Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa masharti matatu kwa mameneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) ili kulinda vibarua vyao.
Alisema kila baada ya miezi mitatu itakuwa ikifanyika tathmini ya kuangalia utendaji wao.
Miongoni mwa masharti aliyowapa ni kuongeza mapato na idadi ya wateja wanaounganishiwa umeme katika maeneo yao.
Sambamba na hilo, mameneja hao watatakiwa kubunifu njia mathubuti za kutatua matatizo ya umeme yanayojitokeza.
“Tutaanza kuwapima kwa idadi ya watu wanaowaunganishia umeme katika meneo husika, kinyume na hapo watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe,” alisema Muhongo.
Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji aliwahakikishia Watanzania kuwa vifaa vinavyohitajika kuwaunganishia umeme vipo vya kutosha hivyo watapiga kazi tu.
Source: Mwananchi