Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by salisalum, Jun 11, 2012.

 1. s

  salisalum JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Tuko hapa kwenye kutoa heshima za mwisho kwa Kiongozi aliyetukuka mwanamaendeleo Bob Nyanga Mohammed Makani. MC alitoa nafasi kwa mwakilishi wa CCM kutoa rambirambi. Akainuka Mkama akazoza kama kawaida yake. Anasema Marehemu makani alikuwa mtu safi na mwenye hekima, kama Chadema wangefuata mfano wake ingekuwa vizuri sana. Halafu akasema umakini na umahiri wake unathibitishwa na ukweli kwamba Makani aliweza kufanikiwa kuwa Katibu Mkuu miongoni mwa watu tisa waliotoka kanda moja ya nchi hii. Yaani kwamba pamoja na ukanda bado Makani aliweza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu. Mkama alitaka wana msiba tuingie kwenye mambo ya kisiasa na kutuaminisha kuwa Chadema ni chama cha ukanda na ukabila.

  Mwenyekiti Mbowe kwa utulivu na hekima ya hali ya juu, wakati wa zamu yake alitoa ufafanuzi wa kurekebisha kauli hiyo akisema, ''Mdomo huumba, si vema kauli hiyo iachwe hivi hivi bila kurekebishwa''. Mbowe alianza kutaja mtu mmoja mmoja kwa wale waanzilishi wa Chadema waliokuwepo siku ile ya kumpata katibu mkuu. Ilikuwa orodha ndefu kwa kweli, katika orodha hiyo walioonekana kutoka kanda ya kaskazini walikuwa ni Mzee Mtei, Mzee Kimesera na yeye Mbowe wakati huo akiongoza vijana.

  Mkama ametia aibu sana kwanza kugeuza mahali pa msiba pawe pa malumbano ya kisiasa, pili alikuwa amevaa kofia ya kihuni kwenye hafla ya heshima na ibada kama hii, tatu kusema uongo, Nne kamdhalilisha Rais Kikwete ambaye zamu yake ilipofika yeye hakutaka kujiingiza kwenye ujinga wa katibu wake. Yeye amesema, ''Hapa ni mahali pa msiba, tumekuja kuwapa pole wafiwa na kuwaombea subira''.

  Ninashauri CCM katika uchaguzi wao mkuu wafikirie kupata mtu mwenye hekima atakayeweza kubeba dhamana ya chama badala ya kubeba aibu ya chama. Vinginevyo tutaamini kuwa Chama chetu hakiwezi tena kuaminika kupewa dhamana ya kuongoza nchi. IMEKUWA AIBU SANA.
   
 2. M

  MAKAWANI Senior Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkama hana talent ya uongozi kwenye siasa, kwanza ni mtu wa jazba na pili anaonekana siasa alijifunzia ukubwani sema tu ana bahati! Sishangai kusikia hivyo!
   
 3. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,697
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Ndio maana Mukama haingei sana, bora hata angeongea Nape. Maana Mukama inaonekana hana busara ya kutosha..
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa alitakiwa awe nyumbani kwake analisha ng'ombe! sijui kwa nini walimteua kuwa katibu mkuu! jamaa hafai hata ukatibu kata!! Vapour zote za CCM kumbe yeye ndiyo huwa anamtuma katibu wa itikadi na uenezi.
   
 5. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,846
  Trophy Points: 280
  mkama mvi nyingi kichwani lakini hamna kitu enzi zetu tulikua tunaambiwa "AKILI YAKO HAINA AKILI" ccm kama itaendela kujisifia hazina ya wazee na wazee wenyewe ni kama MKAMA, MAKAMBA na KINA MKAPA kazi wanayo
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mimi sijawahi kumuona Mukama aki kamua mimi huwa namuona na vikofia vyake utafikiri sokomoko wa kwenye gazeti la udaku la Sani
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkama hana tofauti na Nape wote wanatia kichefuchefu kabisa wakiongea. Asubuhi Nape kaanzisha uzi asubuhi na kuweka katikati maneno ya chuki, fitna na uchongonganishi.

  CCM wasiwawaangalia kwa jicho la makini watajikuta pabaya zaidi.
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Amekosea nn sasa kusema ukweli ? hakuna kitu hapo kwenye thread yako aiseee
   
 9. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hata mzee Kisumo alishalieleza hili mapema, kwamba Mkama ni Kimeo
   
 10. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Huyu mustach wake tu unaonyesha jinsi alivyo mjinga!
  Tabia zake za hovyo ikiwemo kutembea na wake za watu nidiyo ilikuwa sifa yake kuu alipokuwa jiji.

  Magamba hawana watu, kiongozi gani huyu mpuuzi hivi!
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Watanzania sasa tumepata confirmation juu nani muasisi wa siasa za kugawa wananchi kwa ukanda. Nilidhani yalikuwa maneno ya Nape lakini kwa kauli ya Mukama basi ni wazi propaganda hizi zimesukwa toka ngazi ya juu. Ni jambo la kusikitisha sana kuona Mukama anahubiri siasa za kibaguzi, siasa za kugawa watanzania na mbaya zaidi anahubiri huu upuuzi kwenye msiba - mbele ya mwili wa marehemu! Huu ni utamaduni mbaya sana na kila mtanzania anayeitakia mema hii nchi ni vema akalaani kauli ya Mukama.

  NB: Ni Mukama huyu huyu aliwatangazia watazania wakati wa uchaguzi mdogo Igunda kuwa CHADEMA wameleta makomandoo toka Libya na Pakistan ili waje kuchafua nchi! Sijui kwa nini CCM wanaona huyu mzee bado anafaa kuongoza chama!
   
 12. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,215
  Likes Received: 10,577
  Trophy Points: 280
  Aibu iliyoje..
   
 13. Makirita Amani

  Makirita Amani JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,184
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 180
  kwani nape ndio mwenye busara??
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mi nadhani Kauli yake ndio imemuumbua kuwa kumbe CDM haina ukabili muda mrefu... look here Mkani ndio alikuwa Katibu mkuu wa kwanza wa CHADEMA, ambaye ni MSUKUMA, akawa mwenyekiti MSUKUMA sasa hapo inakuwaje kuitwa ni chama cha kikabila?
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  huwa anaongea ovyo sana huyu jamaa huku akirusha mate..
   
 16. Jallen

  Jallen JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Anawakilisha kundi kubwa la viongozi wa CCM, uwezo wao wa kufikiri ndio umefikia hapo
   
 17. 255Texter

  255Texter Senior Member

  #17
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 31, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu ni uthibitisho dhahiri kwamba CHADEMA imewashika pabaya hawa magamba. Endapo kiongozi wa chama tawala anaamua kuacha decency na ustaarabu wetu wa kiafrika na kuanza kutoa mashambulizi ya kisiasa kwenye kadamnasi ya wafiwa, ujue mambo yanazidi kuwa magumu kwa CCM. Same stupidity has been written by Nape Nnauye kwenye post yake moja humu JF. CCM = Chama Mfu.
   
 18. M

  MTK JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  No wonder chama chenyewe kinaporomoka kwa kasi ya ajabu; yatakuwa maajabu ya Musa kutegemea mtu kama huyu mkama kukisaidia chama kuimarika. anyway the rule the game is "ONE MISTAKE ONE GOAL" acha waendeleee kufanya makosa ndio mtaji wa CDM.
   
 19. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #19
  Jun 11, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Unbelievable!
  Kabsa! Kwa mara ya kwanza leo namsifu Kikwete kwa uungwana aliouonyesha....
  Siasa gani hizi hadi kwenye misiba....shame on you Mkama
   
 20. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mkuu, Nape naye amekuja na ujinga huo huo!Som hapa!

   
Loading...