Wamemvisha mbuzi suti na kuwaambia watanzania kuwa huyo ni mtu, sis itunasema SIYO MTU.
Hakuna shaka kuwa watanzani wengi wenye mapenzi mema na nchi hii wamefuatilia kwa karibu sana pilika pilika za uchaguzi tangu kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura, kampeni, kupiga kura mpaka kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Katika uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, lakini ushindi ninaoufahamu mimi ni ule utokanao la na fair play, yaani kuzingatia kanuni zoote za mchezo husika.
Uchaguzi wa Tanzania umekuwa na kanuni zisizojulikana ambapo kuna kanuni jambazi zinazotumika kumfanya aliyeshindwa kutangazwa mshindi.
Kwa wale walioshinda kihalali nawapa pongezi na wale walioshindwa kilahali nawapa pole ila nawaomba wasife moyo. Wanaoniudhi ni wale wanaojua fika kuwa wao hawakushinda uchaguzi lakini kwa hila na mabavu wameamua kujitangaza kuwa washindi. Hao ndio mbuzi wangu. Watu wenye uchu wa madaraka ambao kwao cheo sio dhamana bali ni kichaka cha kufanya uovu. Wana-matabasamu mia mbili kidogo huku moyoni wakijua wazi kuwa ni wafiki. Wanatulazimisha watanzania tuamini kuwa wao ni binadamu ilhali wakijua kuwa ni mafisi-simba. Wamevaa suti na wamejipulizia pafyumu ili tuamini kuwa wao ni watu, sisi tunawaambia kuwa sio watu. Hata kama wakijipaka lipstick midomoni mwao sisi tunawaona kama mashetani kwani tunajua fika kuwa ni mbuzi, si watu.
Tume ya uchaguzi wa Tanzania, mmemvisha mbuzi suti na tai na kutaka kutuaminisha watanzania kuwa ni mtu, nasi tunasema siyo MTU.
Yeyote aliyejipa ushindi kwenye uchaguzi huu ilhali anajua hakushinda, SIYO MTU ni MBUZI.