Mukama awakana akina Nnauye; Hakuna atakayeshughulikiwa ndani ya siku 90!

Mukama nilimsikia katika taarifa ya habari ya usiku ya TBC1 kuwa maazimio ya kikao hayakutaja majina ya watu. Nikajiuliza kama hapakuwa na majina ya watu mafisadi wanaopigana nao wako wapi? Kama hawakuwataja kwa majina ni kwa sababu hawajawafahamu au hawapo? Maazimio yalikuwa ya nini na yalikuwa yakiwalenga kina nani?
 
Sasa nimeanza kuamini hakuna mwenye uwezo wa kupambana na mafisadi ndani ya chama hiki..
 
Chama cha magamba hawana pakutokea wamechanganyikiwa kwanzia mwenyekiti wao pamoja na sekretariati nzima hivi nani ni dodoncha nchi hii ambaye hakusikia matangazo yao huku wakitoa autimatum wakijiapiza kwamba mafisadi lazima wajivue magamba au watavuliwa,makamu mwenyekiti Msekwa aliwataja kwa majina
Mukama ni mwehu mwendawazimu na hafai kabisa kwenye hiyo nafasi wamebandua mropokaji Makamba wameingiza Mkama ambaye ni unpolished politically
cha kushangaza wataitishaje wahariri halafu katibu mkuu na katibu mwenezi wa chama wakatoa matamko mawili tofauti wakati mwanzo wote walikuwa wanaimba wimbo mmoja
hii sekretariati kweli itamsaidia raisi kuongoza nchi au ndio nchi imewekwa rehani kwa UWT ,ambao nao watatumia mchanganyiko wa kiakili na kukwama kwa CCM kwa manufaa yao
Wote tuseme CCM bye bye ,CCM bye bye mapacha watatu wako juu juu wanatikisa nchi hii kali kweli
 
mapacha watatu kweli noma wanamtisha mr president mwenye vifaru na majeshi duh this is serious tunatakiwa kutafakari kama taifa . Anaetuongoza ni kipofu hakawii kutuingiza shimoni.
 
Wakuu hivi siku tisini walizoweka zinaisha lini? Manake hizi deadline zimeanza kuwa nyingi, manake nasikia mwana nae katoa wiki moja!
 
Kwa hili la Wmukama limenifurahisha, nahisi wakati wanajivua gamba la huyu jamaa lilitoboka, afadhali ya uupuzi wa Nnauyee aliokuwa akiendelea nao kuwadanganya watanzania, huyu jamaa kazigwaya zile figure 3, hapo hakuna alichofanya sana sana, umarufu wa lichama chao utaporomoka maradufu, nashawishika kusema watz miaka mingi tangu uhuru tulikuwa gizani hatukustahili na wala hatusitaili kuendelea kuongozwa na chama kisichokuwa na mwelekeo kama hiki, kusema chama hakina mwelekeo namanisha viongozi wake hawana mwelekeo, nilitaka nione sura ya gamba jipya jamaa wakivuliwa uanachama na madaraka mengine yote walioyapata kupitia chama chao.
Mchawi unaweza ukaloga sana watoto wa wenzio wakisha utaendelea kutafuna wa ndani mwako, ndo kinachotokea kwa upande wa ccm, njia inaendelea kusafishwa kwa ajili ya cdm 2015
 
Nilipomwona Lowassa kwenye yale maadhimisho ya Muungano kule Zanzibar nikajua yamekwisha. Sio Mukama wala Nape waliompa Urais JK.
 
Teh teh wanataka kulivaa tena gamba wataliweza litawachubua limeshakauka.

yaani nawaonea huruma kweli hasa wale waliojidai kurudi CCM na wengine kufungua tawi huko Marekani kisa chama kinajivua gamba kumbe changa la macho.....hapo Mukama anapingana na Nape na huku mzee wa kaya akisema anayosema Nape ndiyo kauli za chama sasa Mukama yeye anasema ya nani???? kazi ipo CCM, gamba halijavuliwa nadhani wanalipaka mafuta liwe laini na liendelee kuwepo...
 
Nadhani akina Nnauye wanapotoka.

Kuwasingizia akina EL, RA, EC, kwamba wao ndio walisababisha CCM kupata ushindi kidogo siyo sawa, kwa sababu katika majimbo yote matatu CCM kwa ngazi zote ilishinda kwa zaidi ya asilimia 80, labda wangetafuta sababu nyingine kama ya ufisadi, hata hiyo kisheria lazima uwe na ushahidi vinginevyo inakuwa ni defarmation ambapo mtu anaweza akadai remedies.
Sio kuwasingizia, sema ni kuwaonea, kuwabebesha mzigo huo wote peke yao ni gross unfairness'kwenye collective responsibility kwani waliandaa kwa pamoja, wakagawana kwa pamoja na kusheherkea kwa kishindo pamoja, sasa kwa nini watatu tu?!
 
Wanakwepesha movie hawa, tulitaka kuona baada ya hizo siku 90 wangefanya nini!. Natamani Mukama awe amekosea ili wachukuwe hatua baada ya hizo siku, yaani movie itakuwa tamu kweli kweli. Du, wanataka kuikwepesha!.
hakuna siku tisini hapo...
 
Wanakwepesha movie hawa, tulitaka kuona baada ya hizo siku 90 wangefanya nini!. Natamani Mukama awe amekosea ili wachukuwe hatua baada ya hizo siku, yaani movie itakuwa tamu kweli kweli. Du, wanataka kuikwepesha!.
hakuna siku tisini hapo...kazi yao kupingana wenyewe kwa wenyewe...Nape jivue gamba maana kauli yako inakinzana na ya boss wako..kaaazi kweli kweli
 
Taanzaniaaaatanzaniaa,nnakupeenda kwa moyo wiote!!!,
Nchiii yanguuu,tanzaniaaa nnakupenda kwa moyo wootee!!
"ZIDUMU FIKRA ZA MJINGA(Watz wote)
 
Wakuu hivi siku tisini walizoweka zinaisha lini? Manake hizi deadline zimeanza kuwa nyingi, manake nasikia mwana nae katoa wiki moja!

matia,nadhan tuwaombe Mods waweke kabox ka countdown to 90 days,ili tuone tamko kwa waliogangania gamba la chatu wa kijani. Hata ivi Visenti kashasema kuwa yeye si gamba bali mkulu aliyewagawia magamba ndo li gamba. Ili kusovu tatizo itabidi waendelea kumiliki gamba zao!
 
Back
Top Bottom