MUHIMU: Yanayoandelea kuhusu Miswada ya Uchaguzi

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
WanaJF

Naomba niwape mrejesho muhimu kuhusu mchakato wa majadiliano ya miswada ya sheria ya uchaguzi unavyoendelea.

Mtakumbuka kwamba Desemba 11 Waziri Mkuu alichapisha kwenye gazeti la serikali(government gazette) miswada miwili: Mosi, wa Marekebisho Mbalimbali ya Sheria za Uchaguzi( Miscellaneous amendments), Pili; Sheria ya Fedha za Uchaguzi(Elections Finance Act 2009) na tarehe 22 mwezi huo huo Katibu Mkuu wa Wizara husika akatoa tamko kwa umma pamoja na tangazo kwenye magazeti ya umma.

Jana tarehe 13 Januari gazeti la Raia Mwema lilikuwa na habari hii ifuatayo ya kiuchambuzi kuhusu muswada husika: http://raiamwema.co.tz/news.php?d=1971

Leo tarehe 14 Januari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa imeitisha majadiliano na vyama vyote vyenye usajili wa kudumu kuhusu miswada husika.

Kesho tarehe 15 Januari Taasisi isiyo ya kiserikali ya TADIP imeandaa mjadala wa wazi wa umma ambao yoyote anaalikwa kujadili muswada husika utakaofanyika Dar es salaam International Conference Center(PPF Tower) kuanzia saa 3 mpaka 10 jioni.

Wiki ijayo kuanzia tarehe 18, 19 Januari Kamati husika ya Bunge itajadili Miswada husika; kwa mwelekeo wa mambo ulivyo inalekea serikali imedhamiria miswada hii ipitishwe kwenye mkutano wa bunge wa sasa. Hivyo, ni muhimu tukaongeza kasi ya kujadili ili wabunge na watawala wazingatie maoni ya wadau na wananchi wakati wa majadiliano yanayoendelea kuhusu miswada hii muhimu kwa demokrasia na maendeleo ya nchi yetu.

Hii ni fursa ya ama kurekebisha hali ya mambo kuwezesha uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 uwe huru na haki ama kuongeza vikwazo vya ziada vya kuzuia mabadiliko katika taifa letu.

JJ
 
John,

Nimesoma mahala kuwa watu wanataka mabadiliko ya mfumo. Hapa ndo pake, nasikitika sana sitaweza kuhudhuria any of them.
 
Back
Top Bottom