Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Alituma kwa Wana Tumaini University Yahoo Group
Salaam wana Tumaini na wapenzi wa ukweli kote mliko. Tangu Amina alipofariki usiku wa juzi, mimi binafsi kama Mhariri wa gazeti la Rai, nimepokea simu na ujumbe mwingi wa simu. Nimepokea emails nyingi tu. Nimewasikia waheshimiwa, vijana kwa wazee wakiomboleza kifo chake.
Wengine kama tunavyojua wanajaribu kwa kila wanavyoweza kutaka kubashiri kwa nini Amina kafariki katika umri huu mfupi. Mimi ninajiuliza tumejifunza nini kutokana na kifo cha mwanamapinduzi huyu? Jawabu ninalolipata, ni kwamba sisi ni wanafiki.
Wakati fulani, nilikuwa kuandika makala ya ukurasa mzima katika Rai nikisema: "WANAOMPENDA AMINA, WATAMLINDA." Kwanza wana Tumaini nataka niwaeleze kwamba Amina alikuwa rafiki yangu na mshauri wake. Siku alipopata matatizo ya kuanzisha urafiki na mume wa mtu mwaka 1999 wakati huo akiwa Tambaza kidato cha tano, mimi na aliposongwa na mashutumu na majaribu mengi, mimi na mwandishi mwenzangu, Absalom Kibanda, ndiye tulimpa ushauri wa kuwaambia walimu wake.
Tulimshauri akubali na awaeleze kuwa yule mwanaume alimuingia kwa gia ya kutaka kumuoa. Akasema yeye kama Mwislam, hakuwa na kipingamizi. Amina alitoa sababu hizo shuleni, wakazikataa. Akaenda shule ya private ya Makongo. Wakati tunamshauri, alikuwa akifanya kazi ya utangazaji pale Clouds FM. Ofisi yake ilikuwa ghorofa ya tano
ya jengo la Kitega Uchumi na mimi ofisi yangu ilikuwa ghorofa ya sita. Kwa hiyo tulikuwa karibu sana yeye na mwimbaji maarufu Lady Jaydee. Kipindi hicho, alionekana kijana anayeimudu fani yake katika umri mdogo. Absalom Kibanda alimfanyia interview na kuchapishwa kwenye jarida la Wiki Hii ambalo baadaye ndiyo liligeuka jina na kuitwa Mwananchi. Wakati huo nilikuwa Mhariri Mtendaji.
Katika siku za hivi karibuni, watu wenye malengo mengi, wamekuwa wakimtumia Amina. Wakati wa vita ya biashara ya dawa za kulevya hakuwa peke yake.
Kuna kundi kubwa la wafanyabiashara mashuhuri lilikuwa nyuma yake. Kwa sababu yeye ni jasiri, walimpatia orodha ndefu sana aipeleke kwenye mamlaka zinazohusika. Siku moja Rais Kikwete alitueleza kuwa kama angeamua kuishughulikia orodha hiyo, hakuna watu wangeshikana uchawi. Anasema kwamba baadaye, iligundulika kwamba majina mengi kwenye orodha hiyo, yaliwekwa si kwa sababu ni wafanyabiashara ya dawa za kulevya. Hakufafanua zaidi lakini wengi tulijua kwamba ni vita za kibishara zinazotembea katika nchi zote zilizoamua kuukumbatia ubepari.
Kasi ya Amina ilinitisha, kama mhariri na kama rafiki yake. Nilimwita tukazungumza naye. Akaniambia kwamba hiyo ndiyo njia aliyoamua kupandia kisiasa. Niliamua kukubaliana naye lakini nikamwambia achukue tahadhari. Nilimwambia kwamba Morocco ni nchi ya kwanza kulima bangi duniani. Shamba kubwa la bangi mjini Rabat liko upande wa kulia wa njia inayokwenda uwanja wa ndege wa nchi hiyo. Bangi imepigwa marufuku nchini Morocco lakini hakuna kiongozi yeyote wa kisiasa anayekubali kuzungumzia shamba hilo la bangi wakati wakienda uwanja wa ndege kuwachukua wageni wao au hata wakisafiri.
Nilimuonya kama ni ajenda yake, aende nayo taratibu, kama siyo yake, awaachie wenye nayo. Hakukubali wala kukanusha kwamba kuna watu wanataka kupandia mgongoni mwake.
Niliamua kuandika makala ya kuwaonya wale wanaomtumia (kwa sababu nilikuwa na habari zao kamili). Amina akapunguza kuwa public, akaamua kuifanya kazi hiyo kisayansi kwa kushirikiana na polisi chini kwa chini kama alivyosema Tibaigana.
Sasa likafuata hili suala la ndoa yake na wanasiasa walioingilia kati. Hilo jambo lilikuja kwa kasi sana . Yeye wakati huo alikuwa na ambition ya kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM. Akaenda kumwomba mwenyekiti wa sasa amuunge mkono. Kwa bahati mbaya kwake Amina, Mwenyekiti huyo akakataa kwa kumwambia point blank kwamba hatamuunga mkono. Kwa bahati mbaya tena, mwenyekiti huyo alikuwa rafiki mkubwa wa mume wake. Mume wake tayari alikuwa akimhisi kufanya mapenzi na Zitto Kabwe. Amina akachanganya mambo, akadhani Mwenyekiti wa UVCCM, ndiye amemchongea kwa mume wake. Ikafuata talaka. Amina akaahidi kwenda kwenye vyombo vya habari pale Maelezo kuanika yote. Yaani kutoa dukuduku lake. Kwa bahati mbaya, wakati vyombo vyote vya kitaifa na kimataifa vikimsubiri pale, baba yake ndiye akatokea. Kwa hiyo Amina akabaki na fundo lake. (wale walioko Tumaini chuoni wanaochukua shahada ya Councelling au walimu wao wanaweza kutueleza hapa).
Kilichotokea ni depression. kwa walimu wetu wa councelling nadhani watakubaliana nami kwamba depression can disrupt, disable, and kill. In terms of human suffering, the consequences of untreated depression are beyond measure. They include loss of self-esteem, family and career disruption, chronic disability and, in many cases, death. Suicide, is the outcome of depression. Kwa wale wanaojua siku za mwisho za Amina, watakubaliana nami kwamba kilichomuua ni depression.
Wataalam wanatueleza kwamba depression inaweza kuua sawa na ugonjwa wa moyo au magonjwa mengine. Kwa mfano Dr. Joseph Gallo, wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania katika jarida la kitabibu nchini Marekani linalojulikana kama Geriatric Psychiatry, anasema kuna uwezekano kwamba depression inaingilia mfumo wa moyo pamoja na kushambulia immunity system ya mwili. Hivi ndivyo anavyosema:
"How depression increases death rates is not clear," said Dr. Joseph Gallo.
"Possibly depression makes people less likely to take care of themselves, or acts directly on the immune system in ways we do not completely understand."
Kosa kubwa alilolifanya baba yake Amina, ni kumzuia kwenda kuzungumza na waandishi wa habari. Kwa yeyote anayejua mambo haya, atakubaliana nami kwamba Amina alianza kufa siku aliyozuiliwa kukutana na waandishi wa habari. Kwa sababu tangu siku hiyo, alianza kuwa recluse. Alianza kukataa kukutana na watu na tunaambiwa alifungiwa ndani, akaanza kujinyoa nywele, na wakati mwingine kuwasahau hata marafiki zake.
Kwa nini nasema sisi ni wanafiki? Nasema hivyo kwa sababu kulikuwa na uwezekano wa kuokoa maisha yake. Jamii haijajiandaa kuwasaidia vijana kutimiza malengo yao na kuvivuka vikwazo vya kimaisha. Amina amekuwa akipambana na mambo mengi ya maisha. Najua hivi kwa sababu ingalau najishughulisha na matatizo ya vijana. Wakati magazeti ya Shigongo yamemwandama kumchafulia jina, jamii ilikaa kimya. Amina akawa analia wakati akiwa chumba cha habari cha Clouds, watu wanasema shangingi huyo.
Leo ni wale wale wanaomsifu na kumwagia sifa. Napenda kumaliza kwa kusema
Amina hajafa. Waliokufa ni sisi tunaodhani tuko hai. Sisi wanafiki wa kupeleka maua kwenye majeneza wakati tungeweza kutoa maua hayo kukamilisha azma yake ya masha. Aliyekufa ni mwenyekiti wa CCM na Katibu Mkuu wake waliokataa kusuluhisha mgogoro wake wakidai ni wa kifamilia. Aliyekufa ni Spika wa Bunge aliyesema mambo ya Zitto na Amina hayalihusu bunge lakini sasa wanatoa ndege ya serikali kwenda kwenye mazishi. Aliyekufa ni mtuhumiwa Zitto Kabwe ambaye pamoja na kuendelea kukataa hadharani, alikuwa akiendelea kuwasiliana naye kwenye simu. Aliyekufa ni Shigongo na magazeti yake ambayo hata baada ya kufariki, waliendelea kuandama maiti yake kwa kutumia vyombo vyake vya habari. Amina hajafa na ndiyo sababu amepumzika siku ya kupiga vita dawa za kulevya; njia aliyoichagua kumjenga kisiasa.
muhingo