Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Mwenyekiti wa Kijiji hicho kilichopo wilayani Muleba, Rahim Kaganda, akizungumzia tukio hilo, alisema Mzee huyo alipofuka macho kwa hivyo alikuwa anatambua kwa kutumia fimbo kuzunguka ndani ya nyumba yake, kwa maana kutoka chumba hiki kwenda kingine na alikuwa na uwezo wa kutoka nje
Kaganda alisema siku ya tukio mzee Setty alitoka chumbani huku akimwambia mkewe kuwa anaenda kukojoa, akapapasa akafungua mlango kwenda sehemu ambayo alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya kujisaidia, kumbe tayari alikuwa na maandalizi ya kujinyonga ambapo tayari alikuwa ameiweka kamba yake sehemu
Sasa alipochelewa kurudi chumbani, mke wake akajaribu kumuita, akamjibu si huwa natoka kwenda kukojoa sasa unaponiita unataka nijikojolee? kwa hiyo nisubiri nikojoe narudi chumbani.
Kwa hivyo mke wake akawa na imani ya kurudi chumbani kumbe tayari alikuwa kwenye maandalizi ya kujinyonga. Hatimaye akafunga kamba juu ya paa la nyumba yake, alipomaliza akajitundika
Kaganda alisema Mzee huyo aliyekuwa Mkulima na Mfugaji alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa macho kwa zaidi ya miaka miwili.
Chanzo: Radio Free Afrika