Muhindi ageuza kibao

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,847
Miss World leo, Lundenga lawamani

na Janelisa William
Tanzania Daima

HUKU fainali za kumsaka Mrembo wa Dunia ‘Miss World’ zikifanyika leo mjini Sanya, China, mwakilishi wa Tanzania katika shindano hilo, Richa Adhia ameitupia lawama Kamati ya Miss Tanzania kwa kushindwa kumtumia DVD, hivyo kumkosesha taji la Beauty with Purpose.
Alisema kukosekana kwa DVD hiyo iliyokuwa ikionyesha kazi za kijamii alizofanya akiwa Miss Tanzania, kukamnyima alama muhimu ambazo zingemsaidia katika kuwania taji hilo, hali ambayo imemvunja moyo.

Alipoulizwa kwa simu ni vipi hakuondoka na DVD, Radhia alisema hadi anaondoka, Kamati ya Miss Tanzania ilikuwa bado haijakamilisha kutengeneza DVD hizo, hivyo akaelezwa atangulie, watazituma.

Radhia alisema, siku chache kabla ya shindano hilo la Beauty with Purpose, alipowasiliana na Kamati ya Miss Tanzania, akaelezwa kuwa kwa bahati mbaya, wameituma DVD hiyo Uingereza.

“Hii imenivunja moyo, nilipowasiliana na Mratibu wa Kamati ya Urembo Tanzania, Hashimu Lundenga, akanieleza amekosea kutuma DVD, kwani badala ya kutuma Sanya China, akatuma Uingereza,” alisema.

Mrembo huyo pia amelalamika kitendo cha kamati hiyo kumtelekeza kwani mbali ya mama yake aliyemsindikiza katika shindano hilo, hakuna mwingine aliyekuwa amemsapoti.

Wakati hali ikiwa hivyo, mrembo huyo wa Tanzania pamoja na wenzake zaidi ya 100, leo atakuwa akiwania taji la dunia, Miss World 2007 katika shindano ambalo mwaka huu, kwa Tanzania limekosa msisimko.

Shindano hilo litakalofanyika katika Ukumbi wa Beauty of Crown Theatre, linatarajiwa kuwa la ushindani mkubwa kwani kila mshiriki atakuwa akitaka kulitwaa taji hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Miss World, Julia Morley kwa upande wake amesema mrembo atakayetwaa taji hilo leo, atatembelea nchi zote zilizo na washiriki ikiwemo Tanzania katika kuhamasisha jamii kujikinga na ukimwi.

Warembo wengine waliowahi kuiwakilisha Tanzania katika shindano hilo na miaka yao katika mabano, ni Aina Maeda (1994), Emily Adolph (1995), Shose Senare (1996), Saida Kessy (1997), Basila Mwanukuzi (1998) na Hoyce Temu (1999).

Wengine ni Jacqueline Ntuyabaliwe (2000), Happiness Magese (2001), Angela Damas (2002), Sylvia Bahame (2003), Faraja Kotta (2004), Nancy Sumari aliyepata mafanikio kwa kuwa bora Afrika ‘Miss World Africa’ mwaka 2005 huku wa mwisho akiwa ni Wema Sepetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom