Muitaliano MIKE BHUSTO aushangaa umasikini wa Tanzania na watanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muitaliano MIKE BHUSTO aushangaa umasikini wa Tanzania na watanzania.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Jun 24, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  "Tangu tulipoachana rafiki yangu mwaka ule tukijifunza sanaa ya michoro pale Itigi RC misheni ulikuwa mdogo sana. Sasa umekua mtu mzima hata mimi naonekana mdogo kwako. Mbona unazeeka mapema hali ya kuwa kila kitu kinapatikana katika nchi yenu? Nakumbuka tulipoachana ilikuwa mwaka 1987. Sikupata nafasi ya kuja tena katika nchi hii niliyokuwa naipenda sana. Sasa nimekuja mara hii kama mtalii. Nimepita maeneo mengi na kushudia nchi yenu ilivyo na mabadiliko pamoja na utajiri wa kutisha. Pori na vichaka pekee bila shaka ni utajiri wa kutosha. Naambiwa nchi hii ni kati ya zile zinazoshikilia nafasi za juu kwa umasikini duniani, siamini hata kidogo..naitizama Somali, Ethiopia na nyingine nyingi. Nashindwa kuelewa maana ya umasikini huu. Jambo moja tu limenishangaza, pamoja na umasikini huo. Magari yote hapa Dar es salaam yanamilikiwa na nani? Majumba ya kifahari pia?" Jamaa anashangaa kama nchi ni masikini, mbona watu wake wanafanya kufuru ya anasa? Magari ya kifahari, starehe, watu wanakesha klabu usiku kucha. Hicho ndicho alichokiona huyu bwana. Ambacho kimenifanya nikae kimya, Je umasikini wa watanzania uko wapi? Je umasikini wa Tanzania uko wapi? Au kuna tabaka la wavivu wanaolia njaa na wachapakazi watendao anasa? Haya si maswali yangu, ni maswali ya Mike Bhusto. Mgeni kutoka Verona Italy.
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Bahati mbaya sana hata kiongozi aliyepewa jukumu la kuongoza taifa la Tanzania hajui kabisa ni kwa nini Wananchi wake ni masikini.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hata Sumaye baada ya miaka hakujua anajua kwa nini Tanzania ni masikini kaka .Wazungu wanatushangaa sana lakini hukaa kimya na kuandaa mafundisho juu ya Umimi wa mtu mweusi na bongo lala na wepesi kwa fitina na majungu .
   
 4. m

  mhondo JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ni mojawapo ya maajabu ya dunia.
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Si ajabu kwa Tanzania kutowezekana linalowekana, tushangae siku likiwezekana linalowezekana.
   
 6. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  yaani ni bora kuongozwa na maiti kuliko kuongozwa na ccm
   
 7. b

  bdo JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Kwanini haukumkutanisha huyo Jamaa na akina Mwigulu, Lusinde na Wasira wamjibu mshangao wake?
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ukiangalia malighafi tulizo nazo ni kweli unachosema mtu wa nje akija hapa atashangaa kwa nini sisi ni maskini. On paper sisi tulitakiwa tuwe tunajitegemea hata misaada kutoka nje tusiombe lakini ndio hivyo tena watanzania tumelala na ni wezi wa kubwa. Angalia nchi kama nigeria, ina mafuta lakini angalia hali ilivyo kwenye ile nchi...hela nyingi zinaingia kwenye mifuko ya wachache.
   
 9. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Umenipa wazo zuri, katika ziara yake najua Gombe hajafika. Ntampeleka kwa mzee Wasi akazidishe mshangao wake.
   
 10. F

  Falconer JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Less tha 10% of the population owns everything and 90% owns nothing. Huu ndio ukweli uliopo na ukiofika dar airport, wezi wanakusibiri wakunyanganye viji hela ulivo navyo. Ushuru wanaiba, benki wanaiba, wafanya kazi serikalini wanaiba.

  Jinchi limejaa wizi kutoka juu hadi chini. Maendeleo yatakuwa wapi. Unga ndio kileo cha vijana. Majuu ukionekana na gamba la TZ unaambiwa ukae kando tunashindada na wa nigeria kwa ujuaji.

  Angalieni nigeria ilivokuwa tajiri wa rasili mali lakini nchi haina mbele wala nyuma na tanzania inafuata mkondo huo. AMKENI wenzangu.
   
 11. h

  hargeisa JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  uhasidi na majungu yt yanaondoa baraka ktk nchi hi
   
 12. p

  papillon Senior Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hata mungu anatushangaa kwa hakika
   
 13. CHIEF MP

  CHIEF MP JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 1,570
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  !!!!!.....
   
 14. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Wanatushangaa nini hao ndio Wazandiki na WAHUJUMU UCHUMI WETU wakubwa. Wanajua UDHAIFU wa Wanasiasa wetu na kuwapenyezea Rupia huku wakijichotea rasilimali zetu kwa style ya "Buffet".
   
Loading...