Muigizaji Tino-Azimia ANGAZA Akisubiri Majibu

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Habari nilizozisoma toka kwenye gazeti la kiu la wiki iliyopita ni kuwa mwigizaji Tino alizimia wakati akisubiri majibu yake alipokwenda kupima UKIMWI katika kituo cha ANGAZA Magomeni.Taarifa ziandai jamaa alimwomba rafiki yake amsindikize ili kajue afaya yake.Habari zaidi zinadai kuwa wakati wanaenda jamaa alikuwa normal na alikuwa anapiga sana stori lakini walipofika kituoni hapo na hasa baada ya damu yake kuchukuliwa jamaa alikuwa mkimya kupita maelezo wakati akisubiri majibu.Gazeti hilo linapasha kuwa wakiwa wanaendelea kusubiri majibu ghafla wakashangaa kijana Tino anaishiwa nguvu na kuwa kama mtu anayesinzia lakini ghafla walistukia mtu anaanguka na kupoteza fahamu.

Habari ndio hiyo.Hivi ni nini hasa kilichomtisha Tino mpaka akapoteza fahamu?Je hajiamini?
 
Yes inawezekana lakini sio kwa kupima watu wanapima kila leo lakini hawabadilishi tabia zao.
wanapima kila leo wanaanza ndio maana hawabadili tabia,majibu wanawaachia madaktari hizo karatasi wawauzie wauza vitumbua wafungie vitumbua.
 
nilidhani we unasoma magazeti makini tu, kumbe hata ya umbea? loo!! kijana anastahili pongezi ingawa najua ni uwongo.
 
Kwa thread zako unazotoa nikakupenda sana nikaona huyu kiumbe ni makini sana, kifaa sana, nikatamani niwe kama wewe ingawa haiwezekani, ila liko moja lawezekana, je waweza kunioa?
 
Kwa thread zako unazotoa nikakupenda sana nikaona huyu kiumbe ni makini sana, kifaa sana, nikatamani niwe kama wewe ingawa haiwezekani, ila liko moja lawezekana, je waweza kunioa?

mboni unamtarai mwana wa mwenzio? lol
 
experince yangu kama CV yako una wasi wasi usiende angaza nenda hospitali zingine. Waelimisha rika nadhani kwao ni kicheko na mafanikio takiwmu za wapimaji wenye ukimwi zikiwa juu

-Wale jamaa wa angaza maswali yao kabla ya kupima yankujenga hofu
-Na vituo vingine vyenye kideo wakati unasubiri majibu kuna picha wanaonyesha watu waliokonda na wanavyotaabika na ukimwi.
-Wengi wakitoka kupima wanakimbia majibu utasikia majina ya kuchukua majibu yanaitwa mtu hatokei.

Huyu aliyezimia nadhani ya aliathiriwa na mazingira na maswali ya wanaojiita waelimisha rika.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom