Muhtasari Wa Kesi Za Kusisimua

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
219
BAADHI YA KESI ZA KUSISIMUA (2005)

1. Mnamo tarehe 09/02/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar Es Salaam, Kikosi cha kuzuia dawa za kulevya kilichopo Dar Es Salaam kilimkamata Mtu mmoja, Mkazi wa Mwenge Dar Es Salaam akiwa amemeza pipi 59 za HEROIN tumboni mwake.Shauri hili bado liko Mahakamani Kisutu.

2. Mnamo tarehe 12/02/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar Es Salaam, askari wa kikosi cha kuzuia dawa za kulevya walimkamata Mtu mmoja Mfanyabiashara makazi wa Kinondoni mtaa wa Togo akiwa amemeza dawa za kulevya pipi 70 za HEROIN tumboni mwake.Kesi inaendelea Mahakamani Kisutu.

3. Mnamo tarehe 12/02/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar ES Salaam askari wa Kitengo cha kuzuia dawa za kulevya wakiwa uwanjani hapo walimkamata Mtu mmoja, Mfanyabiashara na mkazi wa Magomeni Usalama akiwa amemeza pipi 72 za HEROIN tumboni mwake.Kesi inaendelea Mahakamani Kisutu.

4. Mnamo tarehe 12/02/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar Es Salaam, askari wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za kulevya walimkamata Mtu mmoja Mfanyabiashara na Mkazi wa Morogoro akiwa amemeza pipi 54 za HEROIN tumboni mwake.Kesi imeisha Mahakamani Kisutu na alihukumiwa kwenda jela miaka minne au faini Tsh.600,000/=, alilipa faini.

5. Mnamo tarehe 19/02/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar ES Salaam askari wa Kitengo cha kuzuia dawa za kulevya wakiwa uwanjani hapo walimkamata Mtu mmoja akiwa amemeza pipi 82 za HEROIN tumboni mwake .Shauri hili linaendela Mahakama ya Kisutu.

6. Mnamo tarehe 14/10/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar Es Salaam, askari wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za kulevya walimkamata Mtu mmoja Mfanyabiashara na Mkazi wa Kijitonyama Dar es Salaam akiwa amemeza pipi 40 za HEROIN tumboni mwake.Kesi imeisha Mahakamani Kisutu na alihukumiwa kwenda jela miaka kumi au faini Tsh. 2,000,000/=, alilipa faini.

7. Mnamo tarehe 05/11/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro askari wa Kitengo cha kuzuia dawa za kulevya wakiwa uwanjani hapo walimkamata Mtu mmoja akiwa amemeza pipi 88 za HEROIN tumboni mwake .Shauri hili linaendela Mahakamani Moshi Vijijini.

8. Mnamo tarehe 28/11/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar ES Salaam askari wa Kitengo cha kuzuia dawa za kulevya wakiwa uwanjani hapo walimkamata ndugu Mtu mmoja Mkazi wa Ilala Chumbageni Tanga akiwa amemeza pipi 67 za HEROIN tumboni mwake .Shauri hili limeisha Mahakamani alihukumiwa kwenda jela miaka kumi na mbili au kulipa faini Tsh.1000,000/=, alilipa faini.

9. Mnamo tarehe 13/12/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar eS Salaam askari wa Kitengo cha kuzuia dawa za kulevya wakiwa uwanjani hapo walimkamata ndugu Mtu mmoja Mkazi wa Amani Zanzibar akiwa na pipi 72 za HEROIN tumboni mwake .Shauri hili linaendelea Mahakama ya Kisutu.

10. Mnamo tarehe 05/08/2005 huko uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar ES Salaam askari wa Kitengo cha kuzuia dawa za kulevya wakiwa uwanjani hapo walimkamata ndugu Mtu mmoja Mkazi wa Kariakoo mtaa wa Pemba Dar Es Salaam akiwa na pipi 44 za HEROIN tumboni mwake .Shauri limeisha Mahakamani alihukumiwa kwendqa jela miaka saba au kulipa faini Tsh 1,000,000/=,alilipa faini

KESI YA MITAMBO WA KUTENGENEZEA MANDRAX ILIYOKAMATWA HUKO KUNDUCHI

Katika shauri hili wapelelezi wa Dawa za kulevya walifanikiwa kukamata mitambo iliyokuwa ikitumiwa kutengeneza dawa za kulevya katika nyumba moja huko kunduchi Dar es salaam hapo mnamo tarehe 17/02/2001. Mahakama ililidhika na ushahidi dhidi ya watuhumiwa na mwaka 2005 washitakiwa wawili walihukumiwa kifungo cha miaka kumi jela na mali zao ambazo upelelezi ulidhihirisha zilipatikana kutokana na biashara ya dawa za kulevya zilitaifishwa na serikali ikiwa ni jumla ya magari manne.
 
Shy,

Hili jambo la watu wa madawa ya kulevy linatia moyo kama walihukumiwa kifungo na mali zao kutaifishwa.nilijaribu kufuatilia lakini baadae sikujua ilishia wapi,asante kwa kutupa habari hizi. Maana ilikuwa inaniumiza kichwa kuona watu wale walivyo kuwa wanakula maisha kwa kuua ndugu zetu na madawa hayo.
 
Back
Top Bottom