Muhudumu wa lodge anahitajika dar es salaam

DARKMAN

Senior Member
Aug 23, 2012
122
85
muhudumu wa lodge anahitajika
nafasi ni reception.

atakuwa analala hapo hapo lodge na kula hapohapo
wa kutoka mikoani maana wa hapa dar es salaam ruhusa ni nyingi hatutaki.

mshahara ni sh. 100,000 kwa mwezi.

jinsi ya kuapply tuma picha yako ukiwa unaonekana mwili mzima kwenye MP yangu na namba yako ya simu tutakupigia tukikuchagua
 
hahaha! Kazi zake ni zipí je aje na mabegi maana anaelekea hatakuwa na off,na utamtambuaje km katoka mkoani?
 
.., jamani hapa wandugu kuweni na matangazo ya namna hii. Eti anahitajika anayetoka mikoani!. Mwaka 2010 chama cha vyama wafanyakazi walifanya tathimini ya kimo cha chini cha mshahara ikaonyesha kuwa inatakiwa kulipwa kiasi cha sh 315000, kwa wakati huo, kwa sasa garama zimepanda zaidi, je hicho kiasi ulichokitaja ni sawa mwajiriwa kukidhi mahitaji yake?
 
hii lodge inatafuta mke au mfanyakazi? I dont get a point jaman. Tumezoea passport size leo anataka kumuona mtu mpaka unyayo. Mmmh! I doubt if this advertiser is serious. Jaribun lakini.
 
muwe na shukrani watanzania, mtu anapewa chakula na malazi bure, sabuni na maji ya kujifulia nguo zake bure, halafu analipwa laki moja wewe hiyo ajira unaweza kutoa?
 
hii lodge inatafuta mke au mfanyakazi? I dont get a point jaman. Tumezoea passport size leo anataka kumuona mtu mpaka unyayo. Mmmh! I doubt if this advertiser is serious. Jaribun lakini.

kazi ni ya reception, kwa taarifa yako hakuna hoteli wanaajili mtu reception ambaye ni kigangwala, ndio maana ikaitwa reception nenda hoteli zote utakuta vitu vinavyokaa reception ni vya kuvutia
 
hii lodge inatafuta mke au mfanyakazi? I dont get a point jaman. Tumezoea passport size leo anataka kumuona mtu mpaka unyayo. Mmmh! I doubt if this advertiser is serious. Jaribun lakini.

naomba nimtetee mtoa mada unajua hata wewe ukitoa picha ya passpott unavyoenda kwenye interview kuna watu special wa kukuangalia wewe as wewe mwili wako na muonekano wako kumbuka ajira ni ya reception ni lazima mtu awe anavutia wateja kisura na kiumbo fikiria mtu anatoka mkoani akifika dar mwenye lodge anamkataa kisa sio umbo analoliihitaji yule mtu atajisikiaje? bor kama ni kuja anakuja mtu ambaye anajua kabisa ni mtu ninayemhitaji
 
Hii ni njia nyingine ya kutongoza na kutafuta kuwapopoa watoto wa watu, huna lolote wewe mtu wa gizani! BTW: hiyo hotel inaitwaje? Mbona wataka kuona picha za watu wakati wao hawajaiona wala kujua jina la hiyo hotel yako? Do you think this's fair? Je, ikiwa ni guest house au bar za Tandale, wakifika warudi tena mikoani? Nonsense!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom