Mume anapo-support ujinga wa mkewe!!!!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
AT least kwa hapa TZ, hususani ukanda wa pwani, wanawake ni watu wanaopenda sana mipasho na maongezi ya mafumbo!!! Bila shaka ni wahitimu wazuri wa baadhi ya tanzu za fasihi simulizi. Last week, nilimtembelea rafiki yangu mmoja ambae mwenzangu ameoa (mie bado hivyo natoa offer kwa mwana-jf single wa kike apendae kuwa na mume!).

Ile kuingia tu sebuleni, nikakutana na kibao kilichoandikwa "UKIJA UJE NA YAKO, UMBEYA NYUMBANI KWAKO!" Kwa bahati shemeji yangu (mke wa mshikaji) alikuwa hayupo kwa muda huo hivyo tukapata nafasi ya kutosha kujadili masuala ya kimaisha. Baada ya mimi kuona kibao hicho, nikamuuliza mshikaji kwanini ameweka hicho kibao.

Akajibu, aliyeweka si yeye bali ni mke wake! Nikamuuliza kawalenga akina nani; akajibu "sijui yeye mwenyewe!" Baada ya majadiliano ya hapa na pale, nikamshauri akiondoe kibao hicho kwani anafanya embrassement kwa wageni wake! Jamaa akadai kwa kuwa alikuwa ni mke wake basi asingeweza kukiondoa yeye mke wake na yeye ana haki na hiyo nyumba!

Kimsingi, nilishindwa kabisa kumshawishi kukiondoa kibao hicho! Na kama ningekuwa nina mazoea ya kwenda kwenda pale nyumbani au kukutana na huyu rafiki yangu basi bila shaka ningejisikia vibaya sana kuhusu ujumbe ule! Sasa swali ninalojiuliza na kuwauliza wadau, je; ni muhimu kuwa na vibao vyenye ujumbe wa aina hii kwenye nyumba zetu?

Hivi hatuoni tunaanza kumsuta mtu ambae hata kuongea hajaongea tayari unamkaribisha kwa masimamngo? Wengine unakuta wanaweka vibao vyenye ujumbe aina hii kwenye sehemu zao za biashara kama vile "HAPA CASH TU, KUKOPA HUKO HUKO!" HIVI ni busara kuwasimanga watu ambao hata mdomo hawajafungua?

NAWASILISHA!!!
 
ukiona nyumba ya mtu ina vibango vya maandishi kila kona ujue basi shule hakuna hapo hata ka ipo ni ndgo sana

af unauliza hicho kibao kawekewa nani akati we ndo uliekisoma usingekisoma basi kingekua hakikuhusu
 
Amewawekea watu kama ninyi! yahani wewe mwanaume mzima kuingia nyumba za watu unaanza kuchunguza mpaka maandishi yanakuhusu nini? na alijuwa mko kama ninyi maana kama leo umetoka na hilo kesho utatoka na jingine. Mambo ya kwenye nyumba za watu usipende kuingilia wewe kama sijui kuna vibao havikuhusu. Kesho utakuja na issue nyingine ukome babu wewe tena mi sikukaribishi mtu kama kama wewe.
 
Amewawekea watu kama ninyi! yahani wewe mwanaume mzima kuingia nyumba za watu unaanza kuchunguza mpaka maandishi yanakuhusu nini? na alijuwa mko kama ninyi maana kama leo umetoka na hilo kesho utatoka na jingine. Mambo ya kwenye nyumba za watu usipende kuingilia wewe kama sijui kuna vibao havikuhusu. Kesho utakuja na issue nyingine ukome babu wewe tena mi sikukaribishi mtu kama kama wewe.
mwenzangu wa pande zipi? maneromango, kimanzi au kisarawe!!!
 
Kawaida ni kua you can not choose mwenzio aishi maisha gani.... But ukweli unabaki ulooweka hapa ni kweli kabisa kua haipendeza... na thou waweza ona kama wanamsimanga mgeni wao... IMO hio inatoa picha the type of people they are... Hicho kibao says Loads kuhusu Watu wenyewe... mahala wanaishi... attitude towards watu wa nje... Na lack of busara ya kuweza tafakari kua hapo wageni ni aina nyingi na wengine hawastahili kabisa waone huo ujumbe.... as much as they mean it...
 
Hicho kibao kilikustahili hasa maana umeshaleta umbea ulioutoa huko!

Decent person hawezi kuweka maandiko ya kipuuzi ndani kwake unless kama wote wanaomtembelea ni watu wenye staili kama yake! hata wewe, kama una mabandiko kama hayo basi nakushauri uyaondoe mara moja kwani mtu mwenye heshima zake akija kwako na kukuta mabandiko kama hayo anaweza kuhisi kumbe upo si vile anavyokufikiria!
 
Mkuu kama wewe siyo mmbea basi huo ujumbe hautaweza kukusumbua akili..

MKUU, ujumbe haunisumbui lakini nikiwa kama rafiki wa yule mshikaji basi nina wajibu wa kumshauri chochote ninachohisi ni right hata kama sitakuwa right! Nazani ukimuona mshikaji wako ni kicheche basi bila shaka utamshauri aachane na mambo hayo otherwise u're not commited friends! na hiyo ndiyo raha ya kuwa na rafiki kv mara nyingi ni marafiki pekee ndio wanaoweza kutoa ushauri na ndio maana mara nyingi unaweza kumsikia mzazi akisema "hebu mshauri rafiki yako.......!" So, tell me something, unapomshauri mshikaji wako aache jambo fulani ni kwamba wewe unaguswa moja kwa moja na hilo jambo?! Tell me, kama unafahamu biashara za kileo zinazo-keep attention kwenye masuala ya huduma kwa wateja then unaenda dukani kwako unakuta muuzaji wako ameweka kibao "KUKOPA HUKO HUKO, HAPA CASH TU!" Wewe kama mmiliki wa biashara hiyo utachukua hatua gani?! Will u leave it, au utakiondoa?! Nilikuwa nafanya kazi mahali ambako kutokana na nature ya kazi ya pale ni sehemu ya kukutana na watu(wateja) kila wakati. nazani kwenye ofisi zinazohudumia wateja kunakuwa na vibao vilivyoandikwa CLOSED ambavyo ama vinawekwa kwenye meza ya staff au dirishani (in case of cashiers nd the like). Vibao hivi mara nyingi vinawaambia wateja kwamba the service is temporarily closed kwahiyo waende wakapate huduma kwa staff wengine. pamoja na vibao hivi, hapo ofisini nikakuta vibao vingine vimeandikwa DON'T DISTURB! Vibao hivi vilikuwa vinatumika pale staff anapokuwa na kazi nyingine na hivyo asingependa kukutana na wateja kama yeye yupo na wanamuona! Mbaya zaidi, unakuta mara nyingi mtu anaweka kibao cha DON'T DISTURB huku kuna wateja kibao wanahitaji huduma!! Nikavipinga kwa nguvu zote vibao hivi vya DON'T DISTURB hadi vikaondolewa ingawaje wengi waliokuwa wanavitumia ni wale walio juu yangu! Therefore, kushauri kitu sio lazima kiwe kinakuhusu moja kwa moja but unaangalia how civilised people live!!!
 
AT least kwa hapa TZ, hususani ukanda wa pwani, wanawake ni watu wanaopenda sana mipasho na maongezi ya mafumbo!!! Bila shaka ni wahitimu wazuri wa baadhi ya tanzu za fasihi simulizi. Last week, nilimtembelea rafiki yangu mmoja ambae mwenzangu ameoa (mie bado hivyo natoa offer kwa mwana-jf single wa kike apendae kuwa na mume!). Ile kuingia tu sebuleni, nikakutana na kibao kilichoandikwa UKIJA UJE NA YAKO, UMBEYA NYUMBANI KWAKO! Kwa bahati shemeji yangu (mke wa mshikaji) alikuwa hayupo kwa muda huo hivyo tukapata nafasi ya kutosha kujadili masuala ya kimaisha. Baada ya mimi kuona kibao hicho, nikamuuliza mshikaji kwanini ameweka hicho kibao. Akajibu, aliyeweka si yeye bali ni mke wake! Nikamuuliza kawalenga akina nani; akajibu sijui yeye mwenyewe! Baada ya majadiliano ya hapa na pale, nikamshauri akiondoe kibao hicho kv anafanya embrassement kwa wageni wake! Jamaa akadai kv alikuwa ni mke wake basi asingeweza kukiondoa yeye kv mke wake na yeye ana haki na hiyo nyumba! kimsingi, nilishindwa kabisa kumshawishi kukiondoa kibao hicho! Na kama ningekuwa nina mazoea ya kwenda kwenda pale nyumbani au kukutana na huyu rafiki yangu basi bila shaka ningejisikia vibaya sana kuhusu ujumbe ule! Sasa swali ninalojiuliza na kuwauliza wadau, je; ni muhimu kuwa na vibao vyenye ujumbe wa aina hii kwenye nyumba zetu?! Hivi hatuoni tunaanza kumsuta mtu ambae hata kuongea hajaongea tayari unamkaribisha kwa masimamngo?! Wengine unakuta wanaweka vibao vyenye ujumbe aina hii kwenye sehemu zao za biashara kama vile HAPA CASH TU, KUKOPA HUKO HUKO! HIVI ni busara kuwasemanga watu ambao hata mdomo hawajafungua?!

NAWASILISHA!!!

"ULIYOYAKUTA HUMU NDANI UNATAKIWA UYAACHE KAMA ULIVYOYAKUTA" kuwa mwangalifu mkuu ni hatari sana..
 
Kawaida ni kua you can not choose mwenzio aishi maisha gani.... But ukweli unabaki ulooweka hapa ni kweli kabisa kua haipendeza... na thou waweza ona kama wanamsimanga mgeni wao... IMO hio inatoa picha the type of people they are... Hicho kibao says Loads kuhusu Watu wenyewe... mahala wanaishi... attitude towards watu wa nje... Na lack of busara ya kuweza tafakari kua hapo wageni ni aina nyingi na wengine hawastahili kabisa waone huo ujumbe.... as much as they mean it...
kweli kabisa, watu tupo tofauti na ujumbe tunaouona tunatafsiri tofauti.........busara inahitajika.
 
Back
Top Bottom