Mume akiri kufanya kosa na aomba msamaha kwa mkewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mume akiri kufanya kosa na aomba msamaha kwa mkewe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Feb 15, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  BAADA ya kuona mke wake anamsimamo wa kuomba talaka na kumwambia kuwa ataonyesha meseji hiyo kwa mshenga ili ionyeshwe kwa wazee kama uthibitisho, mume huyo aliamua kumuomba radhi mke wake na mke huyo kurudi nyumbani kwake
  Aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuona atakwenda kudhalilishwa mbele ya wazee na kuamua kumfuata mke wake huyo alipokwenda kuishi kwa rafiki yake.

  Akiongea kwa njia ya simu mwanamke aliyekuwa anaomba talaka kwa mumewe alisema kuwa amerudi nyumbani kwake Ijumaa baada ya mume huyo kumuomba radhi na kukiri kosa hilo.

  Alisema Ijumaa wa wiki iliyopita mumewe huyo aliwasiliana nae na kumtaka amuelekeze sehemu alipo ili aweze kukutana nae, na kudai kukiri kutenda kosa hilo na kumuahidi kuwa hatorudia tena kosa hilo.

  Alisema kwa kuwa mumewe huyo alimtafuta baada ya kuona kuwa nina msimamo na talaka hiyo aliamua kumsamehe kwa kuwa walikuwa wametoka mbali na mume wake huyo.

  Alisema hadi jana siku ya kusherehekea siku ya wapendanao yaani “Valentine Day” waliisherehekea kwa pamoja wakiwa Hotel ya Blue Pearl wakipata chakula cha mchana na kudai waliamua kulala hapo ili kurudisha pendo hilo ambalo lilikuwa limeshaingia doa wiki moja nyuma.

  Hivyo alidai kuwa mume huyo kwa kuonyesha kuwa alifanya kosa hilo alimtumia ujumbe mfupi wa maneno mwanamke aliyekuwa anataka kuhatarisha ndoa yake kwa kumwambia aachane nae na amerudisha mapenzi kwa mke wake.

  Alidai mara baada ya kumtumia ujumbe huo dada aliyetumiwa ujumbe huo alimpigia simu mume wake huyo na mume wake kumtaka apokee simu hiyo na kudai aliipokea simu hiyo na kumpa vipande dada huyo na kuendelea na sikukuu yao hiyo Spesho

  Mwanamke huyo alitaka kuvunja ndoa yake baada ya kukuta ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwenye simu ya mume wake ulioashiria kuwa alikuwa ana uhusianao na mwanamke nje ya ndoa yao.

  Hivyo wasomaji hali ndivyo ilivyokuwa kwa wanandoa hao na mapenzi yamerudi upya baada ya mume huyo kukiri kosa mbele ya mkewe.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,259
  Trophy Points: 280
  ....Good for them :) Another marriage saved.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...