Mukandala calls UDSM Academic Staff 'lazy and money hungry'

Bubu Ataka Kusema said:
``Time and again you have been reminded to submit revised curricula of the programmes you teach, but out of sheer laziness, deadlines come and go with no one living up to his responsibility. We currently have almost 1,200 faculties, but only about five or six faculties have submitted theirs,`` a visibly agitated VC thundered.

Anategemea nini kama hawalipwi vizuri? Kinachotakiwa ni kuwalipa vizuri ili waweze ku - concetrate na kufundisha pamoja na kufanya research ili kuweza kusaidia kuondoa umasikini wa taifa letu
 
Kuna mtu ameuliza wanalipwa kidogo ukilinganisha na watu gani?, na mwingine amejaribu kuonyeshwa kuwa wanalipwa vizuri ukilinganisha wao na mainjinia walio kwenye ofisi za serikali. Hatuna sababu ya kulinganisha Kwa sababu ni watu tofauti kabisa. Malipo ya wahadhiri si mabaya sana ukilinganisha na watu wengine waliopo serikalini. Lakini tukumbuke kuwa majukumu yao ni mazito. Ili upate uprofesa wa uhandisi unahitaji zaidi ya miaka ishirini kuanzia digrii yako ya kwanza, sasa unataka huyu mtu alipwe laki mbili?. Suala la kufundisha vyuo vingine hata ukiwapa milioni ishiri kwa mwezi hawataacha ndugu yangu, suala la msingi hapo ni kwamba wao wanatakiwa watimize wajibu wao kwanza sehemu walizoajiliwa ndiyo waende huko kwenye nyumba ndogo za dodoma, mzumbe, IFM na vyuo vingine.Kwa bahati nzuri mie ni mhandisi nimesoma udsm Engineering miaka sita pale, jamaa wanafanya kazi za nje lakini hawakosi vipindi, wanajua wajibu wao sijui huko kwingine. Na mimi sasa nafundisha kwenye hivi vyuo. Suala la msingi hapa wahadhiri wanatakiwa watimize wajibu wao na VC naye atimize majukumu yake. Ukishaona mambo yanakuwa hayo yanayotokea ujue hakuna mahusiano mazuri kati ya uongozi na wafanyakazi.
 
Infact mshahara wa lecturers kwa sasa ni mkubwa sana tena wa kutosha ukilinganisha na sector zingine za serikali. Mfano engineer kwa sasa aliyeajiliwa na serikali akiwa kwenye ngazi ya mshahara wa TGS E analipwa take home isiyozidi 300,000/= kwa mwezi !!!!! na huyo utamkuta ni engineer wa manispaa au wa wizara anayetoa maamuzi ya projects za billions of money. Sasa lecturer analipwa 1.5 million bado anasema ndogo anajilinganisha na nani?????

Mkuu hebu angalia vizuri hapo usichanganye lecturer vs engineer hivi unawaongelea wote wakiwa katika level moja? lecturer ana PHD na uzoefu wa miaka kadhaa, sasa hapo unamlingalisha na engineer wa level ipi? level ya lecturer hawezi kulinganishwa na engineer kwenye manispaa? vipi wa tanroads? na vitengo vingine?
 
hawa ma engineer manispaa wachache wana masters na inatosha wakiwa na B.Sc tu na uzoefu na wakati mwingine wana elimu ndogo zaidi mf. Kihiyo alikuwa enzi zake
 
Wandugu,

Wasomi wetu siku hizi wanalipwa vya kutosha si haba. Suala ni kuwa katika dunia hii ya matabaka wasomi nao hawako nyuma katika kutamani kuwa tabaka la juu ama WALA NCHI ama Walala hai wakati wote tunajua kuwa unapochagua kufanya kazi katika sekta ya elimu na haswa katika asasi ya umma hupaswi kuwa na ndoto za kuwa katika tabaka la walaheri...

Alichosahau Prof Mukandala, na labada alikiongelea lakini hakijaripotiwa, ni kuwa UDSM kuna tatizo kubwa la mazingira mabovu ya kufanyia kazi. Hili ndilo suala ambalo naamini kwa kutumia kipaji chake cha UJASIRIAMALI anapaswa kuja na mkakati mzuri na wa uhakaka wa kuhakikisha serikali na hata wananchi waliwahi kusomea MLIMANI wanatimiza wajibu wao wa kufinance development plans za chuo. Ukichukulia manani kuwa karibu vigogo wote serikali, katika siasa na hata sekta ya biashara ni wahitimu wa UDSM sioni ni kwanini tunashindwa kuwa na mkakati kabambe wa kuwatumia hawa KUWEZESHA ipasavyo dira ya maendeleo ya UDSM....

omarilyas
 
"Wasomi wetu siku hizi wanalipwa vya kutosha si haba. Suala ni kuwa katika dunia hii ya matabaka wasomi nao hawako nyuma katika kutamani kuwa tabaka la juu ama WALA NCHI ama Walala hai wakati wote tunajua kuwa unapochagua kufanya kazi katika sekta ya elimu na haswa katika asasi ya umma hupaswi kuwa na ndoto za kuwa katika tabaka la walaheri..."

Omarilyas, heshima yako mkuu!

Ningependa kidogo kuchangia maoni yako hapo juu!

Nadhani kuna masuala kadhaa tunayasahau sana tunapokuwa tunajadili maslahi ya "watumishi wa umma" (sijui kama kuwaita hivi bado ni muafaka) kule nyumbani.

Moja tunatengenasha matabaka mawili, walalahoi na watawala ama watu wa tabaka la juu, tunasahau tabaka la kati (middle class) ambalo kwa nchi zilizoendelea ukiwa na elimu na a decent job automatically unakua hapo, kwa Tanzania, hapana, elimu na a decent job haikuweki tabaka la kati. Kipato chako halisi (kwa mshahara ama mshahara na mbinu m'badala) ukilinganisha na kinakuwezesha kuishi maisha ya namna gani ndio kinapelekea uwe kwenye daraja fulani, so usishangae watu wa qualification sawa na kazi yenye title moja mkawa mko kwenye madaraja tofauti kabisa! Sidhani kama wasomi waliowengi nia yao nikuwa tabaka la juu, wengi wana-struggle kuwa tabaka la kati! Kuwa tabaka la kati Tanzania si kitu kirahisi, wala cha ku-take for granted ila ni kitu cha kuhangaikia!

Secondly, baada ya kupata uhuru, concept ya "real wage" haikuendelea kutumika kwa muda mrefu kama kigezo cha kupima maslahi sahihi ya wafanyakazi! Sasa hivi serikali ikipanga watumishi walipweje sijui hata wanatumia kigezo gani, but certainly si gharama za maisha! Consequently, culture ya kutafuta mbinu m'badala imejengeka sana. Mbinu m'badala kwa walio wengi si tamaa ya kujilimbikizia bali ni survival strategy, kutafuta namna ya kuishi decently katika mazingira hayo na attempts za kujenga future security! Haya yote yako mikononi mwa muajiriwa, na ni reality anayoishi nayo kila siku, awe ni mkufunzi ama any other sector! Hakuna asiyejua mtumishi ambaye hakufanya haya nini yanamkuta anapostaafu! Lakini kabla ya kustaafu, ni maisha yanamna gani anaishi yeye na familia yake ama wanaomtegemea!

Kitu cha tatu ni lazima tujue kuwa maisha ya kitanzania yanategemea sana fedha uliyonayo mkononi (cash at hand)! Kama hawajabadilisha, kwa mfano wafanyakazi wa UDSM health insurance yao ni pale health center (kwa tuliopita chuo tunapaelewa vizuri). Huduma za pale ni duni, na pia si convenient kwa watu ambao hawaishi campus! Kwahiyo hata ukiwa na mgonjwa, uwe na cash kumpeleka kwenye huduma bora! Sasa jiulize kwa gharama tu za maisha ya kila siku zilivyo, then angalia thamani ya Tshs. 1,000,000, (roughly USD 850), when you break it down kuitumia kwa mwezi mzima ni fedha kidogo kwa maisha ya daraja la kati! Sidhani kuwa kuwa mkufunzi inabidi uwe pathetic, no nadhani financial stability na security ni muhimu sana! Na mfumo mzima hautoi hiyo currently or long term! Kabla hujafikiria ku-save mshahara huo hautoshi kukidhi mahitaji ya kila siku!

Nne, nakubaliana na wewe kuhusu mazingira ya kazi kuwa ni magumu! Nakumbuka kuna mkufunzi mmoja pale alishawahi kuniambia kuwa hata computer ni desktop iliyoko kwa head wa department, hakuna mkufunzi anayepewa hata hiyo desk-top achilia mbali laptop! Kama wanapewa ni kwa hela ya mradi fulani kwenye department yao, ama some project, but never through the university! Ila wakufunzi karibu wote kila mtu anajinunulia computer yake kufanyia kazi! Hakuna hela hata ya kununua vitabu, wanasema mpeleke requests library, they never buy the books you order, university subscription kwenye journals ni very limited! So, walimu wanakisaidia sana chuo kwa kutumia fedha zao kufanya yote haya!

Tano, kuna generation sasa hivi ya watu ambao experience yao kubwa si kusoma bure, afya bure sijui nini bure, ila watu wamegharamia elimu zao, afya na mambo mengi tu, kama si wao wenyewe basi ni jitihada binafsi za kutafuta namna ya kujiendeleza na bado watu wa namna hiyo wanaongezeka, kiasi kwamba hata hiyo legitimacy ya muda mrefu ya kuwa 'tuliwasomesha' inakwisha, serikali kama hai-invest kwao kwanini wategemee hawa wajitoe zaidi kwa ajili ya Taifa!

Nadhani badala ya Mukandala kuwa na outbursts za kitoto, awatie moyo walimu wake, hata kwa ku-acknowledge kazi wanazofanya katika mazingira hayo na kuwakumbusha kuwa sacrifice wanazofanya ni kwa ajili ya Taifa. Hata kama wanasiasa wamesahau uzalendo, wao wasisahau. Utawala na walimu washirikiane kutafuta mbinu za kuboresha maisha yao, kuboresha mazingira ya kazi na kuwa wanajitahidi kwa kila namna kuhakikisha hawa-compromise quality ya elimu! The fact kuwa VC ni presidentail appointee , does not mean hawezi kuweka a working relationship na walimu! Anatakiwa kuwa kiongozi, na alichokifanya si kitu cha kiuungwana wala cha hekima, hakina tija bali kinaongeza tu gap kati ya uongozi na walimu!
 
I don't see tatizo la kufundisha more than one college. Hili swala lipo kwenye nchi nyingi tuu na ni kutakana na uchache wa walimu, however hiyo isiwe excuse ya mwalimu kushindwa kutoa muda wa kutosha kwa wanafunzi wake ( office hours), au kukamilisha paper work ambazo ni requirement kwa kila mkufunzi.

Mimi i do have friends ambao mchana nipo nao kazi na jioni wanakwenda kwenye public universities na kufundisha. Na wamefanya hivi kwa miaka nenda uje.
 
Tuwe tunajadili kwa fact,hebu tuone huyu jamaa kwa mwezi anapata ngapi? harafu tuweke hali halisi ya maisha ktk nchi hizi.

IT Lecturer / IT Teacher / ICT Lecturer
Nottinghamshire (Norfolk, East Anglia, UK, United Kingdom)

Yearly Salary: £24000 - £34000 per annum + Pension, Holidays, Training

Experienced and Qualified I.T Lecturer, with a knowledge of networking and software needed... . A lucrative salary and benefits plus excellent holidays is on offer for the correct candidate. Please don't... across the UK so if you are keen to teach we will be able to help!
Contract: Permanent
Description : Experienced and Qualified I.T Lecturer, with a knowledge of networking and software needed for a challenging and rewarding role within a top Further Education Institution.
You will be required to teach on a variety of curriculum based courses in Information Technology with the possibility of A-level ICT, Applied ICT, A-level Computing or BTEC. You should possess a degree in a relevant subject and a teaching qualification (Cert Ed / PGCE) together with knowledge of up-to-date developments in Information Technology. Flexibility and time management together with good organisational and communication skills are essential.

A lucrative salary and benefits plus excellent holidays is on offer for the correct candidate.


Please don't hesitate to send in your CV if you would like to apply or want further information. jjFOX also covers other lecturing and training opportunities, not just in I.T and Computing roles. We have similar opportunities across the UK so if you are keen to teach we will be able to help!
 
In USD as of Apr 22, 2009 20k 40k 60k
lecturer in UNITED STATES $42,000

Average lecturer salaries for job postings in UNITED STATES are the same as average lecturer salaries for job postings nationwide.
 
In USD as of Apr 22, 2009 20k 40k 60k
lecturer in UNITED STATES $42,000

Average lecturer salaries for job postings in UNITED STATES are the same as average lecturer salaries for job postings nationwide.
 
Jamani alikuwa anapresent paper kufunga Mwl.Nyerere festial week.Unajua na ulimi nao huteleza!!
 

Nadhani badala ya Mukandala kuwa na outbursts za kitoto, awatie moyo walimu wake, hata kwa ku-acknowledge kazi wanazofanya katika mazingira hayo na kuwakumbusha kuwa sacrifice wanazofanya ni kwa ajili ya Taifa. Hata kama wanasiasa wamesahau uzalendo, wao wasisahau. Utawala na walimu washirikiane kutafuta mbinu za kuboresha maisha yao, kuboresha mazingira ya kazi na kuwa wanajitahidi kwa kila namna kuhakikisha hawa-compromise quality ya elimu! The fact kuwa VC ni presidentail appointee , does not mean hawezi kuweka a working relationship na walimu! Anatakiwa kuwa kiongozi, na alichokifanya si kitu cha kiuungwana wala cha hekima, hakina tija bali kinaongeza tu gap kati ya uongozi na walimu!


Nakubaliana na wewe kabisa, Mukandala anachotakiwa kufanya ni kuakikisha kuwa pale Mlimani kuna kuwa na good working environment. Ukweli ki kwamba mishahara haitoshi. Unakuta lecturer analipwa basic salary ya 1.5m ukiweka makato kama PAYE na madeni mengine aliyo nayo anajikuta anpata Net salary ya Laki saba. sasa unategemea asizunguke zunguke kutafuta pesa?
 
Colleagues, assuming the following article quoted Prof. Mukandala, (the Vice Chancellor in the UDSM) correctly, what are your opinions?

What was he doing just few years ago? Running from one CCM office to another then back to classroom, then to CCM meetings, then etc. etc.

Mukandala is just another VC at its earliest uselessness. Living happy life, in bed with politicians instead of academic and leadership responsibility.
 
Jamani alikuwa anapresent paper kufunga Mwl.Nyerere festial week.Unajua na ulimi nao huteleza!!

Kama ulimi uliteleza aombe radhi, vinginevyo hana tofauti na Mbeki wa South ambaye aliwasahau walala hoi akajiambatanisha na wenye nazo kinacho mpata unakijua...
Sasa huyu Mkandara yeye anajiona si mwalimu wa chuo tena bali ni mtawala na hivyo kuwaona wenzie ki hivyo... ili hali anaelewa fika shida ziwapatazo!

Fikiria huo mshahara wa 1.5 akipewa nyumba chuo badala walau akae bure kama insentive wanaupunguza huo kwa 10% manake wanapunguza 150,000, na sasa wameweka bima ya afya, nayo wamkombe kama 50 alfu, hapo hujaweka payee na makato mengine, kimsingi anaondoka na kama laki 5 hivi... sasa unataka aishije maisha yenyewe ya kibongo, ukoo mzima unajua kaka/mjomba, baba mdogo ni dr. chuo kikuu, michango kila kona hasa kwa ndugu yetu dr. lazima kadi ifike, and so on... you can fill the rest!
 
Infact mshahara wa lecturers kwa sasa ni mkubwa sana tena wa kutosha ukilinganisha na sector zingine za serikali. Mfano engineer kwa sasa aliyeajiliwa na serikali akiwa kwenye ngazi ya mshahara wa TGS E analipwa take home isiyozidi 300,000/= kwa mwezi !!!!! na huyo utamkuta ni engineer wa manispaa au wa wizara anayetoa maamuzi ya projects za billions of money. Sasa lecturer analipwa 1.5 million bado anasema ndogo anajilinganisha na nani?????

Tatizo ni kuwa hapa Tanzania, wale watanzania wanaofanya kazi saaana za kujituma wakimemo Lecturers, waganga hawalipwi kulingana na muda wao. Lectuctures most of the time wanafanya kazi za ziada nyumbani(marking, kuandaa notes nk!) hapo ni usiku lakini pia wengi wao wanaonekana ofisini siku za weekend lakini zote hizi ni kazi ILA HAWALIPWI POSHO NA OVERTIME!!,

SASA WEWE UNAYEULIZA WANAJILINGANISHA NA NANI! NENDA PPF/ NSSF HAWA VIONGOZI WAO WANAJILIPA MISHAHARA YA MILION 4 NA PIA HIZI HUWAWEZESHA KUJICHUKULIA MIKOPO HADI YA MILION 80! BAADA YA HAPO KUKATA NA KUBAKI NA HELA NDOGO SANA KILA MWEZI SASA JILUZE WANAISHIJE? HAWA WANACHOFANYA SASA KI KUZUA ZIARA MBALI MBALI MARA DUBAI MARAZA HUMU NDANI NA POSHO WANAZOPATA ZINAWASABABISHA WAPATE MARA NNE YA MISHAHARA YAO KWA MWEZI!!!!


kama unaona za Lecturers ni nyingi utakufa ukijua za wengine(kama wewe ni engineer) sema ufumbuzi utafutwe badala ya kusema Lectuers wanajulinganisha na nani!

Nenda PPF utalia mwenyewe!! na hizo ni hela za mlalahoi! ambaye anakatwa kwenye mshahara wake.

Mtu mwenye diploma anakuzidi wewe engineer. Take home yake naye ni above 500,000/=


Kama hatuamuka tutakuja LIA SAAAANA!!

KUNA GREEDY KATIKA NCHI HII NA WANAFANYA KAZI KIDOGO TU!!

NINASEMA NENDA PPF PLEASE!
Nenda
 
Mkira,

In a just society..basi kuwa na fairness the way the cake inavyotumika!

Hatetewi mtu..awe Mbunge, mhadhiri, Daktari, mfanyakazi BoT, PPF au mwal. wa primary..yaani kusiwe na kupishana hivyo kwa mishahara..wote ni wafanyakazi wa sekta ya umma!!

Kila Mtz mfanyakazi ni mwanadamu na anahitaji kula, kulala, maji n.k

Mie sioni haja ya hizi tofauti kubwa hivi: Lecturer apate 1.5m-3.0m na mwal. primary 135,000 ktk nchi hiyo2 na pesa hiyo2 ya kodi?

Is it fair? Is this a kind of just society we need?
 
Mkira,

In a just society..basi kuwa na fairness the way the cake inavyotumika!

Hatetewi mtu..awe Mbunge, mhadhiri, Daktari, mfanyakazi BoT, PPF au mwal. wa primary..yaani kusiwe na kupishana hivyo kwa mishahara..wote ni wafanyakazi wa sekta ya umma!!

Kila Mtz mfanyakazi ni mwanadamu na anahitaji kula, kulala, maji n.k

Mie sioni haja ya hizi tofauti kubwa hivi: Lecturer apate 1.5m-3.0m na mwal. primary 135,000 ktk nchi hiyo2 na pesa hiyo2 ya kodi?

Is it fair? Is this a kind of just society we need?


Ndiyo maana ninasema tuamke ili haki itendeke? Kama kuna haja ya mishahara mikubwa basi mtu alipwe kulingana na ujuzi na muda wake. je hao wanaolipwa 4 milioni tunaenda nao kwenye the same market? au kuna masoko tofauti kwamba yeye kilo ya nyama anainunua kwa sh 10000?.

kwanza lazima tujiulize sntandard yetu ya maisha kwa nini iwe juu kiasi hicho is it realistic, kinachotufanya hivyo kishughulikiwe ni VAT kubwa kama alivyosema mama Kilango? au ni nini?
I absolutely agree with you upite mdajal wa kitaifa nini kifanyike ili haki itendeke inaniuma sana kuona watu wanajilipa mishahara mikubwa!!! huku wengine wakipata midogo etc!


Kwa nini mbuge adai mi 12 kwa mwezi haklafu watu wakae kimya tu! this is tax payers money!

LAKINI KWA KUWA HUMAN DEVELOPMENT INDEX YA MTANZANIA NI 0.467, MKENYA NI 0.521, UGANDA NI 0.505 KATIKA AFRICA MASHARIKI NDIO MAANA WANANCHI WAKO KIMYA HAWAJUI KINACHENDELEA NA MATOKEO YAKE SLAA ATAKOSWA WA KUMPATIA SUPPORT PALE ATAKAPOBANWA NA WABUNGE KWA KUGUSA MISHAHARA YAO!

INEGKUWA TUNA UELEWA MKUBWA HAKIKA WABUNGE NA SERIKALI WANGEKUBALIANA NA SLAA!
 
Tunavuna tulichopanda.

Watanzania tulio wengi zaidi ya 90% tunaamini fedha ni muhimu kuliko kazi.
Cheti ni muhimu kuliko elimu.
Ukiwa na fedha wewe una akili, hata wazazi wako watakusifu na kukuabudu. Kam huna fedha huna akili yeyote, mjinga mbumbumbu hamnazo.
Watanzania wengi ikiwa ni pamoja na wazazi wako watasema darasani zilikuwa zinachemka kweli lakini ndo hivyo masikini ya Mungu akili ya maisha hakuna, maana yake( Siyo mwizi, siyo mbabaishaji, hachangamki, havuti kitu kidogo, si mtu wa manuva nk).

Ukiwachunguza kwa ukaribu watu wengi wanaodhaniwa wana akili utaona dhahiri wamo kwenye makundi ya;
Wezi, wababaishaji, matapeli, watu wa kujipendekeza, wavivu, waongo na vinyonga wa tabia na mienendo, mchana Vegeterian usiku wanajichana nyama aina zote mpaka Kiti Moto.

Tulio wengi tunaamini fedha ndo kila kitu.
Huna fedha mfukoni? Hata ukitupwa jalalani utaonekana ukijaza jalala bure, hufai kukaa hata huko jalalani.

Viongozi wa kitaifa wanatafuta fedha na umaarufu kwa nguvu za kidola bila kufanya kazi yeyote ya maana. Kutwa kucha wako kwenye vikao vya kuumiza Matacko na vitambi vyao vya supu za utumbo wa kuku na chapati tu?????!
Rais Mwizi Mawaziri wezi Wabunge wezi, wanajeshi wezi Polisi wezi na wauaji, majaji wala rushwa wakubwa.
Hakuna mtu anayewajibika kwa lolote.
Wote tunawajibika kwa Mzee FWEZA.

Kwa nini Professor wa Chuo Kikuu ajitolee kufanya kazi kwa moyo mmoja?
Yeye pia ni Mtanzania anastahili kwa 90% kuwajibika kwa Mzee wetu mashuhuri Mzee FWEZA.

Nawaunga mkono walimu wote popote pale mlipo kwa juhudi zenu za Kuhastle ili msiachwe nyuma.

Ni Heri kwako wewe Prof kulaumiwa kwamba ni mvivu kuliko kufedheheshwa na umma mzima kwamba umesoma una midigirii kibao lakini mjinga( Huna hela)
 
Last edited:
hivi wanafunzi wa UD wanazo forums zao kwa sababu most that i've seem to be so dumb wanataka kuoneglea siasa za kishabiki tuu especially niokutana nao waliograduate fro social sciences ni aibu tupu!
 
Nilikuwa nasoma kwenye chuo fulani hapa juzijuzi tuu kwenye kozi ya cheti cha uzamili kwenye masomo kadhaa walimu wetu walikuwa wanatoka chuo kikuu MLIMANI ili waweze kuenda na muda walifanya kila janja kuna wakati waliunganisha madarasa yote matatu na mwalimu mmoja akafundisha mitihani wakasahihisha na kukosea kuweka kumbukumbu ikawa taabu sana kupata majibu ya ujumla ya kumaliza muhula
Wale waliopangiwa walimu hao kuwasimamia miradi ya utafiti wamekoma ubishi wamebaki wanazunguka ofisi moja baada ya nyingine walimu hawaonekani
wengine mpaka leo hawajui watapata wapi maksi zao
LAKINI KAMWE SITAWALAUMU WALIMU HAWA BORA WAMEBAKI NCHINI KWA TAABU SANA WANAJARIBU KUTOA ELIMU YAO KWA WENGINE,WALIOTENGENEZA MAZINGIRA MAGUMU KWA WALIMU HAWA NI WATU KAMA MUKANDARA KWA SABABU YEYE ALIVUNA AKIWA REDDET HATAKI KABISA WALIMU WALA WANAFUNZI WAZUNGUMZE CHOCHOTE KUHUSU MAPUNGUFU YANAYOTOKEA CHUONI HAPO
KWA KWELI ANGEJITAHIDI KUINUA HADHI YA WAALIMU HAWA WANAKUWA KAMA OMBA OMBA UTASIKIA KAMA MUNATAKA TUWAFANYIE KAZI TUAMBIENI WANAWAMBIA WATU WA CHINI KIELIMU BORA TUU WANAPESA ZA KUWALIPA NI VIPI WATU NGAZI YA UDOKTA AU UPROFESA ANAWEZA KUGEUKA AKAWA OMBAOMBA HII NI MBAYA SANA TENA SANA
AMKA MTANZANIA JALI NA HESHIMU WASOMI WAKO
 
Back
Top Bottom