muhudumu wa msikiti wa Babati apata tuhuma za kulawiti mtoto

ThinkPad

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,844
232
MHUDUMU wa msikiti wa Babati Mjini, Athumani Mdoe Sogora, 30, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa akiwa ndani ya nyumba hiyo ya ibada mkoani Manyara.


Tukio hilo la linadaiwa kutendwa na mtuhumiwa Novemba 6 mwaka huu majira ya saa 4:00 wakati Sogora alipomlawiti kijana huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Bonga.


Kwa mujibu wa taarifa ya polisi kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Parmena Sumary kwa niaba ya Kamanda Luther Mbutu, baada ya sala ya jioni, mtoto huyo alikuwa amelala msikitini.


Taarifa inaeleza kwamba mtoto huyo alilala msikitini baada ya kutoroka nyumbani kwao kijiji cha Bonga na ndipo saa 04:00 mhudumu huyo alimlawiti na mtuhumiwa amekamatwa na alifikishwa mahakamani Jumanne ya Novemba 11.

Jamani tumlejee Mungu ali imekuwa mbaya mno
 
..Huyu mtu inabidi apimwe akili yake kwanza katika mazingira ya kawaida utiifu katika nyumba za ibada ni mkubwa mpaka mtu akifikia hatua ya kufanya matendo machafu kama hayo kuna tatizo katika bongo yake.
 
Back
Top Bottom