Muigizaji Joti wa Ze Komedi apata ajali

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,793
5,372
Habari zilizotangazwa leo asubuhi na shirika la utangazaji TBC one na za uhakika zinasema Muigizaji Joti amepata ajali kwa kugongwa na gari la Ubalozi wa Ubeligiji ,Kavunjika shingo na yuko Hospital ya Moi pale Muhimbili ,More info please mnaweza kutuletea
 
nampa pole sana, niliwahi kuwa shabiki wake kitambo.
kwani siku hizi anaigiza kituo gani cha TV ?
 
Kama kweli watu wa karibu naye naomba mmpeni pole, kama mtaani kwenu kuna umbea karibu kwetu kila mtu na hamsini zake
 
eeeh!basi me mshamba duh!
kwanti mamushka therengetitherengeti humjui yule muasisi wa mwendo na miondoko ulioleta tafrani hadi watoto watano wakafukuzwa shule kule kigoma kwa kuiga mwendo wake?
 
eeeh pole yake sana,but ndo nani joti?ndugu yako dia?
n7103698221_9532.jpg


Watatu kutoka kushoto
 
Msanii nguli wa maigizo ya kuigiza, vichekesho, vituko na vibweka vya kila aina ukiwemo ubunifu wa mwendo na miondoko iliyokula chati afrika mashariki na kati ikijulikana kama mwendo wa kijotijoti, amepata ajali baada ya kugongwa na gari alipokuwa akiigiza sakata zima la jini muotesha manyoya.
Joti amelazwa kwenye kitengo cha mifupa moi, kilichopo kwenye hospitali ya taifa ya muhimbili.
Habari zaidi zinapasha kuwa hali yake inaendelea vizuri.
Mungu msaidie kijana wetu wa mdebwedo na kunyeza kizenji apone haraka.
Amina.
 
Habari zilizotangazwa leo asubuhi na shirika la utangazaji TBC one na za uhakika zinasema Muigizaji Joti amepata ajali kwa kugongwa na gari la Ubalozi wa Ubeligiji ,Kavunjika shingo na yuko Hospital ya Moi pale Muhimbili ,More info please mnaweza kutuletea

Walikuwa wakiigiza lile sakata la "manyoya" pale Salendar Bridge jana mida ya saa kumi na moja jioni, ombaomba wakawaanzishia tafrani wakati anakimbia akivuka barabara ndipo akagongwa na gari na kukimbizwa MOI
 
MWIGIZAJI maarufu wa maigizo wa kundi la Komedi Orijino, Lucas Mhavile 'Joti', amelazwa katika hospitali ya Muhimbili Kitengo cha mifupa MOI, baada ya kugongwa na gari maeneo ya daraja la Salenda wakati akiwa na wenzake, wakirekodi kipindi cha vichekesho cha Komedi kinachorushwa na Televisheni ya Taifa TBC1 kila Alhamisi.
Kufuatia uvumi uliojitokeza siku za hivi karibuni, kuhusiana na Mwanamama aliyekumbwa na sakati la kuota manyoya katika mkono wake, wakati akimpatia msaada wa fedha aliyedaiwa mlemavu 'ombaomba' katika eneo la Salenda.
Jana walemavu waliandamana hadi katika ofisi za Idara ya Habari Maelezo wakilalamikia uvumi huo ambao wanadai hauna ukweli wowote zaidi ya kuwaharibia mpango wa kusaidiwa na wenye magari wanaopita katika eneo hilo, ambpo walidai kwa sasa wenye magari wote wamekuwa wakipita eneo hilo na kufunga vioo vya magari yao.
Baada ya walemavu hao kutoka katika Ofisi hizo za Idara ya habari Maelezo, waliwakuta wasanii wa Komedi, wakiigiza tukio hilo katika eneo wanalokaa na kufanya shughuli za kuomba msaada na ndipo sekeseke hilo baina ya ombaomba na Wasanii hao lililopoanza wakati wakiwatimua wasanii ili wasiigize habari hiyo katika eneo hilo wakidai si ya kweli.
Akizungumza na Mtanzania Afisa Uhusiano wa MOI, Almas Juma, alisema kuwa Joti alipatwa na kasheshe hilo kwa kugongwa na gari wakati akiwakimbia ombaomba hao waliokuwa wakimtimua na magongo yao, huku akijaribu kukwepa magari na ndipo alipogongwa na kuumia shingo, na maeneo ya kichwani.
Naye Msanii mwenzake 'Masanja' alipoulizwa kuhusiana na hilo alida hawezi kuongelea chochote juu ya hilo. "Siwezi kuongelea lolote kwa sasa kwani nimechanganyikiwa na huu mkono wa Manyoya", ila hata Joti mwenyewe mbona anamanyoya kibao kwani we hujamuona miguuni??alisema Masanja
Mwandishi wa habari hizi alipofanya jitihada za kuzungumza na Joti, hakuweza kuongea lolote zaidi ya kusema kwa kunong'ona "nasikia maumivu makali kichwani na shingoni, na nyie nae nani kawaambia fasta namna hii?". alisema huku akinong'ona kwa kificho baada ya kukatazwa na daktari kuongea na kuwafanya wauguzi waliokuwapo eneo hilo kuangua kicheko.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom