lara 1
JF-Expert Member
- Jun 10, 2012
- 15,700
- 29,111
Wakubwa zangu shikaamooni!!!!!!!!!!!
Peopleeeeeeeeeessss!!!!!!!!!!!!
Habari nayoileta hapa inakinzana kabisaaaaaaaaa na siku ya ukimwi duniani ila Habari ni Habari iwe ya Kidaku, Kiumbea, Kimajungu, ama Kipashukuna ni Habari!!!!!!!!!!!
Kwenye viti virefu huko bwana kuna mjadala ulizuka jana juu ya Bi dada mmoja, Muke ya Mtz mmoja hivi, aliolewa na Kijana mwenzie! Sasa baada ya Muda Mwanaume akapata small house akaanza kumnyanyasa mwenzie! Mara we mwanamke gani, sijui nilikupendea nini, mbayaaaaa! Itakuwa uliniloga si bure, usiongozane na mimi wewe si hadhi yangu! Manyanyaso hata enzi za utumwa zina nafuuu!
Watu wakmsihi vumilia bi dada ndoa ndoano! Yatapita, hapo kazi huna utaenda wapi? Wakaweka vikao na vikao, Mwanaume kakomaaa mi simtaki huyu mwanamke mbayaaaa! Nimepata katoto kasupu, kichuna cha haja!, hili zee linanipotezea muda! Halali ndani, hamsemeshi, akimsemesha kashfa juu ya kashfa! Hapo miaka 3 ya ndoa! Kavumilia wee dada wa watu.
Siku moja akaamka akwaza mimi ndo kwanza im 25, hivi naupungufu gani mwilini kukaa humu ndani kama mtumwa wa mtu!? Kwani bila ndoa hamna maisha? Akafungasha vitu vyake vyote akaketi kumngojea Nyampara aje kumnyanyasa kama kawaida yake, Mwanaume kutinga akamwambia "Bwana mimi ndo naenda hivi, nakoenda sijui, ila nimesikia malalamiko yako, na miaka 3 ulionipotezea sio ishu, hicho kigari chako wala sitaki tugawane baki nacho, nigee talaka yangu tu nikagange maisha mbele ya safari! Mi fighter" Mwanaume kagoma kutoa talaka! Bi dada kajitwisha begi kichwani usiku wa saa 2, NDOA NDO IMESHA HIVOOO!
Siku mbili tatu kazoea ukweli kuwa sasa yuko mwenyewe, Miaka ikapita Mungu si Lara 1, akapata Buzi la hajaaa! Likamjengea nyumba huko mbezi beach! Usafiri nini, si yule muke ya Mtz tena! Mambo supaaaaaa! Toto limekuwa toto! Juzi juzi kahamia kwenye kigorofa chake mbezi huko. Ashasahau yooote, moyo mweupeee!
Hamad! Ugeni ukamjia ndani ya kigorofa chake!!!!!! Mumewe na wakwe zake wamekuja kusuluhisha!!!!!! Mume kaomba msamaha wewee, mpaka huruma! Baada ya kubembeleza siku kibao, bi dada karudisha moyo nyuma! Ila akamwambia " Mimi niko tayari tuanze upya sasa wewe nenda Kapange nyumba Sinza au Mwenge mimi nitakuja kuhamia, tujaribu kuishi wote tena! Hili jumba pamoja na kukusamehe huusiki nalo hata chembeee!!!!!! Nikija huko kwako hapa napangisha najipatia kodi! Ukishapata hiyo nyumba ya kupanga niambie nije" Kaka ndo hatujui ataamuaje!
Safi sanaaaaa bi dada! Pata Amarula na Sminorf ujipooze na kujipongeza kwa ushindi!!!!!!! Ingekuwa mtu mwengine Basi yameisha njoo tu uhamie hapa takaage! Thubutuuuuu!