Muhingo Rweyemamu abwaga manyanga New Habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhingo Rweyemamu abwaga manyanga New Habari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Jan 28, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Muhingo Rweyemamu, Mhariri Mkuu (ME) wa Magazeti ya New Hadari Corp na boot licker number one wa RA ametangaza rasmi kubwaga manyanga kutoka kampuni hiyo,

  Ametangaza leo asubuhi katika kikao cha post mortem kwa kusema kuwa anachukuwa likizo ya mwezi mmoja, na baada yahapo kazi basi. Amegusia kwamba anatarajia kuanzisha kituo cha redio huko Iringa.

  Kuacha kwake kazi kumetanguliwa na kuyumba sana kwa kampuni hiyo, kiutendaji na kifedha. Alikuwa haelewani na Mtendaji Mkuu (CEO) aitwaye Bobby, mwenye asili ya Kiasia, kwani Muhingo aligundua kuwa u-ME wake si wa kifedha, masuala ya fedha yanathibitiwa na Bobby, na wahindi wengine waliojazana hapo, ambao hawana habari kabisa na masuala ya editorial ambayo ndiyo hasa huzalisha pesa.

  Muhingo alisikika akilalamika kuwa sasa anafahamu kwa nini Rosemary Mwakitwange – CEO aliyemtangulia Bobby na ambaye alikuwa kipenzi kwa wafanyakazi – alishindwa pia kuelewana naye. Hata hivyo Rosemary aliposhika madaraka ya u-CEO, Bobby alipewa kazi ya u-Financial Manager, lakini mama huyo aliweza kumtimua kutokana na wizi wa fedha, na mambo yakawa mazuri kabisa, mishahara tarehe 26 kila mwezi. (sasa hivi ni tarehe 45 hadi 50).

  Rosemary alilazimika kuondoka kutokana na editorial policy ambapo mmiliki, RA alisisitize iwe ya kumsafisha na kumjenga yeye RA na EL kutokana na kashifa zao za ufisadi. Hapo ndipo magazeti yakaanza kuanguka kimauzo, ingawa RA mwenyewe alikuwa hajali hilo kwani ma-boot licker wake aliowaweka na kuwalipa vizuri walikuwa wanatimiza malengo yake.
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kumekucha!.....

  i hope sio ''CCJ in the making''
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Jan 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nikiwa Dar es salaam miaka minne iliopita niliwahi kuongea na Muhingo, juu ya kuanguka kwa Habari Coorp wakati huo ilikua bado haijachechemea sana, alinibishia, akasema kuwa kuyumba kwao ni kwa kipindi tu , na kumesababishwa na targeted leaders wa magazeti yao, ambapo mwanzo waliwalenga wale ambao walikua hawaipendi serikali, (kumbuka Habari coorp ya Jenerali Ulimwengu na wenzao) sasa wanawawinda wasomaji wapya, wale wenye mlengo wakati, ambao wanatamani kuona watawala wakisifiwa sana na kukosolewa kiasi kidogo na kwastaha.

  Hakujua mabadiliko yalikua yakiendelea kinyume na matarajio ya wanataaluma wahabari pale Kijiweni.

  Kifupi Muhingo ni Editor aliekua akipenda kulambalamba sana kizazi cha mafisadi, amekua akipendwa sana na wapambe wa RA kwa namna anvyowapamba kupitia magazeti ya taasisi hiyo.....otherwise amevuna alichoshiriki kukiasisi , kukipanda.
   
 4. k

  kisikichampingo Senior Member

  #4
  Jan 28, 2010
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huenda sasa tusoma magazeti yao. Mimi huwa naboreka sana uandishi wa habari wa ku-target au ku-wasafisha individuals. Bado Mwanahalisi na Tanzania Daima. Yaani kabla hata hujanunua gazeti, msomaji umeshajua kwamba heading itakuwa; Lowassa.... au Sitta.......n.k
   
 5. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nilidhani RA ni smart sana (katika maeneo yake), ila kwa kampuni ile amechemsha. Nataka kumuelewa, may be hana nia na lolote katika fani ya uandishi wa habari zaidi ya kuyatumia kisiasa tu.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  Tanzania yetu. RA ana-play part kubwa sana ila mwisho wake waja.
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Jan 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  situ kisiasa bali RA aliamini kwa kudhibiti chombo cha habari chenye nguvu angeweza kupambana na wale wote anao waona ni maadui zake, alijisahau kua watu hawapendi kusoma habari za kumsifu JK, SERIKALI na wazembe wengine . maana ipo wizara ilio najukumu hilo(wizara ya habari, na kitengo cha habari Ikulu )
  RA ni fisadi kweli, kimkakati na kivitendo, kifikra na kutafuna uchumi wa taifa hili.
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Sasa natarajia Muhingo ataanza kurejesha makali yake na kuwa 'Muhingo' tuliyemfahamu. Kina Manyerere nao vp?
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Jan 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  INVISIBLE, Muhingo anaweza kurudi kwenye makali yake, lakini hataaminika kirahisi, maana alikubali kusaliti Watanzania kwa vipande vya noti, alikua mwokozi leo amekuwa Yuda/msaliti.

  Manyerere yupo anasaka mkate wake kwenye vigazeti vya karamagi, hana tofauti na mwanamke malaya pale kinondoni makaburini ambaye anauza utupu wake kwa vijisenti .
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,549
  Trophy Points: 280
  Muhingo na Manyerere ni macomredi wa damu ya Baba wa Taifa, Mwl.Nyerere, ila wakaendekeza njaa kwa kujiunga na timu ya JK kwa payrol ya RA na wakati muungwana akigombea ile 2005, ni Muhingo ndie aliratibu waandishi akizunguka Tanzania mzima, huku Salva na timu ya jikoni wakipigilia misumari.

  Nilitegemea naye angeitwa magogoni.

  RA kweli anapesa lakini Habari Corp imekaa mkao wa kifo kifo, hivyo Muhingo ameona mbali ameamua kuanza mbele. Kama mzee 'Maxwell wetu' mwenyewe ameyumba, itakuwa kina Ruppet?.

  Ila pia wajameni, hizi njaa hizi kwenye tasnia ya habari, zitatuua, Kama Muhingo kaachia, Comredi Jacton, usisubiri mpaka jahazi lizame, wala usiendekeze njaa, anza mbele wakati kabla bado, kifo cha mafisadi chaja!.
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu Nguvumali, nakusoma sana tu. Naamini waandishi wanaosifiwa kwa uandishi wao wanajifunza kitu tokana na andishi hili. Mwingine aweza tafsiri atakavyo lakini kwangu najifunza kitu kikubwa katika maandishi yako mkuu. Shukrani kwa bandiko lako na kunifahamisha aliko Manyerere, ndio 'Sauti Huru'?
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Jan 28, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Jacton hana aibu wala haya, ni mtu wa hovyo kabisa.
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuwa mwaka mwingine wa neema umekuja bado mtu anakimbia chaka lake! Miaka hii michache tumepitia mambo mengi sana ambayo yamewafanya baadhi ya watu wawe very exposed na kupoteza focus ya yale waliyozoea kuyafanya.
  Ila tunavuna tunachopanda hilo wala silishangai1
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu Ndahani,

  Unamaanisha anafanya hivi kwakuwa 2010 imefika?
   
 15. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,748
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  Siamini kwamba muhingo ametoka kwa jema... ni kafulia kutokana na expectations; vilevile tutambue kwamba ile camp ya burushi ya mamvi kwa mtazamo wa nje zinahitaji ujasiri wa hali ya juu kuziremba

  Muhingo, yule mjita wetu aliyekimbilia south baada ya texas, (na sasa Guardian editor) ni watu wanaopima upepo... wamesahau zama za kumsifia "kasimu" upate bia zinaelekea ukingoni

  kuna usemi usemao "mtoto mtembezi atakula miguu yake" Muhingo... kanyaga twende baba!!!!!!!
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama amepatia huko aliko Jackton. kwa mujibu wa bodi ya uhariri ya gazeti la Mtanzania, jackton ni Mhariri wa habari Mwandamizi wa gazeti hilo. Sidhani kama ndilo analomaanisha kuwa ni la Karamagi.
  Na kwa wale tunaomchambua Muhingo, ingekuwa vema kama tungefanya homework na kumjua mtu huyu vema la ya ku-comment juu yake... ni ushauri tu
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Jan 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Safi; bado najifunza. Naamini wengi tunapata taarifa za aliko Manyerere. Wakuu hawa mpaka tushawasahau kabisa! Hawasikiki mkuu Mpita Njia, kama wamepigwa ganzi vile
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sasa hivi yuko Dodoma, anaripoti Bunge kwa niaba ya gazeti lake-Mtanzania
   
 19. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwangu binafsi mwandishi huyu wa habari ni uthibitisho halisi wa waandishi chumia tumbo, asiye na maadili na mwenye kusujudia pesa hata kama inabidi kuuza utu na uhuru wake.

  Kwangu mie mwandishi huyu anawakilisha uozo uliopo kwenye taaluma hii. He will not be missed!
   
 20. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  RA unawatesa watanganyika.

  Shoga yangu anafanya hapo ananiambia mwisho wa mwezi umefika na hakuna hata dalili. Mambo ni magumu haswa na wanamkumbuka mwakitwange sasa wanasema enzi zile mshahara ungekuwa tayari.

  Ila pia wanasema mhingo afadhali aende manake alikuwa anatumia cheo chake kutisha waandishi wa kike na kawazini kwelikweli
   
Loading...