Muleba, Kagera: Watu 56 wanusirika kufa baada ya boti kuwaka moto

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
BOTI KUUNGUA: ABIRIA 56 WANUSURIKA KIFO WATATU WALAZWA HOSPITALI YA KAGONDO- MULEBA

Abiria 56 wanusurika kifo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kutoka Kemondo Wilayani Bukoba kuelekea Rushonga Bumbire Wilayani Muleba kuwaka moto na kubadili uelekeo na kusababisha tafrani kubwa kwa abiria waliokuwemo katika boti hiyo.

Akitoa taarifa ya ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi alisema kuwa boti ijulikanayo kwa jina la Lulimbe ikiwa imebeba abiria 56 na mizigo yao ilianza safari majira ya saa 8:00 mchana Septemba 16, 2019 muda mchache baada ya kuanza safari ilishika moto gafla na kubadili elekeo kurudi bandarini ilikotoka.

Kamanda Malimi alisema kuwa katika boti hiyo yenye uwezo wa kubeba abira 84 abiria waliokuwemo 56 waliokolewa na wananchi waliokuwa nchi kavu pia abiria wengine waliweza kujiokoa kwa kougelea majini. Aidha, majeruhi watatu walikimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph Kagondo na kupatiwa matibabu ambapo hali zao zinaendelea vizuri.

Shuhuda wa tukio hilo aliyekuwa katika boti hiyo Bw. Michael Dominick mkazi wa Isamilo Mwanza alisema kuwa mara baada ya kuanza safari umbali kidogo kutoka mwaloni gafla ulitokea mlipuko mkubwa eneo la nyuma ya boti kwenye injini na kusababisha moto mkubwa uliogeuza mwelekeo wa boti kwasababu ya upepo na kurudi bandarini ilikotoka abiria wakipiga kelele kuomba msaada na wengine kurukia majini kuogelea ili kujiokoa.

Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akiwapa pole manusura wa ajali hiyo na kuzungumza na wananchi katika eneo hilo la tukio aliwasisitiza wananchi kuhakikisha wanazingatia usalama wao wakatia wa kusafiri kwa kuvaa life jacket na kwataka wakaguzi wa vyombo vya usafiri majini SUMATRA kuhakikisha wanavikagua kikamilifu kabla ya kuanza safari.

“Pia na nyinyi wananchi mtusaidie sisi Serikali kwa kuhakikisha mnavikagua vyombo hivi kabla ya safari mkivitilia mashaka toeni taarifa kwa mamlaka husika ili tuweze kudhibiti ajali hizi kabla ya kutokea.” Alisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Mkuu wa Mkoa Gaguti pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya mkoa waliwatembelea majeruhi watatu katika Hospitali.Muleba
FB_IMG_1568736656745.jpg

FB_IMG_1568736808091.jpg
 
Pole yao.
Vifaa vya kuzimia moto ni muhimu sana kwenye hivyo vyombo. Mchanga na extinguisher nyingine ili kupunguza majanga
 
Mheshimiwa alisema wazime na maji tu sasa hapo ilikuaje? Ziwa linakupwa?
 
Hizo boti nimepanda sana kipindi naenda visiwa vya Bumbire(Iroba),ndani full burudani unaweza kusahau kuwa upo majini.
Tatizo la kulipuka kwa injini ya boti hutokea pale propera zinapokuwa juu ya maji badala ya kuwa ndani ya maji kabisa.
Omukama Katonda Asimwe.
 
Back
Top Bottom