Muhindi kanipa Ajira lakini mkopo wa nauli na lunch hadi tarehe 15 kanitosa. Nifanyeje?

EdwardC8

Senior Member
Nov 2, 2017
181
257
Wakuu,

Nimepata ajira kwa muhindi tena nafasi nzuri tu kwenye kampuni kubwa, ila nikamwambia naomba advance hata ya elfu 50 kwaajili ya nauli na lunch, kawaka vibaya anasema hatoi hata 100! Nimecheki na staff wengine kwamba jamani eeh, nikicalculate usafiri na lunch hadi tarehe 15 mwezi huu napata kama elfu 50, mtu anikopeshe then ntampa 60 au 70, kila mtu kilio. Wadau nifanyeje maana hapa ninapoandika sina hata 100 na jumatatu niwe kazini kama kawaida!
 
omba kwa ndugu jamaa na marafiki wakutoe.kama unakuaga muaminifu kwenye kulipa utapewa tu.pole sana ,Mahindi wana roho nyeusiii
 
Wahindi ni shida.

Nilikua mtunza bustani wa hoteli moja ya wahindi lakini nilifanya hadi kazi za kutengeneza milango na makochi, mara kuzibua vyoo yaani vululu vululu.

Halafu sasa, muda wa kuingia unajulikana ni saa moja kamili kutoka haijulikani ukileta masikhara unatoka usiku wa manane
 
Mh mkuu toa wasiwasi shida hazina baba wala mama twambie kabla ya kazi ulifanya nini mtaan?? Na hapo kwa mhndi utakuwa unajishugurisha na nini??
 
Wakuu,

Nimepata ajira kwa muhindi tena nafasi nzuri tu kwenye kampuni kubwa, ila nikamwambia naomba advance hata ya elfu 50 kwaajili ya nauli na lunch, kawaka vibaya anasema hatoi hata 100! Nimecheki na staff wengine kwamba jamani eeh, nikicalculate usafiri na lunch hadi tarehe 15 mwezi huu napata kama elfu 50, mtu anikopeshe then ntampa 60 au 70, kila mtu kilio. Wadau nifanyeje maana hapa ninapoandika sina hata 100 na jumatatu niwe kazini kama kawaida!
Karibu tunatoa mikopo ya dharura tukikikabiliana unapata pesa papo hapo
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom