayari hutambulika kisheria.Mmoja kuhama dini haiathiri ndoa hiyo kwa kuifanya batili,ndoa huvunjwa mahakamani tu.
Kwa dini yeyote? Rekebisha hii sentesi katika uislamu yeyote atakayebadiki dini basi ndoa inakuwa batili hapo hapo na ni kila mmoja atafuata hamsini zake.
 
Kwa dini yeyote? Rekebisha hii sentesi katika uislamu yeyote atakayebadiki dini basi ndoa inakuwa batili hapo hapo na ni kila mmoja atafuata hamsini zake.

Anamaanisha ndoa ya dini yoyote huwa inasimamiwa na sheria za nchi. Mtu anapobadili dini haiwi sababu ya ndoa kuvunjika automatic kisheria.. ni lazima ivunjwe na mahakama

Siku hizi huwezi mpa mke wako talaka tatu ukasema umevunja ndoa sababu uislam unaruhusi.. ni lazima muende mahakamani wakaivunje kisheria.

Cheti cha ndoa iliyofungwa kiislam huwa kinatoka bakwata ambayo ni taasisi ya serikali.
 
Back
Top Bottom