Mume achoma godoro na Nguo za Mama mkwe baada ya Mkewe kumkimbia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Maafisa wa polisi eneo la Kiminini kaunti ya Trans Nzoia wanamsaka jamaa mmoja mwenye umri wa makamo ambaye anadaiwa kuvamia makazi ya mamake mkwe na kuchoma malazi yake.

Amos Wanjala anasemekana kuvamia makazi ya mamake mkwe na kuchoma malazi na baadhi ya nguo zake.

Amos Wanjala alitekeleza kitendo hicho baada ya mkewe kumtoroka. Akiwa mwenye ghadhabu, Wanjala alivamia boma la Mercyline Wanyama Alhamisi, Mei 28 mwendo wa saa tano usiku, alimuasha mama mkwe na kisha kuchoma malazi na baadhi ya nguo zake.

Mama huyo alisema alipoteza mali inayogharimu zaidi ya KSh 6,000 kwenye mkasa huo na hadi kwa sasa anashangaa ni nini kilichomfanya mkwe wake kumvamia. Mshukiwa anasemekana kumtishia maisha mama huyo, hii ni kulingana na OCPD wa Kiminini Francis Tumbo.

Tumbo alisema mshukiwa akikamatwa, atashtakiwa kwa uharibifu wa mali na pia kumtishia maisha mama huyo. " Akishakamatwa, atashtakiwa kwa kosa la kuharibu mali,"

OCPD huyo alisema. Kwa mujibu wa taarifa za The Standard, mkaaji mmoja aliyetambulika kama Juma Barasa ametaka mshukiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa ajili ya kukiuka mila.

Ni kinyume na okoo ya Wabukusu kwa mtu yeyote kuwashambulia wakwe zake ama kuharibu mali yao," Barasa alisema. Mmoja wa majirani amesema kwamba Wanjala atapigwa faini ya mbuzi ambayo itachinjwa kwenye sherehe ya utakaso

kiswahili.tuko.co.ke
 
Wakenya bwana 😂😂
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom