Muimbaji wa zamani wa Blue 3 Jackie Chandiru hoi kwa madawa ya kulevya

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Madawa ya kulevya si janga linaloviumizwa vichwa vya wadau wa muziki wa Bongo Flava, bali Uganda pia mambo si mambo.
1311771148_DSC_47_95.jpg

Muimbaji wa zamani wa kundi la Blue 3, Jackie Chandiru yupo kwenye hali mbaya baada ya kuathirika na utumiaji wa unga. Amekuwa kwenye wakati mgumu zaidi baada ya ndoa yake kuvunjika na sasa yupo rehab huku afya yake ikiwasononesha wengi.
11032055_10153249760609631_2923013444745489357_n.jpg

Yupo kwenye kituo cha Bunamwaya ambako madaktari na washauri nasaha wanamsaidia arudi kwenye hali yake ya kawaida. Waliomuona wanadai kuwa hata ngozi yake imeanza kubabuka. Amekuwa akitumia cocaine na madawa mengine.
page-1.jpg


moja kati ya nyimbo zake zilizobamba
 
Ninaanza kuhisi hii fani ya muziki ina laana ya kipekee. Haiwezekani zaidi ya asilimia hamsini ya wasanii wa muziki maisha yao 'hayaeleweki heleweki'. Yani ni kuanzia kwenye ndoa, matumizi ya madawa n.k...
Ni wakati wa kila anayetaka kuingia kwenye fani hii kujitathmini tena na tena...
 
Ninaanza kuhisi hii fani ya muziki ina laana ya kipekee. Haiwezekani zaidi ya asilimia hamsini ya wasanii wa muziki maisha yao 'hayaeleweki heleweki'. Yani ni kuanzia kwenye ndoa, matumizi ya madawa n.k...
Ni wakati wa kila anayetaka kuingia kwenye fani hii kujitathmini tena na tena...
umaarufu unakuja na pressure na expectations kubwa sana kutoka kwa jamii inayomzunguka msanii, sasa wakishindwa kuishi kuendana na huo umaarufu wao ndio wanakua frustrated na kukimbilia kujipooza na madawa ya kulevya
 
mbona wa bongo movie wako vizuri,.?.....


oh! yes wao hupambana na mikorogo...sasa nimejua kila fani na ulevi wake
 
Nimeipenda hyo. Ulevi wa bongo movie mkorogo ila Ulevi wa wasanii wa muzik ni unga aka sembe tembele bamia.
 
Aiseee...huuyu dada mzuri hivi ndo amebadilika hivi..jmn kuna nn kwenye cocain?? Mbona mastaan wanaikimbilia
 
Back
Top Bottom