TANZIA Muimbaji mkongwe wa nyimbo za Kimasai, Ole Pakuo afariki dunia.

Dr Restart

JF-Expert Member
Jul 15, 2021
3,225
16,847
Kwa masikitiko makubwa, muimbaji maarufu na mkongwe wa nyimbo za injili kwa lugha ya Kimaasai, Ole Pakuo amefariki dunia.

Ole Pakuo amefariki dunia leo mchana wa Tar 28-01-2022 katika hospital ya Rufaa ya kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Alifikishwa hapo baada ya kuugua kwa muda mfupi na baadae kupoteza maisha.

Msanii huyo raia wa Kenya, anakumbukwa sana na jamii yake kwa nyimbo zenye mafundisho makubwa ndani yake.

Ametoa nyimbo nyingi zilizobamba na bado zinasikilizwa hadi leo pasipo kupitwa na wakati.

Katika nyimbo zake aliusia upendo, kutokata tamaa, kutodharauliana, kumrudia Mungu na mafundisho mengi.

Wimbo wake wa mwisho aliotengeneza video, alimshirikisha msanii Ole Sankok, iliyoenda kwa jina la 'Osim'.

Ratiba ya mazishi yake bado haijatoka lakini bila shaka atazikwa nyumbani kwake Kajiado.

Tunamuombea kwa Mungu aipokee roho ya Mtumishi wake Ole Pakuo na apumzike kwa amani. Bwana ametoa, Bwama ametwaa jina lake lihimidiwe. Amen
 
Dah!! Pigo kubwa sana hili kwa Wamasai wenzake. Maana ndiyo waliokuwa wasikilizaji wakubwa wa hizo nyimbo zake.
 
Back
Top Bottom