Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,445
- 7,813
Naibu Waziri wa zamani wa Elimu na Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo leo Bungeni amesema mwaka kesho serikali itashindwa kuwapeleka watoto Form one kwenye shule za serikali kwasababu mpango wa elimu bure ulianza miaka sita iliyopita hivyo watoto waliopo leo darasa la sita ni takribani 1.8 milioni ilhali madarasa na madawati ya shule za serikali uwezo wake ni kuchukua wanafunzi laki saba na nusu.
Amesema serikali itabidi ijenge shule jambo ambalo hadhani kama itawezekana, ameiomba serikali ije na mpango wa PPP kwani shule binafsi zina kila kitu lakini zinakosa wanafunzi na nchi ni ya wote hivyo ameomba wawe pamoja.
Mulugo ame-declare interest kwamba yeye ni mdau wa elimu na mmiliki wa shule binafsi.