Muhudumu wa afya na mwanafunzi wa udaktari (intern) hospitali ya wilaya Kaliua, mkoani Tabora wasimamishwa kazi kwa kufanya mapenzi wodini

MKUU wa wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora Paul Chacha amewasimamisha kazi watumishi 2 wa Kituo cha Afya Kaliua kwa tuhuma za kufanya mapenzi wodini wakiwa zamu usiku.

Akitoa taarifa hiyo juzi mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa amechukua hatua hiyo baada ya watumishi hao kulalamikiwa na wagonjwa juu ya kujihusisha na vitendo hivyo wanapokuwa zamu usiku.

Alisema baada ya kupata malalamiko hayo aliitisha kikao cha dharura cha watumishi wote ili kujua ukweli juu ya watumishi hao ambao ni Muuguzi wa kike (Mwajiriwa) na Mganga aliyeko Mafunzoni (sio Mwajiriwa) waliokuwa wakituhumiwa kufanya mapenzi wodini usiku.

Alisema baada ya kujiridhisha kuwepo tuhuma hizo ameamua kuchukua hatua ya awali ya kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi na hatua nyingine za kinidhamu ziweze kuchukuliwa na Mamlaka husika.

Alibainisha kuwa kitendo hicho ni cha utovu wa nidhamu, Mtumishi yeyote wa umma na hata sekta binafsi anapaswa kujiheshimu na kutekeleza wajibu wake kwa kufuata taratibu na miongozo ya kazi yake.

‘Siwezi kufumbia macho tabia za namna hiyo, tutaendelea kuchukua hatua stahiki kwa mtumishi yeyote asiyezingatia maadili ya utumishi katika eneo lake, huyu mmoja ni Daktari mwanafunzi, anajifunza nini sasa kama anaweza kufanya mapenzi wodini?’, alihoji.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya amemsimamisha kazi mara moja Mganga wa hospitali ya wilaya hiyo Dkt Irene Apina kwa tuhuma za kukataa kumpatia matibabu mtoto wa miaka tano na kusababisha kifo chake.

Alisema kuwa kitendo cha Mtumishi huyo kushindwa kumhudumia mtoto huyo kutokana na wazazi wake kukosa fedha za matibabu sio cha kiungwana, alipaswa kumhudumia kwanza ili kuokoa maisha yake.

Aidha Mkuu huyo pia amemsimamisha kazi Muuguzi wa Kituo cha Afya Kaliua Elias Bwire kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya utoaji mimba na Muuguzi mwenzake Austina Justin kwa kukiuka maadili ya kazi yake.

Akifafanua juu ya tuhuma hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Jerry Mwaga alithibitisha kupokea tuhuma hizo na kubainisha kuwa watazifanyia uchunguzi wa kina na hatua stahiki zitachukuliwa kwa yeyote atakayethibika kuhusika.

Aliongeza kuwa kwa Mtumishi aliyekuwa mafunzoni hayupo tena huku akibainisha kuwa hakuwa mafunzoni bali aliletwa na Shirika moja (jina tunalo) ambao ni wadau wa afya kwa ajili kusaidia kutoa huduma za utabibu.

Wakati huo huo baada ya kupata taarifa za Mganga wa Hospitali aliyekataa kumhudumia mgonjwa (mtoto wa miaka 5) kwa sababu ya kukosa fedha na kusababisha kifo chake, Mkuu wa Mkoa huo Dkt Batilda Burian ameagiza akamatwe na kuwekwa ndani wakati akisuburi hatua nyingine za kinidhamu.
 
Hapo ndiyo wamepata nafasi yakwenda kufanya kwa nafasi kabisa na bila kuingiliwa na mtu.
 
Hapo ndiyo wamepata nafasi yakwenda kufanya kwa nafasi kabisa na bila kuingiliwa na mtu.
Hilo jambo huwa ni kama laana fulani'ivi!

Tena wamesambaratishwa kwa aibu, kuna mapenzi tena hapo?

Thubutuu!

Niliiangalia hiyo video, huyo mtumishi wa kike alivyosimamishwa na DC kutoa maelezo kanyonga mdomo kwa dharau, hana adabu kabisa yaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ananyonga mdomo haoni aibu? Mie hata sijaiona, halafu maranyingi kama si zote wanaofumaniwa huwa hawaendelei kila mmoja anaenda kitafuta mwingine
 
Mkuu wa wilaya ya Kaliua, Paul Chacha amewasimaisha kazi watumishi wawili wa hospitali ya wilaya hiyo kwa tuhuma za kushiriki mapenzi hovyo wodini.

Chacha amesema awali ulifanyika uchunguzi baada ya wagonjwa kulalamikia vitendo vya wauguzi hao kufanya mapenzi wodini wakiwa zamu za usiku.

Mmoja wa wahudumu hao alikuwa kwenye mafunzo ya vitendo na mwenzake alikuwa ni mtumishi wa hospitali hiyo.

Chanzo: CG FM

======

Siku chache baada ya mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Kaliua, Irene Apina kusimamishwa kazi kwa tuhuma za kukataa kumpa matibabu mtoto wa miaka mitano, wauguzi wawili wa hospitali hiyo wamesimamishwa kazi kwa vitendo vya utovu wa nidhamu.

Watumishi hao, mmoja anatuhumiwa kufanya mapenzi wodini na daktari ambaye yupo katika mafunzo kwa vitendo huku mwingine akituhumiwa kuwa kinara katika utoaji wa mimba.

Katika kikao chake na watumishi wa sekta ya afya, Mkuu wa Wilaya ya Kaliua (DC), Paul Chacha aliwasimamisha kazi watumishi hao na kila mmoja kumpa tuhuma zake.

DC Chacha amesema kuwa baada ya kuwasimamishwa kazi, tayari kuna timu imeundwa kuchunguza tuhuma zao.

Amesema kuwa muuguzi wa afya katika hospitali hiyo ambaye jina limehifadhiwa anatuhumiwa kwa kuwa kinara wa utoaji mimba huku mhudumu wa afya akilalamikiwa na wagonjwa kufanya mapenzi wodini na daktari ambaye yupo kwenye mafunzo.

"Kama huyu mtu ni daktari akiwa mafunzoni maana yake ndio kipindi cha matazamio halafu bado mnamuacha hapo anafanya nini? Taarifa yake iende mbaya kuwa hafai" amesema Mkuu huyo wa Wilaya

Daktari huyo aliye mafunzoni anatuhumiwa kufanya mapenzi wodini ambapo inadaiwa wagonjwa wamekuwa wakikerwa na kitendo hicho na kuanza kulalamika.

Mkuu huyo wa wilaya amesema hataki kuona mambo yasiyofaa katika Wilaya anayoiongoza na kwamba hatasita kuchukua hatua stahiki lengo ni kukomesha tabia mbaya na watumishi wawe mfano kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mwananchi
Kumbe Tabora mliwapiku MOI kitambo
 
Video iko wapi kama sio uzushi
 
Back
Top Bottom