Mume 'ameamua' kuwa na mtoto 'nje ya ndoa'!!!

linda0169

New Member
Jun 2, 2010
4
0
Ni mume kwa miaka zaidi ya 25.
Anasema ameamua kuwa na mtoto nje ya ndoa.
Ndoa ina mtoto mmoja, zaidi ya miaka 23.
Ni ndoa halali ya ki-kristo.
Mtoto alezaliwa hana mwaka. Mume kasema 'aliamua' .
Hii imekaa vipi? Hatua gani mke achukue hatua gani sahihi?
 
Mtoa mada.... napata shida kidogo kukuelewa hapo kwenye red color.

Haya ameamua tu?? HAkuna kuamua pasipo sababu? .... akueleze hicho kilichompelekea kuamua hivyo!!
 
mtoa mada.... Napata shida kidogo kukuelewa hapo kwenye red color.

Haya ameamua tu?? Hakuna kuamua pasipo sababu? .... Akueleze hicho kilichompelekea kuamua hivyo!!

mj1 mtoa mada naona amechanganyikiwa na maswaiba ya ndoa
 
Kuna wakati nashindwa kuwaelewa wanaume kabisaaaaaa,
Huyu Baba atakuwa na zaidi ya miaka 40 mpaka 50
leo anaenda kuzaa na mwanamke mwingine..hana lolote kacheza faulo kampa dada mimba matokeo ndio hayo dada kamganda umri huo ni wa kuamua kuzaa ?
mara 100000000000000000% nikute mwanaume ana mtoto kuliko aniletee mtoto nikiwa ndani ya ndoa ...

Pole sana dada ..nakosa hata la kusema hapa..
 
Mke ashukuru kupata mtoto wa pili, maana kwa sisi waafrika mtoto mmoja kama Clinton, sio zetu !
 
Noda ya watu 3, labda na zaidi - waiojulikana.
'UKIMWI' unapewa nafasi gani hapa?
UKIMWI + it's associated diseases.
Please people. think a bit deep. HIV/AIDS
 
Ni mume kwa miaka zaidi ya 25. Anasema ameamua kuwa na mtoto nje ya ndoa. Ndoa ina mtoto mmoja, zaidi ya miaka 23. Ni ndoa halali ya ki-kristo. Mtoto alezaliwa hana mwaka. Mume kasema 'aliamua' . Hii imekaa vipi? Hatua gani mke achukue hatua gani sahihi?

Miaka 25 ya ndoa, mtoto mmoja. Kwa nini mmoja? Waliamua au kulikuwa na tatizo? Kuna mambo mengi tu yanaweza kuchangia hasa kama kuwa na mtoto mmoja halikuwa suala la makubaliano bali matokeo tu.

Kwa kuzingatia umri wa ndoa, bila shaka wameshapitia majaribu mengi na kuyashinda hivyo hili la mtoto bado nalo linazungumzika. Lakini ni vema pia huyo mama katika maamuzi yake akazingatia pia hatari iliyopo kwenye hiyo ndoa ya kuambukizwa HIV (kama bado!).
 
Kuna mengi ambayo hayajawekwa wazi, ila nampa pole huyo mama kwani mme wako kupata mtoto wa nje si hali nzuri katika mahusiano ya wawili.
 
Noda ya watu 3, labda na zaidi - waiojulikana.
'UKIMWI' unapewa nafasi gani hapa?
UKIMWI + it's associated diseases.
Please people. think a bit deep. HIV/AIDS

pole Linda, ila napata taabu kukuelewa, sasa kama kuna ukimwi, sasa unauliza nini tena? kapime afya yako ufanye maamuzi!!! uamuzi unao mwenyewe

DN
 
Kuna wakati nashindwa kuwaelewa wanaume kabisaaaaaa,
Huyu Baba atakuwa na zaidi ya miaka 40 mpaka 50
leo anaenda kuzaa na mwanamke mwingine..hana lolote kacheza faulo kampa dada mimba matokeo ndio hayo dada kamganda umri huo ni wa kuamua kuzaa ?
mara 100000000000000000% nikute mwanaume ana mtoto kuliko aniletee mtoto nikiwa ndani ya ndoa ...

Pole sana dada ..nakosa hata la kusema hapa..

Huyu mama kweli anastahili pole nyingi... Sidhani kama huyu jamaa aliamua kusaliti ndoa yake au aliamua hivyo kwa makusudi yake, amevumilia kwa miaka 25, why now??... huo ni mtego, mzee kategeshewa... Mimba ikaingia... labda hakufahamishwa mapema. Na ukizingatia kwamba ana mtoto 1, ameamua asitupe damu yake. Ujue wanawake wengine wanatumia Mimba/Watoto kama vitega uchumi...
 
ndio mana nisemaga ctapokea mtoto chini ya umri wa wanangu, wa mr wa ujana wake nilienae ananitosha kabisa,chini ya umri wa wanangu waleane huko bila mie kushirikishwa kwa lolote, mtoto ana miaka 23 unakaribia kupata mjukuu then unazaa nje, na kama alikuwa anahitaji lakini mama hakupata/shika mimba hayo ni mambo ya mungu solution sio kuzaa nje....wanawake tuna kazi kubwa na hizi ndoa.
 
Poleni sana. Sasa mtafanyaje na mambo ndo yameshakuwa hivyo?
 
asante sana, ndio hivyo tena"till death do us apart".....nikikumbukaga wale waliopokea mahari yangu nashikwa na hacra kweli.
Walipokea bila ridhaa yako? Sore, tuko ofu topiki hapa ujue honey.
 
Walipokea bila ridhaa yako? Sore, tuko ofu topiki hapa ujue honey.

ndio unanipeleka ofu topik....wangeniambia kwamba kuna mashimo marefu humo mie c ningejifikiria mara mbili mbili? wao wamepokea tu na chereko kibao...
 
Saafi sana kiongozi - mtoto ni mtoto - hakuna mtoto wa nje!
Jamani jamani! Sasa na huyu mama nae akiamua kuzaa wake wa nje nae atakuwa mtoto tuu? Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni! Lolz, dada, Mungu akupe nguvu. Follow your guts mamy but take time to think.
 
Back
Top Bottom