Mulugo: Mimi ni yatima kwa sababu ya Mamba, Serikali inilipe fidia

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Akichangia kwa uchungu na hadi kutaka kulia kwenye hotuba ya mali asili na utalii bungeni, Mulugo amesema mamba jimboni kwake wanazaliana kwa kasi sana na serikali haiwavui kama inavyotakiwa hivyo kusababisha maafa makubwa sana kwa wananchi wa jimbo lake.

Amesema yeye ni mhanga namba moja wa mamba kwa kuwa wazazi wake na ndugu waliuawa na mamba.

Anashangaa serikali kudai inalipia watu lakini watu wa jimboni kwake na yeye hawajawahi kulipwa fidia na ametaka ilipwe.

Saa hizi analia lia usiku wanawatumia kuua wenzao wenye visa nao....hao wanafiki Mamba ndio silaya yao kuu kwenye kurogana na kuuana huko Mbozi! Hawezi kuwavua maana kuna miujiza mikubwa sana kwenye hao mamba sikia tuuuu!!! Mnafiki huyo....mchawi mkubwa anajua nini anaongea
 
Mzungu: Where is Masanja?
JAMAA: Masanja iz...iz..... iz kuliwa na mamba eeeende minzi iiizi gwalaluka zazaza.
 
Akichangia kwa uchungu na hadi kutaka kulia kwenye hotuba ya mali asili na utalii bungeni, Mulugo amesema mamba jimboni kwake wanazaliana kwa kasi sana na serikali haiwavui kama inavyotakiwa hivyo kusababisha maafa makubwa sana kwa wananchi wa jimbo lake.

Amesema yeye ni mhanga namba moja wa mamba kwa kuwa wazazi wake na ndugu waliuawa na mamba.

Anashangaa serikali kudai inalipia watu lakini watu wa jimboni kwake na yeye hawajawahi kulipwa fidia na ametaka ilipwe.

Mamba wamewaua watu wengi sana Nchi hii hata kule mbugani seolue kuna ziwa na mtu rufiji mamba wanakula watu sana pia wanyama wengi huliwa na mamba pindi wakienda kunywa maji, binafsi siwapendi mamba maana wamekuwa Hatari kwa binadamu kama ilivyokuwa Nyoka aina ya Koboko kule Tabora, shinyanga, mwanza na Rukwa kidogo.
 
Saa hizi analia lia usiku wanawatumia kuua wenzao wenye visa nao....hao wanafiki Mamba ndio silaya yao kuu kwenye kurogana na kuuana huko Mbozi! Hawezi kuwavua maana kuna miujiza mikubwa sana kwenye hao mamba sikia tuuuu!!! Mnafiki huyo....mchawi mkubwa anajua nini anaongea
Mkuu ni kweli mamba hutumika kwenye Ushirikina hata pwani mto wami na ruvu wachawi huwatuma mamba kufanya yao, lakini wapo Mamba wengi sana ambao huwaua watu ama kuwajeruhi pasipo kutumwa na mtu kiuchawi, kule morogoro, hata kule iringa mtu kwenye mito watu wengi wamepoteza uhai lakini wengi zaidi wapo kanda ya Ziwa hususani ziwa victoria ambalo lina mamba wengi hakuna mfano na ndipo mamaia kwa mamia wameuawa na mamba ni vyema Serikali iwavune hao mamba wapungue kwa sababu hata mbungani wamekuwa Hatari kwa wanyama ambao ni hazina kwa Utalii.
 
Back
Top Bottom