unanitaka
JF-Expert Member
- Oct 7, 2014
- 2,178
- 1,045
Aiseee jamaa ni jembe na wanamusoma wanajivunia!!!'
Ni hiviiii, habar kutoka Musoma zinasema kuwa, Timu ya madaktari bingwa sita kutoka nchini China yawasili katika Kituo cha Afya cha Murangi, Musoma Vijijini.
Habari za kiuchunguzi nilizozifanya zinaonyesha kuwa Madaktari hao wamewasili kituoni hapo kufuatia mwaliko rasmi kutoka kwa Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Madaktari hao wamebobea katika masuala mbalimbali ambayo ni maradhi ya kina mama, watoto, koo, pua na masikio, macho, upasuaji na daktari wa maradhi yote.
Akizungumza wakati wa kuwatambulisha madaktari hao kwa mamia ya wananchi wa Musoma Vijijini waliofika kupata huduma husika, Profesa Muhongo alisema huduma itakayotolewa na madaktari hao ni bure na mwananchi hatolipia malipo yoyote.
Madaktari hao pia wametoa msaada wa madawa kwa Kituo cha Afya cha Murangi ambayo yamekabidhiwa kwa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho