Mukama huwa simwelewi au nina tatizo?

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,183
2,304
Mara nyingi nikimwona Katibu mkuu wa CCM kwenye TV huwa nabadilisha chaneli mara moja kwani huwa sielewi kama anahutubia,anagombana, ni majigambo, mahubiri au amekuja pale kuchekesha kama wajukuu zake akina Masanja.

Mara nyingi naona kama hayuko serious kwani akiongea anategemea tusikilize kwa makini kama watoto wa chekechea wakisimuliwa hadithi za Sindbad baharia, abunuwasi au hadithi za hisopo.

Juzi aliniudhi alipokuwa anasisitiza kule Igunga eti wataleta maji !!!!. Kama Rostam aliyekuwa karibu na JK ameshindwa kufanya hayo kwa miaka aliyokuwa mbunge ni ndoto kwa Kafumu kufurukuta kwani ni sawa na kudanganya watu kuwa mkokoteni utaweza kubeba mzigo ulioshindikana kubebwa na FUSO. Huu ni utani hasa unaofanywa na Mukama na ni dharau kubwa si tu kwa watu wa Igunga bali kwa waTZ wote.

Kama ni kweli kwanini walisubiri wakati wa Kampeni ndo waje na hizo hoja kwani tatizo la maji limetokea baada ya Rostam kujiuzulu au lilikuwepo siku zote?

Hii inanikumbusha incidence moja wakati huyu Mukama akiwa mkurugenzi wa jiji la Dar aliwahi ulizwa na mwandishi mmoja kwenye TV jiji la Dar lina wastani wa wakazi wangapi akajibu kiurahisi kuwa " HAJUI"

Hapo anakwenda Igunga na kuwasomea wananchi kipande cha karatasi alichoandika mikakati ya uongo ili tu wapate jimbo jambo ambalo ni DHAMBI

Huyu bwana haeleweki na mara nyingi speech zake huwa na makelele na majigambo, uzushi , kujidefend, kukashifu badala ya kutoa mambo yenye contents ambazo waTZ wanataka kuzisikia ili angalau matumaini yao kwa Mafisadi yarejee.

MI NAMTAKIA MAFANIKIO KATIKA KUIZAMISHA VEMA " MV SPICE MAGAMBA" ikiwa imejaza kupita kiasi mafisadi ambao wamekataa kuachia meli ili wengine wa safiri salama na kuamua kama ni kuzama basi tuzame tufe wote wote.
 
Sio wewe tu hata mimi huwa simuelewi, lakini anaona kama anaigiza. ukatibu mkuu wa mafisadi si mchezo
 
Waulize masheikh wa mwembechai Mukama ndo alikua mkurugenzi wa jiji na ndo aliamuru wakatandikwe ndami ya msikiti.
 
Mdogo wangu siyo wewe tu!

Hili nalo ni janga la kitaifa. Yaani hotuba zake zimejaa makelele utafikiri kiziwi anaongea na viziwi wenzake!!


Jana kwenye taarifa ya habari anaongea hadi mapovu yanatoka mdomoni na huku akijua kabisa alichokuwa anakisema ni uongo uliotukuka! Haitakaa itokee kwenye uongozi wa magamba maji ya ziwa yafike Igunga. Kishapu kwenyewe hawajafikiriwa ambao nao wana ukame wa kufa mtu ndo waje wafikiriwe watu wa Igunga walioko umbali wa kilomita zaidi ya 200 kutoka Kahama au Shinyanga?


Hii fursa watu wa Igunga hawatakiwi kuipoteza kabisaaaaa! Wakipe fundisho hiki chama dhariri hiki!
 
hilo zee halina jipya ni pambe la mifisadi kwanza sina hata muda wa kulisikiliza nkilionaga kwenye kativii kangu nabadilisha chanel bora niangalie viduku kuliko kuzidisha stress kwa kuandalia mijitu isiyo na fyucha na nchi hii
 
Nasikia alianguka chooni. Ubongo ulileta tabu kidogo wakaustua.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom